Dawa ya Lowassa yapatikana

Dawa ya Lowassa yapatikana

Kwahiyo strategy CCM watajimaliza mapema sana!! Why? LOWASSA NA UKAWA wataweka hadharani mambo ya Escrow, uhusika wa mkulu Richmond, Ufisadi katika miradi ya barabara(Magufuli), uuzaji wa nyumba za serikali(Magufuli), Utajiri wa kutisha wa JK kupitia Rizimoko!!

Kwa kifupi, Ukawa wataelekeza silaha zao kushambulia mfumo wa CCM kama chama then Magufuli personally. Therefore wana two points of attack!!! CCM on the other hand wana one point of attack....kumshambulia LOWASSA personally only if they really need to destroy UKAWA!!!
VUTA-NKUVUTE
 
Last edited by a moderator:
VUTA-NKUVUTE

Mgombea wa ccm aliahidi kutofanya kampeni za kuchafuana,
je wameamua kumuasi hata kabla kampeni hazijaanza?
Na je lowasa akiwavua nguo zaidi itakuwaje?
maana katika list uliyoitaja hakuna aliyewahi kuwa karibu
na ikulu kuliko lowasa,ukombozi wa tanzania tuitakayo umekaribia.
 
Last edited by a moderator:
mnaacha kutafuta dawa ya umaskini wa watanzania mnatafuta dawa ya kumzuia lowasa. hakika nipo kwenye mipango ya kuhama nchi nikaishi somalia

Nyuzi saba si nyingi sana tulia ushonwe, siasa inakaribia kuanza na hapo ndo mtaelewa siasa maana ake ni nini
 
the downfall of ngoyai is imminent

Watamuua jamani make alishajiaminisha sasa siasa inaanza rasmi ..hiyo ndo CCM Afrika nzima hakunaga tena ..mtu mmoja atasumbuaje wazee wazima?
 
1. olesendeka kapigwa mawe juzi na wananchi
2. mwigulu alikamatwa na pccb kwa rushwa
3. nape alikamatwa na pccb kwa rushwa
4. mwakembye hakumalizia kutuambia ukweli kwenye richmond
5. sita kaharibu mchakato wa katiba mpya....
6. kibajaji...........Nacheka.......utamalizia wewe

YUPI KATI YA HAO ANAEWEZA KUWASHAWISHI VIJANA......
MWAKA HUU MNALO WAKUU....MWENYEKITI WENU SHATI LINA MZIDI KIMO.....HAHAAAA
 
hiyo itakuwa powa sana na kama itafanyika hivyo basi ni nzuri sana kwa munufaa ya watanzania wote na kwataifa. hakika ile siri na sintofaham ya mda mrefu soon itafahamika maana hakika mashaka yote kuhusu lowasa yataanikwa na vipi yy fisadi itafahamika na lowasa naye najua kamwe hata kaa kimya atajibu mashambulizi sasa hapo ndio patamu yale mambo ya mwaga ugali ni mwage mboga ndio yatakapotokea so suala la RICHMOND litakuwa wazi kabisaaa maana hata bunge lilishindwa kutuwekavwazi nani mhusika mkuu
AYAA.. hakuna atakae baki hata mwakyembe atakwenda na maji kwa kuficha uchafu mfukoni a.k.a mavi na yeye ni mchafu.
LOWASA KAMA NDIO wa kwanza kujitosa uwanjani na kusema mwamba ajitokeze nina hakika ndani ya nafsi yake ni msafi 100% vinginevyo asinge take mo e.
NASISITIZA WATABAKI KULOPOKA PEMBENI KATI MAHAKAMANI ASOGEI MTU.
SASA KWA TAARIFA ATAKAE ROPOKA ATAFUNGULIWA MADAI MAHAKAMANI ASIBITISHE.
Mwaka huu kitaeleweka. wasogee uwanjani
 
Mafaili yao wote mbona yamejaa hilo sio tatizo waseme ili wananchi tujue mbivu na mbichi lakini mwisho wa siku ukawa wanatinga ikulu asubuhi na mapema walaji wa habari ni sisi wananchi natutakao toa kura ni sisi wananchi
 
Kwa upande wangu siwezi hata kuwasikiliza. Aliwezsje kuwa mbunge! pia, kwa nini hawakumfichua mapema katika kura za maoni 2010? Amekuwa FISADI baada ya kuingia CHADEMA? Watanzania wa leo siyo wa karne 19!
 
Taifa linapoacha misingi ya kuongozwa kwa kufuata sheria na kufuata fitina na majungu ni hatari.
 
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

unaota wewe itakuwa
 
Ukawa wana simple strategy, ni kupeleka moto mkali kwenye majimbo ya hao wapambe
 
CCM mmeshachelewe ni heri mkubali tu kwamba imeshakula kwenu
 
Kwahiyo strategy CCM watajimaliza mapema sana!! Why? LOWASSA NA UKAWA wataweka hadharani mambo ya Escrow, uhusika wa mkulu Richmond, Ufisadi katika miradi ya barabara(Magufuli), uuzaji wa nyumba za serikali(Magufuli), Utajiri wa kutisha wa JK kupitia Rizimoko!!

Kwa kifupi, Ukawa wataelekeza silaha zao kushambulia mfumo wa CCM kama chama then Magufuli personally. Therefore wana two points of attack!!! CCM on the other hand wana one point of attack....kumshambulia LOWASSA personally only if they really need to destroy UKAWA!!!

Unaweza usione ugumu wa chadema/ukawa kwenye suala la kukanusha tuhuma zao za mwembe yanga zilizotolewa na katibu wao Dr.slaa huku zikikolezwa na viongozi wao kama lema,msingwa na mnyika, najua wale wafuasi wafia chama hawataelewa ila kuna kundi lisilo na msimamo wowote wa kiitikadi/kichama wataelewa mantiki hiyo.
 
Mkuu nadhani unasahau point ya msingi, point hapa si ufisadi..Mark my words, watu wanaona ni bora huo ufisadi ufanywe na mtu wa chama chochote hata UDP lakini siyo na mtu kutoka CCM, so point hapa si ufisadi. Na hili ndilo CCM mnakosea mnadhani watu mnashindana na watu kwa moja, yaani mwe na hoja msiwe nayo issue ni kutoa CCM madarakani tu.

Usiombe kufanya ushindani na mtu aliyekata tamaa, na watu wamekata tamaa na CCM.

Kukata tamaa ni tatizo la kiakili tu ambalo linaweza kutatuliwa kwa masaa machache tu na mtu mwenye kujua kucheza na akili, ndio maana kuna ujanja mwingi sana kwenye siasa na lengo ni kubadilisha fikra za watu au kuwafanya watu wakate tamaa na maamuzi yao..

Baada ya magufuri kuteuliwa na ccm hata waliokuwa mashabiki wa chadema walianza kumuita ni jembe na wengi walisema wangempigia kura lakini lowassa amebadili upepo kwa kuwa ccm baada ya kumteua mtu wao wakaamua kuwa kimya ambacho kinawafanya wapinzani wasikike.

Kwahiyo hilo la kusema watu wanataka ccm ing'oke halina ukweli kamili bali ni mitazamo ya mashabiki wa upinzani. Kila mtu yupo upande fulani kwa maslahi fulani lakini kutumia wingi wa wananchi kupata hitimisho la kuichoka ccm sio sahihi.

Leo si ccm wala cdm/ukawa wanaoweza kuwashawishi wananchi wote wafuate matakwa yao.
 
Back
Top Bottom