Hayo maswali ni mepesi sana kuyajibu
1. Walimkata kwa sababu wanazojua wao! Hawakuwaeleza wanachama wao au hata wagombea! Kina Pinda, mwakyembe, sitta hata judge Augustino Ramadhani, Mwingulu walilakatwa bila kujitete! Mzee wangu Mwandosya naye alikatwa bila huruma. Hilo ukitaka walijibu litakula kwa ccm.
2. Alikuwa anakubalika miongoni mwa wagombea wote! Hilo latosha kusubiri hadi uone mwisho wake. Sio kuwa hakujua watamkata hapana! Hata JK alishasema mipango ya kuondoka ilishapangwa siku nyingi! Alisubiri ili litimie neno lililosemwa na manabii kuwa ccm ni mafia
3. CDM kama chama cha siasa kazi yake ni kushambulia na kukichafua chama pinzani ili kionekane hakifai mbele ya macho ya jamii! Kuna vitu vingi Dr Slaa alishasema na ushahidi kuwa anao lakini hajavitolea ushahidi! Unakumbuka wakati wa uchaguzi 2010 alisema anazo takwimu za kuwa alishinda lakini hadi leo hakuzitoa! Kuna vitu kweli babu alikuwa analishwa na anaropoka bila kuwa na ushahidi! List of shame inasemekana iliandaliwa na Lisu. Kuna possibility ushahidi wa moja kwa moja hawakuwa nao bali walilishwa sumu ya ripoti ya mwakyembe! Hilo sio tatizo kwenye politics!
4. Kuhusu Slaa na Lipumba, hiyo ni mitifuano ya kugombea uraisi! Slaa alishajiandaa sana kugombea na utakumbuka hata ziara zake za kwenda US zilikuwa moja ya mikakati ya maandalizi! Ujio wa Lowassa ulimpokonya nafasi hiyo! Siamini kama Slaa amezira kwa sababu Lowassa kaja Ukawa, ameziri kwa kuwa Lowassa kapewa nafasi ya kugombea uraisi. Lipumba alikuwa na mipango miovu dhidi ya chadema. Sidhani kama kukubali kwake kumuachia Slaa ilikuwa genuine, ukumbuke yeye na bwana mkubwa ni marafiki! Alikuwa atumiwe kuipasua Ukawa! Slaa angechukua form na lipumba naye angechukua! Maalimu Seif aliliona hilo na akacheza alivyocheza, lipumba akaangukia pua.
Ni vyema watu wakatambua muungano wa ukawa ni tishio kubwa kwa ccm! Linaunganisha vyma vikubwa viwili vyenye wafuasi wa dini kubwa mbili! Cuf inahusishwa na uislamu, cdm inahusishwa na ukristo! Hili ni kweli halina ubishi kwa kuwa hiyo mijadala ipo! Ukiwaunnganisha hivi vyama unapata matokeo mazito toka pande mbili na kuondoa dhana hafifu inayotumiwa na wanasiasa uchwara kuwa ni vyama vya dini fulani. Ccm haiko comfortable kuona huo muungano unadumu. So ni vita!!!