DC aliyewacharaza viboko walimu afukuzwa kazi

hata mimi naona huyo DC angekamatwa na wale walimu wote waliochapwa kwa amri yake wakaletwa wamchape yeye pia na issiishie hapo tu bali wapewe na fidia ya kuzalilishwa mbele ya wanafunzi wao na watoto wao
 
jamani si mmeona wananchi wa bukoba wenyewe wanampongeza DC...


acheni kutetea tu hao walimu,

Date::2/16/2009 Bukoba: DC aungwa mkono kwa walimu kuchapwa viboko *Polisi wazima mpango wa waalim kuandamana kulaani adhabu hiyo
Na Lilian Lugakingira
WAKATI walimu wa mkoani Kagera wamenyimwa kibali cha kuandamana kuunga mkono uamuzi wa Rais Kikwete wa kumvua madaraka mkuu wa wilaya aliyechapa viboko walimu, wakazi wa mjini Bukoba wamedai hatua ya DC huyo ilikuwa sahihi katika kukomesha utoro uliokithiri wakati wa kazi.
Wakazi hao wanadai kuwa walimu wengi wamejitumbukiza kwenye biashara binafsi tangu waanze kupata mikopo kutoka kwenye mabenki na hivyo kutumia muda wa kazi kwa shughuli zao binafsi badala ya kufundisha.
Kikwete alimvua madaraka mkuu huyo wa wilaya, Albert Mnali, kwa kosa la kuwachapa walimu. Mkuu huyo alienda kwenye shule tatu za Kansenene, Katerero na Kanazi na kumuamuru koplo wa jeshi aliyeambatana naye kuwachapa walimu hao viboko kwa makosa ya uzembe na kuchelewa kazini.
Walimu mkoani hapa walikuwa wamepanga kuandamana jana lakini maandamano hayo hayakufanyika kutokana na kutopata kibali cha Jeshi la Polisi, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Walimu cha Kagera, Dauda Bilikesi.
Bilikesi alisema kuwa walimu walikuwa wamepanga kufanya maandamano ya amani kulaani kitendo cha mkuu huyo wa wilaya ya Bukoba cha kuwachapa walimu viboko, na kuwa kunyimwa kibali cha kufanya hivyo ni kunyimwa haki yao ya kujieleza na kutoa hisia zao.
Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi zimesema kuwa, walimu hao walinyimwa kibali kutokana na kuhofia kuvunjika kwa amani. Hata hivyo, kamanda wa polisi mkoani hapa, Henry Salewi hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo.
Wakati walimu wakishindwa kuandamana, wakazi wa wilaya ya Bukoba wanamuona DC Mnali kuwa alifanya kitendo sahihi cha kuchapa walimu viboko, wakidai kuwa utoro, uchelewaji na uzembe umezidi.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema kuwa adhabu aliyoitoa rais kwa mkuu huyo haistahili, wakisema kuwa walimu hao walistahili adhabu hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya utovu wa nidhamu.
Wakazi hao waliitupia lawama serikali iliyopitisha utaratibu wa walimu kupewa mikopo ambao wamesema umechangia kwa asilimia kubwa walimu kukiuka maadili ya kazi yao, ikiwemo kufanya biashara saa za kazi na kushindwa kufundisha.
Helleni Lianda, mkazi wa kata Kashai katika manispaa ya Bukoba, alisema kuwa wapo baadhi ya walimu ambao wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi na taratibu za kazi, lakini walimu walio wengi wamejiingiza katika biashara na kuwa wanapaswa kuchagua moja, kama kuingia madarasani kufundisha au kufanya biashara.
"Ni haki yao kupigwa viboko; wanafanya biashara saa za kufundisha; wanafika kazini wakiwa wamechelewa; wanapiga soga kazini badala ya kufundisha. Mimi sioni sababu ya kumwadhibu DC eti kwa sababu kawapiga walimu, ni haki yao," alisema Lianda.
Naye Beatrice Mshumbusi, mkazi wa kata Hamugembe, alisema walimu walistahili kuchapwa viboko, akidai kuwa wamekuwa kero hasa kutokana na vitendo vyao vya kulewa saa za kazi, hali inayosababisha wengi wao kuwa wachafu kupindukia.
Mbali na asilimia kubwa ya watu waliohojiwa kuonekana kumuunga mkono mkuu huyo wa wilaya, wapo baadhi ambao wamesema kitendo cha kuwachapa viboko walimu sio cha kiungwana maana zipo taratibu za kumwajibisha mtumishi wa serikali anayeenda kinyume na taratibu za kazi, sio kumchapa viboko.
Baadhi ya wazazi walisema wanaandaa maandamano kupinga kitendo cha kumwajibisha mkuu wa wilaya ya Bukoba kwa sababu ya kuwapiga walimu viboko.
Mzazi mmoja wa Hamugembe aliyejitambulisha kwa jina la Athuman alisema kuwa endapo Jeshi la Polisi litatoa kibali kwa walimu hao kuandamana kuunga mkono uamuzi wa Rais Kikwete, na wazazi wataandamana kupinga hatua hiyo
 
Nilisema kuwa Mheshimiwa Raisi amefanya kosa kumfukuza DC na nilisema kuwa yule aliesema DC akapimwe akili alikuwa sawa kabisa na wale waliosema DC aadhibiwe hawakuwa tofauti na DC wote walihitaji kupimwa akili.
Majuto ya Mheshimiwa Raisi yapo wazi kwa hali inavyokuwa tete ,Wazazi /Walimu/DC/Raisi.

Raisi amemtimua DC ,walimu wamemuunga mkono Raisi ,wazazi wanamuunga mkono DC nani mwenye nguvu hapo ? Inamaana wamepinga kitendo cha Rais ,kwa maana hiyo wameipinga CCM ,hivyo DC ni more powerful tayari wananchi wapo upande wake ,Je CCM watampeleka DC mahakamani ? Je CCM watamfukuza uwanachama DC ?
 
DC Kuvuliwa madaraka haitoshi lazima afikishwe mbele ya vyombo vya dola... haki itapatikana wapi kama vyombo vya dola vinaona DC hana makosa?!?!?
 
Kutana na Albert Chipande Mnali, DC aliyechapa viboko walimu Bukoba
279_mnali.jpg

  • Sasa ni mkulima na mwenyekiti wa CCM Nachingwea
  • Asisitiza kuendelea kuwachukia walimu wote wazembe
  • Asema mikataba mibovu matokeo ya walimu wazembe

HIVI karibuni, Mwandishi Wetu Ahmed Mmow, amefanya mahojiano na Albert Chipande Mnali, kuhusu masuala mbalimbali. Mnali ndiye mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Nachingwea, aliwahi kuwa katibu msaidizi wa Bunge, ofisa mipango makao makuu ya Wizara ya Kilimo na Mkuu wa Wilaya mbalimbali nchini. Huyu ndiye DC aliyewachapa viboko walimu mkoani Kagera. Yafuatayo ndiyo yaliyojiri katika mahojiano hayo.

Raia Mwema: Kwa kifupi, tueleze historia ya maisha yako.

Mnali: Historia ya maisha yangu imekuwa ikitembea kwenye vipeperushi mara nyingi. Hata hivyo nitaeleza japo kwa ufupi.

Nilizaliwa miaka 64 iliyopita, yaani 1949 katika Kijiji cha Lipuyu kilichopo Kata ya Lionja, Wilaya ya Nachingwea. Kuhusu namna nilivyopata elimu ni kwamba nilianza shule ya msingi katika Shule ya Msingi Namalongo, sasa inaitwa Nditi, mwaka 1958.

Baadaye nilisoma katika Shule ya Msingi Liwale, kwa elimu ya kati (middle school). Elimu ya sekondari (ordinary level) nilisoma katika Shule ya Sekondari Ihungo iliyopo Bukoba. Mwaka 1981 nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa shahada ya kwanza ya mipango na uchumi (economic planning) nikiwa nimetokea kazini, nilihitimu mwaka 1984.

Mwaka 1986 nilipata scholarship ya kwenda kusomea shahada ya pili nchini Uingereza, katika Chuo cha Leicester (M.A. in economic development). Nilimaliza mwaka 1987.

Raia Mwema: Ukiondoa wadhifa wa mkuu wa wilaya ni kazi gani nyingine ulizopata kufanya serikalini na maeneo mengine?

Mnali: Mwaka 1973 niliwahi kufanya kazi Wizara ya Kilimo nikiwa nimetoka shuleni moja kwa moja (direct employment) niliajiriwa kama executive officer (ofisa mtendaji).

Mwaka 1977 nilipandishwa cheo na kuwa higher executive, niliamishiwa Mtwara. Mwaka 1978 nikiwa meneja wa kijiji nafasi ambayo ilinifanya nirudi mkoani kwangu (Lindi). Nilikuja katika vijiji vya Naipingo na Mwenge vilivyopo wilayani Nachingwea.

Mwaka 1987 niliporudi kutoka masomoni Uingereza nilirejeshwa Wizara ya Kilimo kwa cheo cha awali cha Ofisa Mipango.

Mwaka 1988 nilihamishiwa ofisi ya Bunge Dodoma, ambako nilikuwa Katibu Msaidizi wa Bunge, kazi kubwa ilikuwa ni kuwashauri wabunge kuhusu masuala ya uchumi.

Nilihudumu kwa nafasi hiyo hadi mwaka 1995 nilipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya. Wilaya yangu ya kwanza ilikuwa Njombe, wilaya ya pili Maswa mwaka 1998, wilaya ya tatu Bukombe (mwaka 2000), wilaya ya nne ni Geita mwaka 2002, wilaya ya tano Tunduru mwaka 2005 na ya sita ni Bukoba mwaka 2007, mwaka 2009 nilistaafu huko Bukoba.

Raia Mwema: Ni muda mrefu tangu ustaafishwe nafasi ya ukuu wa wilaya ukiwa Bukoba, tueleze baada ya kustaafishwa ulikwenda wapi na umekuwa ukijishughulisha na nini?

Mnali: Baada ya kustaafu nilirudi nyumbani hapa Nachingwea nilijishughulisha na kilimo. Nina ekari 15 zenye mikorosho isiyopungua 400, shamba ambalo lipo katika Kijiji cha Nangowe ambalo huwa napanda mahindi, mpunga na alizeti.

Raia Mwema: Mwaka 2010, uliomba ridhaa kwa chama chako cha Mapinduzi ili uteuliwe kuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Nachingwea, hata hivyo kura hazikutosha na Mathias Chikawe alishinda kwenye kura za maoni. Unadhani nini kilisababisha kura zisitoshe kwa upande wako?

Mnali: Kilichosababisha kura sizistoshe, sikufanya maandalizi ya kutosha. Udhaifu katika maandalizi ulisababisha kushindwa kwani wengi walikuwa hawanifahamu.

Hata hivyo, kwa sasa najiona nimefika kwa kupata nafasi ya uenyekiti wa wilaya. Nadhani nitabaki kuwa mwenyekiti na sifikirii kabisa kugombea ubunge, sifikirii kabisa. Nitabaki kuwa na nafasi hii ili niimarishe chama mpaka wanachama watakapoamua kunipumzisha. Ukweli nafasi ya uenyekiti itakoma mwaka 2017, mimi sifikirii kugombea chochote hapa kati, kabla ya mwaka 2017.

Raia Mwema: Mwajiri wako alikuondoa katika nafasi ya ukuu wa wilaya kwa kitendo chako cha kuwachapa walimu viboko ingawa labda nia yako ilikuwa njema. Ulipokeaje uamuzi wa rais ambaye ndiye alikuwa bosi wako?

Mnali: Nilipokeaje uamuzi! (anasita kidogo) nilikuwa mtumishi wa umma nikaajiriwa mwaka 1995 kutoka pale ofisi ya Bunge. Barua ya ajira ilisema kwamba wakati wowote serikali (mwajiri) ikiridhika kuwa nitashindwa kutekeleza majukumu yangu kwa nafasi ya ukuu wa wilaya, haitasita kuniondoa ndivyo nilivyopokea. Nilipokea kwa moyo mkunjufu uamuzi wa rais wangu kwani ni yeye aliyeniteua. Bila shaka alijiridhisha kabla ya kuniondoa. Naamini kabisa nia yake ilikuwa njema kabisa.

Raia Mwema: Lipo vuguvugu la wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuzuia ama kupinga gesi ghafi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, wewe ni mwenyekiti wa chama kilichounda serikali yenye mpango wa kupeleka gesi ghafi Dar es Salaam, lakini wewe ni mkazi wa wilaya ya kusini. Je, uko upande gani kati ya pande mbili za mgogoro huu… upande wa serikali au wananchi?

Mnali: Kwenye suala la gesi mimi nachelea kusema kwamba nipo upande gani. Lakini nikiri kwamba kuna utata ambao umefanywa na viongozi ambao hawakuwaweka wazi wananchi, hususan mawaziri wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara.

Nilitarajia kwamba, kwa mfano, Mkoa wa Lindi una mawaziri wawili na naibu waziri mmoja. Mkoa wa Mtwara una mawaziri wawili, hawa ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri naamini kwamba uamuzi huo ulipitishwa wakati wao walikuwapo, kwa hiyo nadhani kabla ya yote ilibidi warudi kwa wananchi waeleze wananchi kilichofikiwa, wakati huo wangeliomba Baraza la Mawaziri lisifanye uamuzi wa mwisho hadi warudi na maoni ya wananchi. Lakini hayo hayakufanyika. Mpaka wananchi wanaona wanafanyiwa ndivyo sivyo, ingawa nia ya serikali ni njema.

Raia Mwema: Ukiwa kama mwanasiasa-kiongozi wa CCM ngazi ya wilaya, kuna tofauti gani za wazi unazoziona pamoja na changamoto unazokabiliana nazo katika mfumo wa sasa wa vyama vingi?

Mnali: Tofauti na changamoto zipo wakati wa chama kimoja, chama ndicho kilikuwa kimeshika hatamu, serikali na Bunge vyote vilikuwa chini ya chama lakini sasa haiko hivyo.

Hivi sasa chama hakidhibiti Bunge, Chama kinatoa maagizo kwa serikali tu na si Bunge na kuhusu changamoto zipo, wapo viongozi ndani ya chama ni wanachama lakini wanashindwa kutofautisha wakati wa enzi za chama kimoja na vyama vingi.

Ni jukumu na wajibu wa viongozi kutambua uwepo wa vyama vingi. Vyama hivyo vipo kwa mujibu wa sheria hivyo wale watendaji walio juu yangu na wale walio chini yangu wanatakiwa kulijua hilo. Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 ipo wazi tu. Hivyo ni wajibu wetu tunaojua kuwakumbuka wale ambao bado hawajui.

Raia Mwema: Umekuwa nje ya madaraka ya ukuu wa wilaya, unadhani wakuu wa wilaya wa sasa wanachangamoto gani tofauti na enzi zenu?

Mnali: Ujue kwamba ukuu wa wilaya kazi zake za msingi ni mbili. Kwanza mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani katika eneo lake, na pili ni msimamizi wa kazi katika eneo lake, hizo ndizo kazi na wajibu wa mkuu wa wilaya. Bado kazi na wajibu wa mkuu wa wilaya hazijabadilika.

Changamoto ninazoziona ni kwamba sehemu kubwa ya wakuu wa wilaya ni wapya, pamoja na kupewa semina elekezi wanahitaji muda kujifunza zaidi, lakini jambo kubwa la kufurahisha na hapa nipongeze kwa kuwa ni wakuu wa wilaya walio wengi ni vijana wenye ari na nguvu za kufanya kazi lakini kubwa kuliko yote ni wasomi. Hivyo kukitokea upungufu kati yao ni kama kujikwaa tu.

Raia Mwema: Suala la gesi na kuyumba kwa soko la korosho kunaweza kuondoa utawala wa CCM kwa mikoa ya Lindi na Mtwara, kielelezo ni maandamano yaliyofanyika mara mbili mkoani Mtwara. Wewe unakubaliana na utabiri huu?

Mnali: Hapana sikubaliani na utabiri wako huo. Si kweli kwamba watu wa Mangalea, Nangano, Naipanga, Kiangala, Ngongowele, Lilombe na kwingineko watakihama chama kwa sababu ya masuala hayo.

Wapo watakaokiadhibu chama lakini wachache na si wote wanaoandamana ni watu wa Mtwara, ujue kuna chama kinachohubiri sera za majimbo na wanatumia suala la gesi kujinufaisha kisiasa.

Aidha kuhusu suala la korosho, suala la korosho ni la kimpito, lakini wapo watu wanajificha nyuma ya utata huu (suala hili) ili kuua mfumo wa stakabadhi ghalani ambao ni mkombozi kwa mkulima. Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi wasiingie kwenye mtego wa watu hao wanaotaka mfumo wa stakabadhi ghalani ufe ili wawadhulumu.

Kuhusu kuyumba kwa soko, si korosho pekee hata kahawa soko lake linayumba. Sasa kukiadhibu Chama cha Mapinduzi sidhani kama ni sawa. Lakini CCM haiwezi kuangalia kirahisi kama unavyodhani wewe. Chama sasa kinaongozwa na wasomi, waadilifu na wenye uchungu mkubwa na chama.

Angalia sekretarieti mpya ya chama (anageuka ukutani ofisini kwake na kuwataja majina wajumbe wa sekretarieti yaliyo kwenye bango) ni wasomi watupu hawa ambao wanaongoza chama kisayansi. Hoja ya korosho ni sehemu tu ya siasa ya uchumi (political economy) itajibiwa kisayansi wananchi wataelewa tu.

Raia Mwema: Wewe ni muumini wa elimu, hata kustaafishwa kwako kulitokana na kukazia umuhimu wa elimu ingawa kwa kuwachapa viboko walimu. Kwa sasa ni kama kuna mgongano kuhusu sera ya elimu bure ambayo inatajwa ni ya vyama vya upinzani. Makada wa CCM wanapendekeza elimu itolewe bure tofauti na sera ya CCM ambayo inataka kuchangia. Unatazamaje suala hili ambalo limewahi kuzungumzwa pia na Edward Lowassa, waziri mkuu wa zamani?

Mnali: Ajenda ya elimu bure ni ya Chama cha Mapinduzi, hayo yalizungumzwa kwenye chama. Mapendekezo hayo yamepelekwa serikalini hivi sasa suala hilo lipo serikalini na linafanyiwa kazi ili kuona utashi wake. Lowassa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, hivyo anayasoma maagizo yaliyosemwa kwenye vikao ndani ya chama hivyo hakuna geni ama analozua au kuanzisha. Anasema yaliyotokana na vikao vya Chama.

Raia Mwema: Unazungumziaje matokeo yasiyoridhisha ya kiwango cha kufaulu kwa shule za msingi na sekondari?

Mnali: Hakika sifurahishwi na hiyo hali hata kidogo, ni lazima hatua za haraka zichukuliwe, kuainisha chanzo cha tatizo na kuamua jambo la kufanya kabla taifa halijatumbukia kwenye balaa la kuwa taifa la wajinga. Jambo hili si la mchezo ni jambo serious.

Raia Mwema: Katika miaka ya karibuni kulikuwa na tabia ya migomo na maandamano ya mara kwa mara, kwa uzoefu wako unadhani hali hii inatokana na nini?

Mnali: Ni kweli kumekuwa na migomo na maandamano ya mara kwa mara wakati mwingine bila sababu za msingi. Niseme kwa kifupi kwamba haya ni matokeo ya jamii kukosa uzalendo. Hiki kizazi kinachoandamana barabarani kila uchao bila sababu za msingi ni kizazi kilichokosa mafunzo ya uzalendo, ni kizazi kilichosomea taaluma tu na wengine hawakusoma kabisa.

Mimi wito wangu ni kwamba turejeshe Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika mfumo wake wa asili kwamba ukimaliza kidato cha nne au sita, kabla hujaanza kazi unatakiwa kujiunga JKT. Isiwe jambo la hiari tukifanya hivyo tutafanikiwa. Lakini pia kuwe na mtaala kuhusu uzalendo kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.

Raia Mwema: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, kuna majina yanatajwa kutaka kuwania urais wa Tanzania. Kwa mfano, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri Ujenzi, Dk. John Magufuli na wengine wengi. Kati ya hawa, unamuunga mkono nani?

Mnali: Hata mimi nasikia wapo wanaosema rais hatatoka kaskazini wengine wanasema hawezi kutoka tena kusini alimradi tu tunasikia mengi tu. Mengine hata wewe huyajui mimi nasema tu kwamba suala la nani namuunga mkono njoo uniulize baada ya Halmashauri Kuu ya CCM kupendekeza majina matatu na kuletwa mbele yetu wajumbe wa mkutano mkuu kabla sijaelekea Dadoma, wewe njoo ama nipigie simu niulize nakwenda kumchagua nani, nitakueleza na hakika nitampigia debe nitayempenda kati ya watatu hao, lakini kwa sasa sina mtu ninaye muunga mkono ni mapema mno.

Raia Mwema: Imekuwa ni kawaida kila unapomalizika uchaguzi iwe wa serikali au ndani ya chama chenu, kuacha madonda (mpasuko) hili likoje katika wilaya yako?

Mnali: Ni kweli nakubaliana na wewe kwamba chaguzi zimekuwa zinaacha makovu. Nachingwea ni sehemu ya nchi hii kwani tatizo hilo si la eneo moja. Hivyo hata Nachingwea ipo, ujue kwamba unapoamua kugombea kuna watu wanaokuunga mkono, unatengeneza kambi lakini kumekuwa na tabia kwa walioshinda kupandisha mabega na kuwabeza walioshindwa.

Sisi baada ya kuona hali hiyo tunaamua kuwakutanisha wote waliogombea (walioshindwa na walioshinda) ili kuona uwezekano wa kuvunja kambi. Watakaoendelea kung’ang’ania kambi zao itabidi wajitoe kwenye chama chetu maana watakuwa hawakitakii mema chama

Raia Mwema: Kila binadamu analo linalomchukiza na linalomfurahisha, wewe katika maisha yako unachukia kitu gani na kwa upande mwingine unafurahia kitu gani?

Mnali: Nawachukia na kuchukia watu wanaopuuza suala la elimu. Naamini kwamba elimu ni kitu cha msingi kwa kila mtu. Hivyo nachukia na kuwachukia wale waliopewa dhamana kuhusiana na elimu wanapokwenda ndivyo sivyo. Imekuwa bahati mbaya ama kwa kukusudia, hebu nikupe mfano mmoja daktari alikufanyia upasuaji akasahau kifaa kimoja akashonea, baadaye ikagundulika utapasuliwa tena utashonwa tena na utaishi.

Mchukue mwalimu mzembe hafundishi anazembea na mwanafunzi anatoka hana maarifa wala ujuzi wowote madhara ya mwanafunzi huyu kwa taifa yakitokea tutafanyaje na mwalimu huyo tutampata wapi ili aje kukabiliana na madhara ya uzembe wake?

Ndipo ninaposema watu wa aina hiyo sina suluhu nao hata kidogo. Kwani madhara ya uzembe wao hayana tiba kuhusu nafurahishwa na nini, jibu ni rahisi tu. Ni kinyume cha wazembe nafurahia watendaji wazuri, waadilifu, wachapa kazi na wenye kujali wajibu wao hasa katika suala zima la utoaji wa elimu. Elewa kwamba hata mikataba mibovu inayolalamikiwa ni matokeo ya walimu wazembe. Huenda watendaji ni wale waliofaulu kiujanja ujanja kupitia walimu wazembe.

Raia Mwema: Una wito gani kwa serikali kuhusu malalamiko ya malipo ya korosho walizokopwa wakulima?

Mnali: Sisi kama Chama tulikwishaiagiza serikali nini cha kufanya juu ya malipo ya korosho. Desemba 5, mwaka 2012 kwenye majumuisho ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete katika kikao kilichofanyika Kilwa, Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama alikwishatoa maagizo.

Januari 6, mwaka huu wa 2013, tulipokuwa kwenye Halmashauri ya CCM Mkoa, tulitoa maagizo kwa mkuu wa mkoa nini afanye kuhusiana na suala la korosho. Maana ni kweli wananchi wanashindwa kulipa karo za watoto wao na matumizi mengine kwa sababu fedha zao hawajalipwa. Hata mimi inanisikitisha hali hii.
 
Back
Top Bottom