DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Hivi DAWASCO HAMTAKI KUTATUA TATIZO LA HAPA TABATA KISUKURU eneo la KILIMANJARO? Kwa nini mnaendelea kutupa adhabu ya kutunyima huduma ? Tunaomba mjitafakari kabla UVUMILIVU WETU haujafikia kikomo
 
Hili shirika nalo ni tatizo jingine kwa wateja waona Watanzania kwa ujumla,mfano unakuta maji yanatiririka kuoka kwenye bomba lao kubwa yanajaa mitaani na mitaro ya maji machafu,yanaonekana na kila mwenye uchungu na nchi hii hata kipofu anahisi maji kumwagika hovyo,hapo hapo kuna wenye kuhitaji huduma ya maji yao lakini ukifuatilia ofisini kwao ni sound tu unapigwa,kusoma mita nako ni shida,badilikeni kabla nyakati hazijawabadiliha,ninaishi Vituka
 
Hivi DAWASCO HAMTAKI KUTATUA TATIZO LA HAPA TABATA KISUKURU eneo la KILIMANJARO? Kwa nini mnaendelea kutupa adhabu ya kutunyima huduma ? Tunaomba mjitafakari kabla UVUMILIVU WETU haujafikia kikomo
Tumelipokea tutalifanyia kazi mapema
 
Mradi bado haujakamilika..ukikamilika tutawataarifu wananchi ili waje kujiunga na wapate huduma ya maji
 
Tumekusikia ndugu yangu..tunaahidi kuboresha huduma na kuondoa kero hizo za bili ya maji
 
Chanika hamna maji na sijasikia kama mna mpango wowote ule wa kuleta maji.Tunaomba mtujuze lini mtatuletea maji?
Kukamilika kwa visima vya mpiji na mpera kutasaidia upatikanaji wa maji maeneo ya chanika na maeneo jirani
 
Tunaomba account namba yako pamoja na mawasiliano yako tuweze kukuweka kwenye system
 
Mradi bado haujakamilika..ukikamilika tutawataarifu wananchi ili waje kujiunga na wapate huduma ya maji
Ahsante kwa kupata muda wa kujibu.
Bado nataka kujua 'time frame' kwa sababu kuna maamuzi ya kugharamika nahitajika kufanya juu ya suala la maji. Nikifahamu muda itanisaidia. DAWASCO
 
Kuna mto umepita maeneo ya Msewe, huu mto huwa haukauki hata kipindi cha kiangazi hapa dar, mwisho wa siku umebatizwa jina na kuitwa MTO WA DAWASCO.
Hii ni kwa sababu ya kutiririsha maji ya bomba ya Dawasco kila kukicha, sijui kama mnafanyaga hata kitu inaitwa Water auditing !
 
Msewe sehemu gani
 
Rudia text Yangu kusoma nafikiri hujaielewa, ungenielewa usingeuliza hili swali
Msewe kubwa..sema mtaa ulipo huo mto ili iwe rahisi kwa mafundi kufika..text yako tumeisoma hatujajua msewe ipi
 
Msewe kubwa..sema mtaa ulipo huo mto ili iwe rahisi kwa mafundi kufika..text yako tumeisoma hatujajua msewe ipi
Naposema mto umepita Msewe simaanishi mto upo msew Bali umepita Msewe elewa hilo, huu mto bila shaka umepita maeneo mengi kuanzia Kimara huko, njoo maeneo ya Golani mpaka huku Msewe, hii inamaana maeneo hayo yaliyopitiwa na MTO huo hutililisha maji ya bomba zenu season zote,
Hapa sio ishu ya msewe pekee ni mjumuiko wa maeneo Mengi ambayo inaonekana Miundo mbinu yenu imeharibika na hamfanyi survey za kutosha kujua ama kupewa info na wananchi wanaozunguka miundombinu yenu.
Mi Naku alert tuu, we jalibu kufanya huo utafiti, najua dar hamna mto wenye annually flow of water lkn utashaangaa huu mto hutoa wapi maji kipindi cha Kiangazi ! Jibu nishakupa ,fanyieni kazi.
 
Asante sana tunaifuatilia na kuhakikisha maji hayapotei tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…