DC aliyewacharaza viboko walimu afukuzwa kazi

Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

JANA katika vyombo mbalimbali vya habari kulikuwa na taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya Bukoba, Albert Mnali, ameamuru polisi kuwachapa viboko walimu wa wilaya hiyo kwa kosa la uzembe kazini.

Kwa mujibu wa taarifa hizo uzembe anaousema DC huyo ni kuchelewa kufika kazini, kutofundisha kwa kiwango kinachotakiwa, jambo lililofanya wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika mtihani wa darasa la saba. Walimu hao wapatao 32 kila mmoja alichapwa viboko viwili.

Kwa mtazamo wangu huu ni udhalilishaji na uoneve ni lazima DC aliyehusika awajibishwe kwa kufanya kituko hicho. Ni ajabu kwa kiongozi mwenye dhamana kubwa kufikiria zaidi kuwa matokeo mabaya ya wanafunzi wa darasa la saba, husababishwa na uchelewaji wa walimu shuleni au kutofundisha vizuri.

Walimu hivi sasa wanaishi katika mazingira magumu, hawana mishahara ya kutosha, nyumba, miundombinu mibovu na matatizo mengine ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na serikali ndiyo maana hata ufundishaji wao hauridhishi.

Ni ukweli usiopingika kuwa walimu wa shule binafsi wamekuwa wakifanya vizuri zaidi kwa sababu ya mishahara mizuri, nyumba, usafiri na mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Kama kweli kuwachapa viboko walimu hao ndiyo njia nzuri ya kutaka wafanikiwe, basi ni vema na utaratibu huo sasa uukageukia kwa wanasiasa ambao wamekuwa wakilipwa posho nono zaidi lakini wameshindwa kutimiza ahadi walizozitoa!

Hii leo tuanzie viongozi wa juu wa serikali kuanzia kwa Rais, Mawaziri, Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya ambao wameshindwa kuleta maisha bora waliyoyaahidi kwa kila Mtanzania - barabara, hospitali shule na huduma nyingine ni mbovu kupita kiasi lakini kila kukicha viongozi wetu wamekuwa wakitumia mamilioni ya fedha katika mambo yasiyo na manufaa kwa taifa lakini bado hatujawachapa viboko hadi sasa.

Kwa nini tusiwachape viboko wabunge wetu ambao kila kukicha wamekuwa wakipigania kuongezwa kwa maslahi yao bila kujali fedha hizo ndizo zinazotolewa na wananchi wenye vipato duni vinavyotokana na kuuza mifugo au mazao yao?

Kama kweli tuna nia ya dhati ya kuboresha elimu kwa nini tusimchape viboko Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ambaye kwa miaka miwili sasa viwango vya kufaulu kwa wanafunzi vinashuka pamoja na shule za sekondori za serikali zimekuwa zikipata matokeo mabaya kulinganisha na za binafsi.


Kwa nini tusimchape viboko Mkuu wa Baraza la mitihani la Taifa kwa mitihani kuvuja kabla ya kufanywa, lakini pia tusiache kuwachapa viboko na watendaji wa baraza hilo kwa kutengeneza vyeti bandia na kuziuza kwa gharama ndogo? Hawa si ndiyo wanoshusha kiwango cha elimu? Kwa nini tusiwachape watendaji wa wizara ya elimu kwa kuanzisha mafunzo ya muda mfupi kwa walimu ‘Voda Vasta’ ambao tuna uhakika hata ufundishaji wao si bora.

Binafsi nafurahia mfumo wa kuanza kuchapana viboko lakini ni vema ukaanzia katika ngazi za juu ambako ndiko kwenye maafa zaidi kuliko ngazi za chini ambazo kwa kiasi kikubwa huathiriwa na mfumo mbaya wa uongozi wa juu.

Tungeweza kuwachapa viboko kina Lowassa, Hosea, Karamagi na Msabaha kwa kuiingiza nchi katika mkataba wa Richmond ambao ulilifanya taifa kulipa sh milioni 152 kwa siku hapo ningefurahi, tungeweza kumchapa Mramba kwa kununua ndege ya rais yenye thamani ya bil 40 huku wananchi wakifa na njaa tena kwa kuwalazimisha wale majani hapo ningeunga mkono uchapaji viboko.

Nani atayeweza kufanya kazi kama hajui atakaa wapi, familia yake itakula nini, ataishi vipi na huduma nyinginezo za muhimu? Viongozi wana uhakika na maisha yao, kwani wanakaa kwenye nyumba nzuri, marupurupu mazuri, wanasomesha watoto zao shule za kimataifa na wengine wanawapeleka nje ya nchi, wanatibiwa nje ya nchi sasa kwa nini washindwe kufanya kazi vizuri hasa kwa kutimiza ahadi walizozitoa? Nani asiyejua hivi sasa uongozi ni biashara?

Mbunge anayekaa madarakani kwa muda wa miaka mitano hupata sh milioni 30, gari na posho nono za kila kikao anashindwaje kuisimamia serikali kuwapelekea wananchi maendeleo?

Hawa ndiyo wa kuchapwa viboko kwani wana ‘maisha bora’, lakini hawana moyo wa kufanya kazi, walimu wana moyo wa kufanya kazi lakini hawana maisha bora watawezaje kutekeleza wajibu wao kwa taifa?

Tatizo la nchi hii ni viongozi kutokuwa makini na kusimamia wajibu wao, inawezekanje sekta ya elimu isipewe kipaumbele kinachotakiwa na badala yake fedha nyingi zinaishia kwa wajanja wachache kwa kununua magari ya kifahari pamoja na kuandaa warsha za ujanjauujanja?

Kama tusipokuwa makini ipo siku tutaanza kupigana risasi hadharani kwa kushindwa kutimiza wajibu, kwani itafika wakati tutaona viboko havifai.
 
tena walimu wameandaa maandamano yakumpongeza kikwete kwakumfukuza DC..
ha ha ha..... nahisi hao walimu ndio wa kupimwa akili na sio DC....
 
tena walimu wameandaa maandamano yakumpongeza kikwete kwakumfukuza DC..
ha ha ha..... nahisi hao walimu ndio wa kupimwa akili na sio DC....
 
tena walimu wameandaa maandamano yakumpongeza kikwete kwakumfukuza DC..
ha ha ha..... nahisi hao walimu ndio wa kupimwa akili na sio DC....
 
Hawa waalimu ni waajabu sana, nadhani walistahili kupata bakora, sasa wanaandamana kwa lipi? Ujinga huuu


tena walimu wameandaa maandamano yakumpongeza kikwete kwakumfukuza DC..
ha ha ha..... nahisi hao walimu ndio wa kupimwa akili na sio DC....

Walimu waandaa maandamano kumpongeza JK kumtimua DC
Na Christopher Maregesi, Bunda

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), wilayani Bunda, Mkoa wa Mara kimeandaa maandamano ya amani kwa ajili ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumfukuza kazi MKuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali kwa kuwadhalilisha walimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho wilayani hapa, Fransis Ruhumbika alisema maandamano hayo yatakayowashirikisha walimu wote wa shule za msingi, sekondari na vyuo waliomo ndani ya wilaya hiyo yamepangwa kufanyika Jumanne ijayo.

Kwa mujibu wa Ruhumbika, maandamano hayo yataanzia katika viwanja vya shule ya msingi ya Balili ya mjini hapa saa 2.30 asubuhi na hadi makao makuu ya wilaya hiyo yaliyoko umbali wa kilomita nne kutoka katika eneo hilo ambako yatapokelewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya mkoa na taifa.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi wilayani hapa zinasema limeshapokea barua ya chama hicho kuomba kibali cha kuaandamana lakini bado halijajibu.

Pamoja na kumpongeza pais kwa maamuzi yake hayo ya kumfukuza kazi mkuu huyo wa wilaya,maandamano hayo pia yanalenga kuwalaani maofisa wa serikali wa kada mbalimbali wenye tabia kama za Mnali, ingawa uovu wanaowafanyia walimu haujafunuliwa.

Jana rais Kikwete alimfukuza kazi Mnali baada ya kuwachapa viboko walimu wa shule tatu za msingi wilayani humo zinazosadikika kufanya vibaya katika mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka jana.
 
Hawa waalimu ni waajabu sana, nadhani walistahili kupata bakora, sasa wanaandamana kwa lipi? Ujinga huuu




Walimu waandaa maandamano kumpongeza JK kumtimua DC
Na Christopher Maregesi, Bunda

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), wilayani Bunda, Mkoa wa Mara kimeandaa maandamano ya amani kwa ajili ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumfukuza kazi MKuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali kwa kuwadhalilisha walimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho wilayani hapa, Fransis Ruhumbika alisema maandamano hayo yatakayowashirikisha walimu wote wa shule za msingi, sekondari na vyuo waliomo ndani ya wilaya hiyo yamepangwa kufanyika Jumanne ijayo.

Kwa mujibu wa Ruhumbika, maandamano hayo yataanzia katika viwanja vya shule ya msingi ya Balili ya mjini hapa saa 2.30 asubuhi na hadi makao makuu ya wilaya hiyo yaliyoko umbali wa kilomita nne kutoka katika eneo hilo ambako yatapokelewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya mkoa na taifa.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi wilayani hapa zinasema limeshapokea barua ya chama hicho kuomba kibali cha kuaandamana lakini bado halijajibu.

Pamoja na kumpongeza pais kwa maamuzi yake hayo ya kumfukuza kazi mkuu huyo wa wilaya,maandamano hayo pia yanalenga kuwalaani maofisa wa serikali wa kada mbalimbali wenye tabia kama za Mnali, ingawa uovu wanaowafanyia walimu haujafunuliwa.

Jana rais Kikwete alimfukuza kazi Mnali baada ya kuwachapa viboko walimu wa shule tatu za msingi wilayani humo zinazosadikika kufanya vibaya katika mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka jana.

No disresepct to teachers... lakini kama msimamo wao ni wa kuandamana na polisi wakawaruhusu, basi wanahitaji kupimwa zaidi

maana hawajaandama kushukuru kulipwa malimbikizo, hawajaandamana kulaani wilaya zilizofanya vibaya na hawajaandamana kulaani mengi ikiwa ni pamoja na maisha magumu wanayoishi

Mara nyingine dharau tunazitafuta wenyewe
 
I will not necessarily say that the DC was either completely right or wrong,but one thing is for sure the teachers needed some kind of reminder.Stroking a teacher was the best thing to do,what do you think the children will think of the teacher when they want to give them some kind of punishment?The DC could probably suspend them or anything,but stroking was extreme.And to teachers,it is your responsibility to be in the work place at the right time.Probably you have learn a lesson.
 
Kwanyongeza.. DC yuko right na nimzalendo anauchungu na nchi yake...
me namuunga mkono... tunahitaji viongozi wenye moyo kama huu....


Hatukatai kuwa ana uchungu na nchi yake, na hatujui hata kama waalimu walikuwa na hatia au la. Tunachoshangaa ni kuwa katika karne hii kuna watu ambao wanadhani kupiga wenzao viboko ni adhabu inayofaa. Siku hizi hata wafungwa wenye makosa ya jinai hawapigwi fimbo. Kuchapana viboko kumepitwa na wakati, tufikirie kutafuta njia nyingine za kutatua matatizo. Halafu suala la elimu, au kuelimisha linahusu watu wengi sio waalimu peke yao, wazazi na jamii inahusika sana. Tujiulize wazai wamechangiaje kuzorota kielimu kwa watoto wao? Ukiongea na watu wengi waliofanikiwa kielimu utasikia kuwa wazai walikuwa na mchango mkubwa sana kufuatilia matokeo na kukuuliza kijana mbona temu iliyopita ulipata maksi 80 mbona temu hii una 65 etc.
 
Last edited:
Kuchapa Watanzania bakora katika nafasi zote za utumishi ni muhimu na ni jambo ambalo limechelewa sana kuchukuliwa hadi shujaa Malegeresi (DC)alipochukuwa hatua hiyo. NAMPONGEZA SANA. Hakuna huduma yoyote sasa hivi unayoweza kuipata nchini bila ya kusukumana na ahadi za njoo kesho. Watu hawafanyi kazi ni porojo za michezo siku nzima. Kwa msisitizo naomba Waheshimiwa wabunge wapeleke mswada bungeni kuhusu hii adhabu ya bakora ili iweze kutumika bila ya kuingiliwa na nguvu za watawala. Angalia Wachina wanavyotikisa dunia kwa maendeleo baada ya bakora nyingi kutoka kwa watawala wao, wanaelewa maana ya kufanya kazi katika kila eneo. Hakuna mabadiliko bila kusukumana kwa bakora na mijeledi. Asante Malegeresi tunakusubiri MTWARA.
 
DC aliyewacharaza viboko walimu afukuzwa kazi: Nakubaliana na wana-JF walio-comment kwamba huyu DC alistahili kufukuzwa kazi, na labda hata ingefaa apelekwe kortini kwa tuhuma za kudhalilisha walimu.

Lakini DC huyu ameonyesha jinsi wazazi na Watanzania wengi wanaojali, wanavyokerwa na jinsi elimu inavyoendeshwa bila tija Tz kwa jumla. Mimi nampongeza huyu DC kwa matamshi aliyotoa gazetini, kwamba licha ya kufukuzwa kazi "lakini ujumbe wake umefika".

Kwa shule tatu katika Wilaya ya Bukoba kutofaulisha hata mtoto mmoja katika mtihani wa darasa la saba, ni tatizo linalostahili kuchambuliwa kwa makini na kutafutiwa jawabu. Siyo tu kwamba walimu wapewe mafunzo stahili na vivutio wafanye kazi kwa juhudi zaidi, bali pia hata shule zenyewe ziwe na vifaa na mazingira yanayoleta tija na sio mateso kwa wanafunzi.

Naona hiyo ndiyo changamoto kwa Rais Kikwete na Serikali yake. Shule nyingi kushindwa kufaulisha vijana wa kutosha kwenda sekondari ni tatizo la kitaifa, na nahisi hawa vijana watafedheheshwa na kudhalilika katika maisha yao ya baadaye kwa kukosa elimu ya sekondari.

Kilasara (JF Member)
 
Angekuwa na speed kama hii ya kuwafukuza kazi mafisadi ndani ya chama na serikali basi Watanzania tungekuwa na furaha kubwa. Pamoja na kuunga mkono kufukuzwa kwa huyu Mkuu wa Wilaya bado nashangaa kuona wabunge chungu nzima wa CCM waliogubikwa na tuhuma nziti za ufisadi dhidi ya nchi yetu akiwemo Lowassa, Msabaha, Karamagi, Rostam Azizi, Chenge na wengineo kibao bado amewakumbatia ndani ya chama bila kutia neno lolote.

Pamoja na mapendekezo ya tume ya Mwakyembe kwa Kikwete kwamba Mkku wa TAKUKURU na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waondolewe madarakani kwa manufaa ya umma kwa kuandika ripoti ya uongo kuhusiana na ufisadi wa Richmond, lakini hadi hii leo bado amewakumbatia. Je, kulikoni?

Mh Kikwete wakati sasa umefika wa kutumia rungu lako bila upendeleo wowote ule na kuwafukuza kazi wale wote wasiostahili kuajiriwa na serikali na wale waliomo ndani ya chama ambao wamegubikwa na thuma nzito za ufisadi waliofanya dhidi ya Watanzania bila wiga wowote.

Bubu nashukuru kwa mchango wako juu ya hoja hii. Kimsingi umenitangulia maana nilikuwa nilikuwa na hoja kama yako tatizo naona mafisadi bado wanashambulia mtandao wetu JF sikuweza kupost chochote bali kusoma tu tena kwa shida.

Pamoja na kumpongeza JK, anapaswa kutambua sisi sio watoto. Imekuwa ni kawaida kesi ndogo zinashughurikiwa kwa kasi kubwa kuliko maelezo lakini zile zenye ''Macro economic impact'' kwa nchi kama za radar, richmonduli, EPA, etc anakuwa na kigugumizi kuamua. Inafurahisha hapa anasema nimesikiliza pande zote mbili nimeamua kufuta kazi. Hili limefanyika ndani ya siku 2. Hivi hawa mafisadi inakuwaje mwaka sasa umepita bado longolongo tu zinaendea. Naomba hili lisiwe part ya mafanikio ya kisiasa kwenda 2010.
 
Date::2/14/2009
Wembe uliomnyoa Mnali utumike pia kwa akina Richmond
Mwananchi​


JUZI Rais Jakaya Kikwete alitangaza kumvua madaraka na kumfukuza utumishi wa umma aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali kwa kuamuru walimu wa shule za msingi wachapwe viboko kutokana na shule zao kufanya vibaya katika mitihani ya darasa la saba.

Hatua ya Rais Kikwete imechukuliwa huku makundi mbalimbali ya kijamii nchini, yakiendelea kulaani kitendo hicho cha kidhalilishaji cha mkuu wa wilaya kuamuru walimu wachapwe kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya rais ya kumfuta kazi na madaraka DC huyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi usiku, hatua hiyo imechukuliwa kuonyesha kwamba, serikali haikubaliani na kitendo hicho cha kidhalilishaji na kuwavunja moyo walimu, ili iwe fundisho kwa viongozi wengine.

Tunajua kuwa hatua ya rais imezingatia kanuni na masharti ya utumishi wa umma, ili kulinda mamlaka ya rais na serikali yake ambayo kazi yake kubwa ni kulinda maslahi ya wananchi wake wote, wakiwamo watumishi wa kada zote.

Tunaunga mkono hatua hiyo na kusisitiza kwamba, viongozi wote wa umma wanaotumia madaraka yao kuwanyanyasa wananchi bila kujali kada zao, wachukuliwe hatua kali kama hiyo, ikiwa ni pamoja na wanaotumia madaraka yao kulitia hasara taifa.

Kwa hatua hii tumeamini kwamba, rais ana uwezo wa kuchukua hatua wakati wowote dhidi ya wasaidizi wake wasiofuata kanuni za utumishi wa umma na hatimaye kumchafulia jina na heshima yeye binafsi na serikali yake machoni pa jamii. Kwa hiyo basi tunaomba wembe huo endelee kukata bila kuwaonea huruma baadhi ya watu.

Kwa maana hiyo basi, kama alivyofanya kwa DC Mnali, achukue hatua zinazoridhisha dhidi ya watuhumiwa mbali mbali wa ufisadi ambao ni watumishi wa umma na hasa wale waliotajwa katika kashfa ya mchakato wa umeme wa dharura uliyoipa ushindi kampuni ya Richmond na kuagiza serikali iwachukulie hatua.


Si nia yetu kumshawishi au kumfundisha rais, lakini kwa busara ile ile aliyotumia kumfuta kazi Mnali, awachukulie hatua zinazostahili watu wanaopigiwa kelele na wananchi pamoja na wabunge kuhusiana na kashfa hiyo.

Kwa mfano, katika mkutano wa Bunge uliopita, wabunge hawakukubaliana na ripoti ya serikali kuhusu utekelezaji wa maagizo na maazimio ya bunge kuhusu watumishi wa umma waliohusishwa katika kashfa hiyo ambao bado wako kwenye nyadhifa zao wakati uchunguzi unaendelea.

Hoja ya wabunge, ilikuwa ni kwanini watu hao wasiondolewe kwenye nyadhifa zao kwa kusimamishwa kazi ama kuhamishwa, ili uchunguzi ufanyike kwa haki. Hofu yao ni kwamba, wanaweza kuharibu uchunguzi, hivyo wakapendekeza wawekwe kando.

Tunakubaliana na hoja ya wabunge, kwa vile mtu yeyote anayechunguzwa huwekwa kando ya ofisi au madaraka yake ili kazi hiyo ifanyike kwa uhuru kamili.


Sasa kwa nini hao wasiwekwe pembeni wakati huu? Hapo serikali imeonyesha udhaifu unaowafanya watu wadhani kwamba, ndani yake kuna wateule wachache wasioguswa, ndiyo maana walisema hawawezi kujiwajibisha (kujiuzulu), mpaka atakapoamua aliyewateua (rais).
 
Huyu alikuwa amejiandaa kabisa kuwachapa vyema....akawaingiza kwenye darasa na kuanza kuwachapa....hivi kile kijiji kinatwaje?Vile
 
kwa bongo huyu sio kiongozi wa kwanza kuchapa watu
viboko.

alikuwepo waziri mmoja wa elimu miaka ya 1970s yeye alikuwa
anazunguka mitaani na akikuta mwanafunzi mtaani bila kibali
cha shule ni mboko tuu

alikuwepo mkuu wa mkoa mtwara nadhani miaka ya 1960s au
mwanzoni mwa 1970s na yeye alikuwa anatembeza bakora
kwa walimu pia.

sasa yawezekana huyu ex-dc alikuwa anawazimia hao jamaa
na aliona njia zao zilifanyakazi hivyo na yeye akaamua kuzitumia.
 
sasa bwana mnali kahukumiwa, je kuna utaratibu wa
kukabiliana na matatizo ambayo alikuwa anajaribu
kurekebisha? au ndio walimu watashangilia tu "mchawi"
kaondolewa na wao kuendelea na shughuli kama kawa.

mheshimiwa mbunge wa eneo hilo ni bora upite kwa wapiga
kura wako ukawasikie wao wanasema nini kwani watoto
wao ndio bwana ex-dc alikuwa anajaribu kuwasaidia. inawezekana
wao wanamuunga mkono ex-dc.
 
Kwa habari hii ni udhalilishaji wa utu wa ubinadamu!Hakuwa na mamlaka ya kuwadhalilisha hawa watumishi wa umma ambao ni nguzo muhimu katika jamii ila kuwachukulia hatua madhubuti za kisheria. Nimeona habari hii nchi za nje na mbaya zaidi imesambaa kwenye magazeti ya udaku kwa jinsi ilivyokaa. Ila nampongeza rais kwa kuona hili mapema na kumuondoa kwenye wadhifa wake!
 
Wakati kama huu shule za msingi tatu kushindwa kabisa kutoa hata mtoto mmoja darasa la saba.... nadhani mkuu wetu wa wilaya pamoja na makosa yake kweli UJUMBE umefika..
Nina hakika bila viboko hivyo tungeendelea kufikiria kwamba wahaya wenye kabila hilo ndio wa mwisho ktk elimu maanake Ndivyo Tulivyo... tunatoa credits za elimu nzuri kwa makabila au eneo badala ya kufikiria sababu zinazo tokana na...na ajabu zaidi ni kwamba wizara nzima ya elimu inashangilia kwa madaha mafanikio ya shule fulani au mkoa fulani na kubeza mikoa mingine yenye mapungufu makubwa ktk huduma hiyo ya elimu..
Na ndio maana hata siku moja tumeshindwa kuelewa matatizo yetu.. Utaona shirika la serikali likifirisika kutokana na Uongozi mbaya, tunachukua hatua za kufunga au kuuza shirika zima kisha kwa ujinga wetu tunawatumia viongozi wale wale wabovu walioliangusha shirika kuwa mawaziri, manaibu na wakurugenzi...
Ebu turudi nyuma tuangalie tulipotoka.. ni mashirika mangapi yamekufa!.. lakini zamani hao CEO wa viwanda hivyo hivyo chini ya Ujamaa leo hii ni mawaziri..
 
Mkandara naungana nawewe, nimiezi miwili tangu matokeo yatoke sio waziri wala CWT wamehoji na kuchukua hatua stahiki dhidi ya shule tatu kwa mpigo kutoa sufuri. DC alijua wazi kwa uamuzi wake atafutwa kazi lakini alisimamia dhamira yake. Kama hakuna hatua yeyote dhidi ya ukiukwaji wa haki za hawa wanafunzi then DC dhahiri kaonewa. Kwanini tuwe na "double standard"?

Mbona John Lubuva yeye kahamishwa tu au wale wananchi hawakuwa walimu?

Walimu walishalipwa stahili yao sasa mbona hawachapi kazi? kama mazingira ya kazi magumu siwaache kazi waende kufundisha st.mary's tena kule walimu wanapewa na chai ya maziwa!

Kwahiyo Mwantumu Mahiza roho yake imesuuzika kufutwa kazi DC kichaa! watoto kufeli je? yenyewe sawa tu! CWT mlishalipwa malimbikizo sasa hizi chokochoko na Kanali Albert Mnali za nini sasa? au mna jingine? CWT mnaandama itakuwa jumapili au nayenyewe nisiku ya kazi!
 
Back
Top Bottom