Dawati la msaada kwa HTC smartphones

Dawati la msaada kwa HTC smartphones

Mkuu me nna HTC one S shinda sim card slot haiwezi kushikilia sim card then nmepeleka kwa fundi kkoo anadai hamna spea yake dukani. VP hapo kuna alternative au ndo niifanye game console na Wi-Fi internet

Suluhu hapo ni kutafuta mtu mwenye HTC One S iliyoharibika but board yake iwe nzima... vinginevyo uifuate eBay zinapatikana kwa dollar 4 tu...
Link ya eBay: http://m.ebay.com/itm/321197863464?nav=SEARCH
 
...Kaka kwa utalaamu wako kuna HTC one M7 ya kichina?! Au HTC yeyote ukiiona ujue ni lazima iwe Origional

Zipo HTC One M7 feki mkuu.. tena balaa zaidi kuna wachina wanajiita HDC wapo vizuri maana wazitoa zikiwa zinafanana sana kimuonekano na zile original.. cha kufanya wewe ni kununua kwa mtu au duka unaloliamini.
Kuna baadhi ya simu kama HTC One X, One XL na One S ambazo wale wanaotengeneza feki walizishindwa kabisa...

Ukitaka kuijua HTC One feki unaweza kuangalia kioo chake kama wewe ni mzoefu wa simu utaona resolution yake ni poor.. camera pia..
Pia kwenye hizi feki ni ngumu sana kukutana na HTC Blinkfeed, HTC Zoe na features kibao za HTC kama extreme power saver mode..
 
Htc one M7 ....ni dual sim imasumbua camera haitoi picha nzuri......ukipiga inatoa rangi ya puple na red
 
Imeandika flash succefully

Vizuri, sasa ukiwa kwenye FASTBOOT mode...
Fungua command prompt kwenye ADB bundle... then type
fastboot devices..
fastboot reboot recovery
Baada ya kuingia kwenye recovery
Mount simu yako.. then storage itatokea kwenye PC yako.. copy file la Cyanogenmod...

Baada ya hapo reboot tena kwenye recovery.. install.. then chagua zip file ya Cyanogenmod.. installl...

Subiri hadi imalize... ikisema Done.. rudi kwenye main menu ya Recovery alafu reboot bootloader nenda fastboot mode..

Hapa unahitajika kuflash Boot image ya Cyanogenmod ili iweze kuwaka...
Boot image ipo ndani ya zip file ya Cyanogen uliyodownload.. kwa hiyo unzip the file.. itakua kwenye form ya boot.mmc.. badili hiyo extension ya .mmc kwenda kwenye boot.img..then hamishia kwenye lili folder la ADB (Platform tools)
baada ya hapo fungua command prompt kutoka kwenye hilo folder kwa right click then.. Open Command prompt here...
Huku simu yako ikiwa kwa FASTBOOT mode type

fastboot flash boot boot.img


then piga enter... baada ya kumaliza... restart simu yako.. tupe feedback kwa ajili ya maelekezo zaidi ya kuoata Google Apps..
 
mkuu Mars Rover ahsante kwa uzi wako,

me nina HTC one SV, ilizima ghafla nikijua ni charge imeisha, nilipochomeka kwenye umeme badae simu ikajiwasha yenyewe ila inaishia kwenye logo tu ya hTc, na kwenda kwenye factory mode, yan hai boot Os kabisa, nilijaribu ku factory reset inarudi palepale hata ukiwasha tena, tatizo ni nin mkuu...?

Ahsante

Hiyo ni kuicharaza system files mpya kuanzia recovery, boot,. na ROM

Files zake zipo hapa http://forum.xda-developers.com/showthread.php?t=2317379
 
Last edited by a moderator:
Xaxa mkuu hapa kilichotokea inaleta yale maelezo niliyo kueakea jana ikitaka kurestart
 
Yaani ikitaka kurestart inabakia pale kwenye logo na inaandika yale maneno
 
ha,ha,haaaaa,haaaaaaaaaa, kumbe zinatuhangaisha wengi,nilifikiri ni mimi tu duuuh, yangu ni htc_700 sasa siwezi kuelezea mateso inayonipa...
 
Yaani ikitaka kurestart inabakia pale kwenye logo na inaandika yale maneno

Mkuu zile steps za kuflash Cyanogenmod umefuata.. kuweka recovery ya TeamWin (TWRP) siyo suluhisho.. huo ni mwanzo tu ..
 
Mbona mie hiyo post yangu ya juu hauijibu mjomba au ndio undugulazation mpaka kwenye mitandao ya kijamii....

Hilo ni tatizo la hardware kwa M7 nyingi.., camera inaonyesha purple au pink kwenye mwanga mdogo.. tafuta fundi wa simu mwenyewe spare kutoka kwenye HTC One M7 nyingine..

Angalizo: hizi post ni kusaidiana tu mkuu.. uwe na subira na sio kufanya kama unalazimisha watu.. Sio vizuri mkuu..

Pamoja sana mkuu wangu
 
Bado inakusumbua mkuu?

ndugu yangu weee,yaani ni taabu tupu:
1: charge haikai muda mrefu na hili nimeambiwa dawa ni power bank,sasa hapa tayari natembea na kamzigo
2: juzi imepoteza whatsapp app nimekaa siku mbili kuirejesha kwa kuidownload
3:sasa kubwa ya yote kuna msg inatokea kwenye screen ikionesha kwamba "htc has lost...." ngoja hii ikitokea nitarudi kwako. ila tu inapotokea hii huwa sina control tena kwenye screen,itajizima na kujiwasha yenyewe...... aaaaagh,mkuu huwa natamani kulipiga chini
 
Hilo ni tatizo la hardware kwa M7 nyingi.., camera inaonyesha purple au pink kwenye mwanga mdogo.. tafuta fundi wa simu mwenyewe spare kutoka kwenye HTC One M7 nyingine..

Angalizo: hizi post ni kusaidiana tu mkuu.. uwe na subira na sio kufanya kama unalazimisha watu.. Sio vizuri mkuu..

Pamoja sana mkuu wangu

Ahsante Mkuu ntalifanyia kazi..

Nisamehe bure mjomba nilikuwa nakutania flani hivi sikumaanisha, najua sana unasaidia na mungu akubaliki kwa msaada unaoutoa
 
ndugu yangu weee,yaani ni taabu tupu:
1: charge haikai muda mrefu na hili nimeambiwa dawa ni power bank,sasa hapa tayari natembea na kamzigo
2: juzi imepoteza whatsapp app nimekaa siku mbili kuirejesha kwa kuidownload
3:sasa kubwa ya yote kuna msg inatokea kwenye screen ikionesha kwamba "htc has lost...." ngoja hii ikitokea nitarudi kwako. ila tu inapotokea hii huwa sina control tena kwenye screen,itajizima na kujiwasha yenyewe...... aaaaagh,mkuu huwa natamani kulipiga chini

Hahaha.. usipige chini, hiyo ni HTC mkuu.. itunze
 
Back
Top Bottom