Nani huyo aliemfukuza kazi DC ? Najua mtasema ni Mheshimiwa Kikwete au sio ?
Kwa nini amemfukuza kazi ? Kwa sababu Dc ametoa amri ya kuwachapa viboko watu wazima walimu waume kwa wake hadharani.
Ila ijulikane tu aliewachapa viboko ni askari polisi(Sijui ni polisi wangapi walishirikishwa katika zoezi hilo ,panahitajika uhalisia wa polisi walioshiriki) ,hapo hakuna ubishi.
Je amri aliyotoa DC inamtazamo kisheria katika taratibu za kipolisi ? Ndio ni amri.
Je polisi anayohaki ya kukataa kama ataona alichoamrishwa si haki na ni kuvunja sheria kwa mujibu wa kazi zao ? Polisi anayo haki ya kukataa.
Je kumuadhibu polisi huyu inafaa au haifai ikiwa itaonekana amevunja taratibu za kipolisi ?
Naomba majibu ya masuala hapo juu japo ,pataonekana pana majibu mimi nimeyaweka kama majibu hewa.
Sasa nikigeukia taarifa za Ikulu au za Wakubwa.
Mmoja alitoa jibu la papokwa papo ,DC akapimwe akili. kidogo linaelekea ,kwa nini hakuamrisha polisi wamkamate au wampeleke hospitali kama ni hatua ya kwanza ? Inawezekana kabisa historia ya DC huyo kuwa aliwahi kuugua ugonjwa wa akili pengine Maleria na Tz ipo maleria na huwajia watu juu ikawa ni patashika.
Ikiwa atapimwa na kuonekana Mheshimiwa Dc ana/alikuwa na matatizo ya akili basi ni wazi kabisa kitendo cha kumfukuza kazi kitakuwa ni kumdhulumu na Raisi wetu alichokosea ni huko kuamua moja kwa moja kuwa amemfukuza kazi au sijui kumsimamisha.Natumai kuna haja ya kufikiria kwani kitendo cha DC na Raisi vitakuwa havipishani,natumai nitaeleweka hapo ,ni dhahiri kabisa yule aliesema akapimwe akili atakuwa yupo kwenye mstari mzuri tu wa uongozi ,au sivyo wandugu wa JF ? Na wale wote waliosema achukuliwe hatua watakuwa hawana tofauti na DC ,wote zimewashoti.
Nakubaliana kuwa Raisi anapower zinazomruhusu kutoa maamuzi. Sawa na iwe hivyo ,ila nakumbuka aliwahi kumfukuza mtu mmoja kazi nafikiri alimtaka ajiuzulu au alimfukuza direct sina hakika ya hapo ,na baadae Rais huyu huyu akafikia kujutia kile kitendo. Ndio hapo ,amemfukuza DC ,DC ametenda kosa ambalo linaonyesha kuna matatizo ya akili.
Msemaji kutoka ofisi ya waziri Mkuu Bwire amenukuliwa :- Rais alisema kulingana na taratibu, kamati za nidhamu za wilaya na mikoa ndizo zenye majukumu ya kutoa adhabu kwa wafanyakazi wa umma kama ikionekana inafaa na kwamba kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya kimekiuka kanuni hiyo.
``Amevunja kanuni na ameidhalilisha ofisi na mamlaka ya ukuu wa wilaya,`` sehemu ya taarifa hiyo ilisema kama ilivyosomwa na Bwire
Hapa katika maelezo ya Ikulu kuna utata ndani yake inataka usome kwa makini na uelewe alichokisema Raisi.
taarifa za juu zinasema :- Habari zilizopatikana jana usiku kutoka ofisi ya Waziri Mkuu zilisema kwamba Rais alichukua hatua hiyo...MWANZO ..Rais Jakaya Kikwete, amemvua madaraka na kumfukuza kazi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC), mkoani Kagera, Albert Mnali, kutokana na kitendo cha kuwacharaza bakora walimu wa shule za msingi wa wilaya hiyo.
Ukisoma hapo na kupaelewa utaona Raisi hahusiki na kumfukuza DC ,lakini vilevile panaonyesha amemfukuza ,tupo ? Inamaana timu nzima ya mkoa wa Kagera haifai ,ndio maana yake ! Haielewi sheria wanaogopana ! Samaki mmoja akioza ndio wameoza wote. CCM ing'olewe kwenye madaraka hakuna njia ya kwenda nao namna hii.
Kuna hawa watu wa TUME ZA HAKI ZA BINADAMU ,wenzetu ulaya wana mpaka za wanyama hawa nawaweka kiporo.
Alisema Ibara ya 13 (6) (e) ya Katiba inatamka kuhusu adhabu kwa kusema: ``Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.`` Tume hii inayosoma Vifungu vya Sheria inaongozwa na Jaji Mstaafu Amiri Manento ambae ni Mwenyekiti ,Makamu Mwenyekiti Mahfoudha Alley Hamid.
Wameendelea kujilabu kwa kusema ``Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa mujibu wa sheria za nchi hususan Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora ambayo Tanzania imeridhia,`` alisema Mahfoudha.
Bibie Mahfoudha aliendelea kurapu DC alivuka mipaka kwa kutoa adhabu ya kutweza au kudhalilisha utu, ikiwamo walimu wa kike kucharazwa bakora,
Alisema kitendo hicho alichokiita cha aina yake na cha aibu nchini, kimeleta athari kubwa kwa walimu, ikiwamo kuwavunjia heshima kwa wanafunzi, familia zao na jamii kwa jumla na pia kimewavunja moyo katika kazi zao za kila siku.
Hawa wote wanajipendekeza tu au wanajivutia tu waonekane wapo mstari wa mbele mbona yale yaliotokea Pemba na Unguja hawajayasemea ? Na ruhusa wamepewa kufanya shughuli zao huko ,mbona matatizo ya vurugu yanayotokea katika Nchi nzima hawayakemei ,chaguzi zote zilizofanywa Tanzania Bara zimefikwa na vurugu watu kupigwa na kuumizwa mbona hawajaikemea serikali na vyombo vyake vya dola au wanaofanyiwa vitendo hivi si binadamu na hawastahiki kupiganiwa haki yao ya msingi. ni mengi ya kuwalaumu watu wa Tume hii ambao wamelivalia njuga suala la DC kuwapiga walimu viboko viwili tu. Tuendako ni mbali ikiwa wanaihusika wanajificha mpaka raisi asikie makelele na kumfukuza mtu wao ndio utawaona mstari wa mbele. Ni aibu.
DC masikini ametolewa kafara la uwajibikaji wa Serikali ,Serikali hii haikuchukua jukumu la kuwasimamisha kazi mafisadi wala kuwafukuza ,mafisadi ambao wameliibia Taifa mabilioni ya shilingi ,wizi huo umesababisha maafa makubwa hapa Tanzania kuliko hizo bakora mbilimbili walizopigwa walimu ,wizi wa mabilioni umedhalilisha wanawake kuliko hao wanawake waliopigwa bakora ,mwanamke anapokwenda kujifungua anatakiwa akatafute vifaa vya kumzalishia uraiani kama si kumdhalilisha ni kitu gani ? Walimu na wanafunzi wao maeneo na vitendea kazi ni duni , nchi haina maji safi ,Nchi haina umeme wa kuaminika ,yote yamechangiwa na wizi wa baadhi ya wachache ambao wameliibia Taifa hili fedha isiyojulika kwa wingi wake tunabaki na mahesabu ya miaka miwili mitatu nyuma. Hawa ambao wengine walikuwa maraisi wengine mawaziri wapo mitaani na kujikumbatisha kwenye Chama Cha CCM na CCM kuwakumbatia wao ,nini Serikali ya CCM mnataka kutuambia kwa kisa hiki cha DC mmoja ?
Tatizo la uwajibikaji wa Serikali na vyombo vyake ndilo lililomfikisha DC hapo alipofikia maana hana pa kwenda mambo yanayoendeshwa na serikali ya CCM ni ya kibinafsi binfsi tu ,hakuna maslahi ya kuiba hakuna atakaekusaidia ,ndipo alipofikishwa DC ,ndipo alipochanganyikiwa na akili hajui afanye nini na akili ndio imemtuma labda akifanya hivyo mambo yatakuwa mazuri ,kwa wengine ni bora angeyawacha kama yalivyo ,lakini DC ni mtu masikini anaogopa nae kuja siku akafukuzwa kwa kuwa wanafunzi wa eneo lake hawafaulu vizuri walimu wanachelewa,nini afanye DC ? Katika Nchi hii iliyojaa urasimu na itifaki ,kila anachojaribu hakiwi hakiendi mbele ,serikali haina msaada isipokuwa maneno matupu ,serikali haiwalipi walimu kwa muda muawafaka kinacholipwa hakiumalizi mwezi,walimu wamekuwa wanafanya wanavyotaka ,hawamsikilizi mkubwa wala mdogo ,masikini DC ameona labda akifanya hivi wananchi wa eneo lake wataamka na kuwanza nguvu kazi lakini wapi ,wabaya wake wote wamemsakama na kumgeukia kwa kumtumbukiza kwenye shimo na serikali imeona haina njia isipokuwa kumfukuza bila ya kuchunguza matatizo yaliyomfanya DC kufikia hatua hiyo yana ukweli kwa kina, imemfukuza na kumuua palepale ,ndio maana yake.