DC aongoza upandaji wa miti 1000 Rungwe ndani ya siku moja, aahidi Mbolea ya Ruzuku kuendelea kusambazwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu ameongoza zoezi la Upandaji miti katika Kijiji cha Ijoka, Kata ya Mpombo Halmashauri ya Busokelo ikiwa ni hatua muhimu ya kulinda vyanzo vya maji, kudumisha uoto wa asili, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Jumla ya miti 1000 imepandwa leo Februari 6, 2023 katika eneo hilo huku malengo yakiwa ni kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Haniu.jpg
Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho, Haniu ameagiza wakazi wa eneo hilo kuhakikisha wa wanapanda miti mara kwa mara sambamba na kuepukana na tabia ya ukataji miti hovyo, kuchoma moto, kulima kando ya vyanzo vya maji na kuchunga Mifugo kwenye hifadhi za maji.

Aidha, amewahakikishia wakazi wote wa Wilaya ya Rungwe kuwa Mbolea ya Ruzuku imeendelea kusambazwa katika maeneo yote kwani Serikali kupitia Wizara ya kilimo imeboresha mazingira ya Kilimo na hivyo kila mkazi atapata pembejeo hiyo muhimu kwa maendeleo endelevu nchini.
Haniu zungu.jpg
"Niagize kila kata kuwe na ratiba maalumu inayoonesha ni lini mbolea inaletwa katika kata husika ili kuwaondolea adha wananchi kufuata huduma umbali mrefu huku wakipoteza muda mwingi wa uzalishaji," ameagiza Haniu.

Pamoja na hiyo ameagiza mawakala wote wa usambazaji wa Mbolea kuacha kuuza mbolea kwa magendo kwani kufanya hivyo kunaondoa nia njema ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Watanzania wanazalisha kwa tija na maendeleo bila vikwazo vyovyote.
Ha.jpg

Panda.jpg
Katika hatua nyingine Haniu ametoa maelekezo kwa wazazi wote kuhakikisha watoto wao waliofikisha umri wa kwenda shule sambamba na kujiunga na kidato kwanza wanawapeleka mapema kwani kufanya hivyo itasaidia kupata huduma hiyo muhimu kwa Ustawi wa Mtoto.

Halmashauri ya Busokelo imeandikisha watoto wa darasa la kwanza na wali kwa zaidi ya asilimia 100% huku uandikishaji ukiendelea.
 
Miti wanapanda,wanapiga picha aaafu wanaitelekeza. Mwakani tena watarudia hiki hiki maisha yataendelea km kawaida.
 
moja ya chanzo cha kupungua maji ya mto ruaha ni kupanda miti ya kigeni nyanda za juu kusini na kuondoa au kutoendeleza miti ya asili ambapo miti mingi ya kigeni matumizi ya maji ni makubwa
Ni kweli Mkuu tatizo idara zinachanganya kati ya Forester na Botanist namna ya kuwatumia....
Botanist ni mtu muhimu sana kwenye Landrestoration...natural Forest
 
Back
Top Bottom