Dawa ya Lowassa yapatikana

Dawa ya Lowassa yapatikana

Sidhani kama watakuwa na uwezo wa kujibu maswali au kufafanua sababu ya kuanza kumuanika sasa.
 
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Yangu macho nasubiri kwa hamu nione jinsi anavyosambaratishwa mbona ijumaa ijayo mbali.
 
VUTA-NKUVUTE

Watuwekee wazi kwanza waliochikua zile bilions za Escrow za stanbic ambapo kumekuwa na kigugumizi mpaka leo!

Pili wamsaidie magufuli kuelezea matumizi halali ya zile 252b ambazo alidanganya bunge na ukaguzi wa CAG wa january mwaka huu umegundua kuwa matumizi ya kiasi kikubwa cha hiyo hela hayaeleweki.

Tatuwatuelezee vizuri tuhuma za mgombea wao kuuzia nyumba ndugu zake waliokuwa wanafanya kazi tempo wizarani kwake! Na jewatarejeshanyumba za serikali ambazo walijiuzia kwa bei waliojipangia wenyewe! Na wawaeleze watanzania hasara iliyopatikana mpka sasa ya mawaziri kuishi hotelini kwa miaka mingi kisa hamna nyumba! Nasikia kuna waziri amekaa hoteli mpka bill ikafika 100m !

Kimsingi ccm wametosha acha wajaribu na wengine tuone jamani!
Your statement is not final and conclusive
 
Last edited by a moderator:
CCM kamwe haitaweza kumgusa Lowassa kwa tuhuma za ufisadi katika kampeni zake...

Wanajua tu kuwa wakimgusa Lowassa katika hilo maana yake wanaugusa moyo wa CCM moja kwa moja...
 
CCM vs CCM B,,, kazi kweli hapa hawa ccm B kila ukiwauliza kitu wanakwambia mbona ccm nao wanafanya hizo,,, Lowassa fisadi utasikia oooh mbona Jk naye fisadi yaani unahalarisha wizi eti kwa kuwa baba mwizi duh hii kali na sijui huu ni ukombozi au mapinduzi wapi???,,, jinga vs jinga..
 
Kumbe chama kinajua majizi lakini hakiwashughulikii mpaka wahame. Mimi kura yangu nitampa yeye aliyeamua kuachana na kambi ya wanaolinda majizi na kujiunga na jeshi la wokovu.

Ahsante Mkuu... umeiona hii hoja muhimu
 
Dawa ya moto ni moto. Mapambazuko hayazuiliki kwa pazia. Kama kumekucha ni kumekucha tuu. Mwanga utapenya popote
 
unanuka ufisadi na unakosa uzalendo etiii msaf,mtu hafla zote huchangia mamilion ya hela,ameikamata serikali anageuka mungu mtu na watu wanamsujudia kwa lipi hasa alilolifanya kubwa katika taifa hili?hv kwel makada wa ccm wakubali kuhama kumfuata EL bure bure tu hebu kasome tena
kila mtu na imani yake kama unavyo sali magharibi na mimi nina mashariki hujalazimishwa lowassa ni msafi kabisa na ndiye rais ajae!!
 
Mkuu acha roho mbaya wewe unasali kila Sikh mbona unakuwa Na roho mbaya?
 
ccm itajivua nguo yenyewe! lowassa anayajua maovu mengi ya viongozi wa ccm!!hacha warushe mawe wakati wanaishi kwenye nyumba ya vioo.
 
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
[/QUOTE

Ufisadi sio issue tena kwa Lowasa.kwa kadi ccm wanavyozidi kumzungumzia Lowasa actually wanamjenga zaidi ya kumbomoa. Shida ni kwamba Lowasa amekuwa nje ya serikali miaka 8 lakini bado kuna ufisadi mkubwa sana wa escrow.Kwa upande wangu naona issue ya ufisadi itaiumiza ccm zaidi kuliko Lowasa.unapozungumzia ufisadi wa Richmond ambao hakuna hata senti moja iliyoibiwa lakini ukasahau escrow ya mwaka jana iliyo fisadi 320 billion una matatizo.
 
Salama ya ccm ni kuacha kabisa kuzungumzia ufisadi maana nyumba yao ni ya vioo.wakijaribu kurusha mawe matokeo yake ni nyumba ya ccm yote itabomolewa
 
Ccm wana kazi kubwa ya kuwambia watanzania ni nini wamesahau huko ikulu maana wamekuwa kwa miaka 54. Kama kwa miaka 54 wameshindwa kuimarisha shule, wameshindwa kuimarisha huduma za afya, wameshindwa kuondoa umasikini badala yake umaskini umeongezeka zaidi.umeme bado ni issue.watatuhakikishiaje kuwa wanaweza sasa kama Wameshindwa kwa miaka 54 . CCM ina kazi kubwa na ngumu kuwadanganya tena watanzania kuwa watafanya kilicho washinda kufanya kwa 54 years kukifanya in 5yrs. Lakini watanzania watakuw wajinga mno kama watakuwa tayari kudanganywa tena na wakakubali kudanganywa.
 
Ccm wanatakiwa kuwa wapole tena waigize kama wale wagombea walioonekana wakiwapigia magoti wapiga kura wakati wa kuomba kura ndani ya ccm.ccm wakijaribu tu kuwa wakati imekula kwao.
 
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mkuu nakuaminia sana. List iliyotoka leo uliowataja wapo wote na ziada ila wanajisumbua sana kwani it's too late sasa. Kwanza 79% ya wapigakura wameshaamua watakayempigia kura na hawabadiliki.
 
Nimechunguza wote walioteuliwa kuwa kwenye timu ya kampeni ya ccm.nimegundua jambo moja hakuna hata mmoja anaeweza kumrushia jiwe Lowasa maana wote ni kama wale waliompeleka kwa Yesu yule mwanamke waliyemtuhumu kutenda dhambi ya uzinzi. Yesu aliwauliza neno moja tu kama yupo ambaye hana dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe.kilichofuata badala ya kurusha jiwe wote waliondoka na kumwacha yule mwanamke na Yesu. Ninacho maanisha hapa ni kwamba hakuna msafi anayeweza kumrushia Lowasa jiwe katika wote.
 
Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu sana kwa ccm kwa sababu vijana wanachuki iliyotokana na ahadi zisizotekelezeka kwa muda mrefu.kuna mambo machache ccm wamefanikiwa mfano ujenzi wa barabara.Lakini barabara sio hospitali, barabara sio shule nzuri, barabara sio maji safi.ccm watakuwa na kazi ngumu ya kuwaaminisha watanzania kuwa umasikini wao haujasababishwa na wao
 
Back
Top Bottom