DC aliyewacharaza viboko walimu afukuzwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC aliyewacharaza viboko walimu afukuzwa kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mapinduzi, Feb 14, 2009.

 1. M

  Mwana Mapinduzi Member

  #1
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waandishi Wetu

  RAIS Jakaya Kikwete amemvua madaraka na kumwachisha kazi rasmi kuanzia jana, mkuu wa wilaya ya Bukoba, Albert Mnali aliyeamuru polisi mmoja kuwachapa viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizoko wilayani kwake kutokana na kushika mkia katika matokeo ya darasa la saba.

  Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu jana ilieleza kuwa, Rais Kikwete amechukua hatua hiyo ili iwe fundisho kwa kuwa kitendo alichokifanya mkuu huyo wa wilaya hakikubaliki, kimedhalilisha, cha kuvunja moyo walimu na kinavunja maadili ya kibinadamu.

  Katika uamuzi huo, Rais Kikwete alisema mkuu huyo wa wilaya amedhalilisha wadhifa wa ukuu wa wilaya kwa kuwa alikosea kuchukua hatua hiyo kwa kuwa mwenye mamlaka ya kuwawajibisha walimu ni kamati za nidhamu za mikoa na wilaya na wala si mtu mmoja kama alivyofanya mkuu huyo.

  Alisema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kufuatilia maelezo ya pande zote zinazohusika na kuwa serikali imeridhia kiongozi huyo avuliwe wadhifa.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,438
  Trophy Points: 280
  Angekuwa na speed kama hii ya kuwafukuza kazi mafisadi ndani ya chama na serikali basi Watanzania tungekuwa na furaha kubwa. Pamoja na kuunga mkono kufukuzwa kwa huyu Mkuu wa Wilaya bado nashangaa kuona wabunge chungu nzima wa CCM waliogubikwa na tuhuma nziti za ufisadi dhidi ya nchi yetu akiwemo Lowassa, Msabaha, Karamagi, Rostam Azizi, Chenge na wengineo kibao bado amewakumbatia ndani ya chama bila kutia neno lolote.

  Pamoja na mapendekezo ya tume ya Mwakyembe kwa Kikwete kwamba Mkku wa TAKUKURU na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waondolewe madarakani kwa manufaa ya umma kwa kuandika ripoti ya uongo kuhusiana na ufisadi wa Richmond, lakini hadi hii leo bado amewakumbatia. Je, kulikoni?

  Mh Kikwete wakati sasa umefika wa kutumia rungu lako bila upendeleo wowote ule na kuwafukuza kazi wale wote wasiostahili kuajiriwa na serikali na wale waliomo ndani ya chama ambao wamegubikwa na thuma nzito za ufisadi waliofanya dhidi ya Watanzania bila wiga wowote.
   
 3. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huyu bwana wanatakiwa wangemchapa kwanza viboko kumi na viwili.....aone chungu yake.Sio kumwacha aende tu...

  Haya mambo atakuwa aliyaanzisha kwenye familia yake...nafikiri.Ni udhalilishaji wa hali ya juu sana...huwezi kuchapa watu wazima na familia zao mbele ya watoto...
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Raisi asiishie kumfuta kazi tu, huyu jamaa apelekwe mahakamani kwa kuvunja katiba ya URT!
   
 5. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Utashangaa kwamba huyu jamaa anaweza kwenda mahakamani na kushinda kesi yake ya kufukuzwa kazi bila taratibu zilizopo kufuatwa. Na hivi hapa ina maana akishafukuzwa kazi ndio hili suala limefikia kikomo? Hivi hawezi kushtakiwa kwa ABH? Victims wa hili suala wana nafasi nzuri ya ku claim fidia kwa walichotendewa, wasiogope kwenda mahakamani.
   
 6. M

  Mwana Mapinduzi Member

  #6
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuchapwa mbele ya wanafaunzi...
  aliwafungia ndani, sasa sijui ni darasani au la...
  ila sio mbele ya wanafunzi...
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135


  Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi leo, kwamba hawa victims walilipoti kny vituo vya polisi, na kwenda hospitali kuchekiwa afya zao, na kwamba CWT mkoa wa mara wanaanda taratibu za kumfungulia mashtaka DC (wa zamani) huyo kwa niaba ya Victims wote! Sijasikia kina Mkoba wanasemaji katika ngazi ya Taifa.....lazima wadai fidia kwa udhalilishwaji waliofanyiwa na huyu mkware!
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Feb 14, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Aisee mimi ningekula naye sahani moja mpaka kieleweke. Huwezi kumcharaza mboko mtu mzima aisee. That's a no no. Na kama siku mtoto wangu anarudi nyumbani na kuniambia kachapwa na mwalimu.....it's on. Lazima nimtoe meno huyo mwalimu. I swear....hommie don't play that
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  hawezi kushinda popote pale, kazi ya Ukuu wa Wilaya au ukuu wa Mkoa ni kuteuliwa tu na Rais tena kwa upendeleo fulani. Hakuna taaluma wala nini, tena hakuna mkataba wa muda wa kufanya kazi. Hivyo hakuna appeal atakayoweza kufanya.
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nani huyo aliemfukuza kazi DC ? Najua mtasema ni Mheshimiwa Kikwete au sio ?
  Kwa nini amemfukuza kazi ? Kwa sababu Dc ametoa amri ya kuwachapa viboko watu wazima walimu waume kwa wake hadharani.

  Ila ijulikane tu aliewachapa viboko ni askari polisi(Sijui ni polisi wangapi walishirikishwa katika zoezi hilo ,panahitajika uhalisia wa polisi walioshiriki) ,hapo hakuna ubishi.

  Je amri aliyotoa DC inamtazamo kisheria katika taratibu za kipolisi ? Ndio ni amri.

  Je polisi anayohaki ya kukataa kama ataona alichoamrishwa si haki na ni kuvunja sheria kwa mujibu wa kazi zao ? Polisi anayo haki ya kukataa.

  Je kumuadhibu polisi huyu inafaa au haifai ikiwa itaonekana amevunja taratibu za kipolisi ?

  Naomba majibu ya masuala hapo juu japo ,pataonekana pana majibu mimi nimeyaweka kama majibu hewa.

  Sasa nikigeukia taarifa za Ikulu au za Wakubwa.

  Mmoja alitoa jibu la papokwa papo ,DC akapimwe akili. kidogo linaelekea ,kwa nini hakuamrisha polisi wamkamate au wampeleke hospitali kama ni hatua ya kwanza ? Inawezekana kabisa historia ya DC huyo kuwa aliwahi kuugua ugonjwa wa akili pengine Maleria na Tz ipo maleria na huwajia watu juu ikawa ni patashika.
  Ikiwa atapimwa na kuonekana Mheshimiwa Dc ana/alikuwa na matatizo ya akili basi ni wazi kabisa kitendo cha kumfukuza kazi kitakuwa ni kumdhulumu na Raisi wetu alichokosea ni huko kuamua moja kwa moja kuwa amemfukuza kazi au sijui kumsimamisha.Natumai kuna haja ya kufikiria kwani kitendo cha DC na Raisi vitakuwa havipishani,natumai nitaeleweka hapo ,ni dhahiri kabisa yule aliesema akapimwe akili atakuwa yupo kwenye mstari mzuri tu wa uongozi ,au sivyo wandugu wa JF ? Na wale wote waliosema achukuliwe hatua watakuwa hawana tofauti na DC ,wote zimewashoti.

  Nakubaliana kuwa Raisi anapower zinazomruhusu kutoa maamuzi. Sawa na iwe hivyo ,ila nakumbuka aliwahi kumfukuza mtu mmoja kazi nafikiri alimtaka ajiuzulu au alimfukuza direct sina hakika ya hapo ,na baadae Rais huyu huyu akafikia kujutia kile kitendo. Ndio hapo ,amemfukuza DC ,DC ametenda kosa ambalo linaonyesha kuna matatizo ya akili.

  Msemaji kutoka ofisi ya waziri Mkuu Bwire amenukuliwa :- Rais alisema kulingana na taratibu, kamati za nidhamu za wilaya na mikoa ndizo zenye majukumu ya kutoa adhabu kwa wafanyakazi wa umma kama ikionekana inafaa na kwamba kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya kimekiuka kanuni hiyo.
  ``Amevunja kanuni na ameidhalilisha ofisi na mamlaka ya ukuu wa wilaya,`` sehemu ya taarifa hiyo ilisema kama ilivyosomwa na Bwire

  Hapa katika maelezo ya Ikulu kuna utata ndani yake inataka usome kwa makini na uelewe alichokisema Raisi.

  taarifa za juu zinasema :- Habari zilizopatikana jana usiku kutoka ofisi ya Waziri Mkuu zilisema kwamba Rais alichukua hatua hiyo...MWANZO ..Rais Jakaya Kikwete, amemvua madaraka na kumfukuza kazi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC), mkoani Kagera, Albert Mnali, kutokana na kitendo cha kuwacharaza bakora walimu wa shule za msingi wa wilaya hiyo.

  Ukisoma hapo na kupaelewa utaona Raisi hahusiki na kumfukuza DC ,lakini vilevile panaonyesha amemfukuza ,tupo ? Inamaana timu nzima ya mkoa wa Kagera haifai ,ndio maana yake ! Haielewi sheria wanaogopana ! Samaki mmoja akioza ndio wameoza wote. CCM ing'olewe kwenye madaraka hakuna njia ya kwenda nao namna hii.

  Kuna hawa watu wa TUME ZA HAKI ZA BINADAMU ,wenzetu ulaya wana mpaka za wanyama hawa nawaweka kiporo.

  Alisema Ibara ya 13 (6) (e) ya Katiba inatamka kuhusu adhabu kwa kusema: ``Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.`` Tume hii inayosoma Vifungu vya Sheria inaongozwa na Jaji Mstaafu Amiri Manento ambae ni Mwenyekiti ,Makamu Mwenyekiti Mahfoudha Alley Hamid.

  Wameendelea kujilabu kwa kusema ``Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa mujibu wa sheria za nchi hususan Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora ambayo Tanzania imeridhia,`` alisema Mahfoudha.

  Bibie Mahfoudha aliendelea kurapu DC alivuka mipaka kwa kutoa adhabu ya kutweza au kudhalilisha utu, ikiwamo walimu wa kike kucharazwa bakora,
  Alisema kitendo hicho alichokiita cha aina yake na cha aibu nchini, kimeleta athari kubwa kwa walimu, ikiwamo kuwavunjia heshima kwa wanafunzi, familia zao na jamii kwa jumla na pia kimewavunja moyo katika kazi zao za kila siku.

  Hawa wote wanajipendekeza tu au wanajivutia tu waonekane wapo mstari wa mbele mbona yale yaliotokea Pemba na Unguja hawajayasemea ? Na ruhusa wamepewa kufanya shughuli zao huko ,mbona matatizo ya vurugu yanayotokea katika Nchi nzima hawayakemei ,chaguzi zote zilizofanywa Tanzania Bara zimefikwa na vurugu watu kupigwa na kuumizwa mbona hawajaikemea serikali na vyombo vyake vya dola au wanaofanyiwa vitendo hivi si binadamu na hawastahiki kupiganiwa haki yao ya msingi. ni mengi ya kuwalaumu watu wa Tume hii ambao wamelivalia njuga suala la DC kuwapiga walimu viboko viwili tu. Tuendako ni mbali ikiwa wanaihusika wanajificha mpaka raisi asikie makelele na kumfukuza mtu wao ndio utawaona mstari wa mbele. Ni aibu.

  DC masikini ametolewa kafara la uwajibikaji wa Serikali ,Serikali hii haikuchukua jukumu la kuwasimamisha kazi mafisadi wala kuwafukuza ,mafisadi ambao wameliibia Taifa mabilioni ya shilingi ,wizi huo umesababisha maafa makubwa hapa Tanzania kuliko hizo bakora mbilimbili walizopigwa walimu ,wizi wa mabilioni umedhalilisha wanawake kuliko hao wanawake waliopigwa bakora ,mwanamke anapokwenda kujifungua anatakiwa akatafute vifaa vya kumzalishia uraiani kama si kumdhalilisha ni kitu gani ? Walimu na wanafunzi wao maeneo na vitendea kazi ni duni , nchi haina maji safi ,Nchi haina umeme wa kuaminika ,yote yamechangiwa na wizi wa baadhi ya wachache ambao wameliibia Taifa hili fedha isiyojulika kwa wingi wake tunabaki na mahesabu ya miaka miwili mitatu nyuma. Hawa ambao wengine walikuwa maraisi wengine mawaziri wapo mitaani na kujikumbatisha kwenye Chama Cha CCM na CCM kuwakumbatia wao ,nini Serikali ya CCM mnataka kutuambia kwa kisa hiki cha DC mmoja ?

  Tatizo la uwajibikaji wa Serikali na vyombo vyake ndilo lililomfikisha DC hapo alipofikia maana hana pa kwenda mambo yanayoendeshwa na serikali ya CCM ni ya kibinafsi binfsi tu ,hakuna maslahi ya kuiba hakuna atakaekusaidia ,ndipo alipofikishwa DC ,ndipo alipochanganyikiwa na akili hajui afanye nini na akili ndio imemtuma labda akifanya hivyo mambo yatakuwa mazuri ,kwa wengine ni bora angeyawacha kama yalivyo ,lakini DC ni mtu masikini anaogopa nae kuja siku akafukuzwa kwa kuwa wanafunzi wa eneo lake hawafaulu vizuri walimu wanachelewa,nini afanye DC ? Katika Nchi hii iliyojaa urasimu na itifaki ,kila anachojaribu hakiwi hakiendi mbele ,serikali haina msaada isipokuwa maneno matupu ,serikali haiwalipi walimu kwa muda muawafaka kinacholipwa hakiumalizi mwezi,walimu wamekuwa wanafanya wanavyotaka ,hawamsikilizi mkubwa wala mdogo ,masikini DC ameona labda akifanya hivi wananchi wa eneo lake wataamka na kuwanza nguvu kazi lakini wapi ,wabaya wake wote wamemsakama na kumgeukia kwa kumtumbukiza kwenye shimo na serikali imeona haina njia isipokuwa kumfukuza bila ya kuchunguza matatizo yaliyomfanya DC kufikia hatua hiyo yana ukweli kwa kina, imemfukuza na kumuua palepale ,ndio maana yake.
   
  Last edited: Feb 14, 2009
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Taib.

  Cheo cha ukuu wa Wilaya ni cha KISIASA.. Huko kipindi cha awali iliwahi kushauriwa ktk kubana matumizi ya serikali, pamoja kupunguza baraza la mawaziri, ilishauriwa cheo cha mkuu wa wilaya na vyeo vingine vya ajabuajabu vifutwe, lakini naona ndio hivyo kimya na siku zinazidi kusonga.

  Hivi vyeo vya kupeana kama pipi ndo matatizo yake, mtu hajui awajibike vipi na yepi ni majukumu yake anaishia kuwachapa walimu bakora. Lakini kwa system ya Tz, sitashangaa siku chache zijazo ukamsikia ameteuliwa kwenye bodi ya shirika fulani ktk kuliendeleza libeneke...
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Feb 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wadanganyika bwana,
  Sikubaliani na yaliyotokea huko Bukoba lakini kuna kila haja ya kutazama utawala mzima wa CCM pamoja na sheria zenyewe..
  Wananchi wanapofanya maandamano kupinga serikali hupigwa virungu na sijasikia DC akifukuzwa kazi..Hata mihadhara ya vyama pinzani tu tumeshuhudia wananchi watu wazima wakicharazwa bakora na virungu. Ni kifungu gani cha sheria kinachotumika!

  Amri kama hizi za utumiaji nguvu ya dola ni Udikteta mtupu sasa isiwe mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu..
  Kikwete ameweza kuliona hili nitapenda sana kuona sheria hii inatumika kila sehemu ikiwa kweli tunaitafuta haki..Kikubwa nini hasa hapa? kuchapwa bakora mtu mzima, sheria mkononi au sii haki kumchapa mtu hata kama mtu amekosea!...
  On the other hand sidhani kama ile sheria ya kuchapwa bakora wakosefu toka mahakama zetu imekwisha futwa!..
   
 13. e

  eddy JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,406
  Likes Received: 3,783
  Trophy Points: 280
  Jamani mbona tuna dable standard? hawa walimu walimlamba ngwara rais wao tena mbele ya kamera itv na tbc! hakuna aliyefutwa kazi, sasa waliwa mboko twamfuta kazi DC! anyway hawa waalimu wamesaidia kupunguza wanafunzi wa vasity, wakifaulu wote UDSM patukuwa hapatoshi.
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  dear contributors, i beg to differ with more than 95% of the opinion!
  mr. DC was right!!!!
  1. ni professional soldier!
  2. aliyetekeleza amri ni junior kwake (kanali vs koplo)
  3. uamuzi wa haraka na sahihi
  4. ili iwe fundisho (as a warning) kwa watendaji wengine wazembe
  5. bado uamuzi wake wa kuwaadhibu watendaji wabovu kwa kosa la kufelisha kizazi kijacho ni VALID na ufanyiwe kazi
  6. THE STRONGEST MAN IN THE WORLD IS WHO STANDS ALONE!!!!!
  TO YOU MR DC!!!!!!!
  hii ndiyo TZ ndugu yangu , na hawa ndiyo WA-TZ wenyewe.....! mara nyingi mtu anapochukua maamuzi magumu kwa wakati ule huonekana kama mwehu, insane, sinner, na majina mengine mengi.
  chukua mfano wa OKONKWO ambaye alichukua uamuzi wa kumuua kibaraka na mtumwa wa wazungu....! akidhani jamii itakuwa on his side ! jamii ikawa kinyume chake! HADITHI IKAENDELEA!
  NAKUTIA MOYO WA KUENDELEA KUPAMBANA KWA MOYO WA KIZALENDO, JAPOKUWA HUENDA TUMEBAKI WAPIGANAJI WACHACHE!!!!!
  KIKOSI CHETU KIPO HIVI
  KANALI
  KOPLO
  MAHESABU
  ???????
  ???????
  ??????/
   
 15. M

  Mwana Mapinduzi Member

  #15
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu mahesabu nakuunga mko no mia kwa mia...
  me naona DC alikua right.. watanzania hatuendi bila bakora...
  nimemshangaa sana kunamtu alicomment eti akisikia mtoto wake amechapwa na mwalimu atakula nae sahani moja... sidhani kama huyu mtu ni mzima,
  kama umefatilia miaka yahivi karibuni tangu hivi visheria vimeingia vya watoto kutochapwa ,performance ya wanafunzi imepungua sana....
  mimi binafsi bila bakora nsingekua hapa nilipo...
  watu wengi mnakumbuka walimu kama mzee ndosi wa muhimbili primary... tulikua tunashika adabu...
  watoto wa kizazi cha sahivi wamekua wajinga sana....

  nashaangaa Rais kikwete kureact fasta katika ishu hii...
  kunamambo mengi sana alitakiwa awe anatoa maamuzi ya haraka kama haya ila ameishia kukaa kimya.... sasa nashindwa kumwelewa kabisa....
  watanzania kuanzia Rais wetu mpaka wananchi tuna shangaza mno...
   
 16. M

  Mwana Mapinduzi Member

  #16
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanyongeza.. DC yuko right na nimzalendo anauchungu na nchi yake...
  me namuunga mkono... tunahitaji viongozi wenye moyo kama huu....
   
 17. C

  Chokona Member

  #17
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nafikiri na mfumo wetu wa elimu ni duni sana kwani walimu walitakiwa wakatae maana wanajua kuwa mwajili wao si mkuu wa Wilaya na hivyo they are not responsible kwake kukubali kuchapwa ilikuwa ni kujidhalilsha kwa hali ya juu unless kama wamekubali at gun point!! Pia na hao askari waliohusika nao inabidi wachukuliwe hatua maana askari polisi wajibu wake ni kulinda usalama wa raia na mali zao nasiyo kuwaadhibu watumishi wenzao kama wangegoma huyu mwendawazimu asingefanya uhuu wendawazimu
  Mwisho ni hayo matatizo ya kupeana vyeo bila kufuata taratibu, I would not be suprised nikiambiwa kuwa huyu jamaa ni mwanamtandao au alikuwa karibu na wanamtandao nafikiri rais wakati anteuwa maDC first qualification was mwanamtandao na hivi unalipwa fadhila.
   
 18. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  " VIBOKO KUMI NA MBILI SIKU YA KUINGIA,KUMI NA MBILI SIKU YA KUTOKA UKAMWONESHE MKEO"-mwalimu legacy KWA waalimu.
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sitashangaa kuona maandamano nchi nzima yakiongozwa na walimu kumpongeza kwa hatua aliyoichukua!
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kitendo cha kumfukuza kazi mkuu huyu wa wilaya ni kitendo cha uonevu. Mkuu huyu aliamua kuwatandika viboko kwa nia njema kabisa ya kuwatisha walimu ili wasirudie tena tabia ya kuchelewa na kutowapa huduma muhimu sana ya elimu bora watoto ambao wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu kutokana na tabia hii mbaya ya walimu.

  Ni uonevu kwa kuwa yeye alifikia hatua hiyo akiwa na nia thabiti kabisa moyoni mwake ya watoto wa Bukoba kupata Elimu bora kwa manufaa ya Taifa katika siku zijazo. Huenda kama angepewa muda wa kujitetea basi tungeingiwa na huruma jinsi ambavyo angejitetea na hata chozi kumtiririka kwa uchungu aliyo nao juu ya watoto kutofundishwa na walimu hawa watoro na wazembe, tena usijekuta wengine wamesha sahau hata kusoma kwa uzembe wao. Hapa Rais hajatenda haki kwa mtazamo wangu, kwani hakufanya kwa kujifurahisha bali kwa manufaa ya Watoto - Rejea ya Pinda na wauaji wa Albino ndiyo utakubaliana na mimi kuwa huyu kaonewa
   
Loading...