Dawa ya Lowassa yapatikana

Dawa ya Lowassa yapatikana

Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa
Sitta, Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Labda hao wengine lakini Sitta na Mwakyembe sio wapambanaji wa ufisadi bali washiriki. Sitta nyumba ya Spika na Ofisi ya Spika kwao Urambo ni wizi wa waziwazi, mabehewa fake ni uhaini wa kutupwa; Lowassa akiingia tu, huyu jamaa tunampeleka Korea ya Kaskazini akapigwe kombora la kudungulia ndege.
 
ukweli wa ccm leo utakuwa uwongo wenye kunuka mbele ya wa TANZANIA !!
LOWASSA NI MTU MTAKATIFU NDANI YA NAFSI ZA WATANZANIA 80% WATAKACHO ONGEA CCM MDA HUU NI SAWA NA MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA!!

kusema uongo ni dhambi ha km ni mzaha.... imani ya dini yangu huniambia... kwa kauli hiyo kwa ushahidi wa MUNGU aliyejuu kuwa lowasa si fisadi????
 
pande hiyo akina nape mropokaji na nchemba na sitta pande hii watu mahiri akina tundu antipasi, john john professa safari jussa ismail kwa hiyo ninyi semeni uongo na uzushi sisi tunakuja kupangua uongo wenu na uzushi wenu kwa hoja na data zilizokamilika. ifikapo oktoba 25 mtajua kama yenu ni dawa au pipi
Usimsahau kiungo mkongwe maalim Seif kati kati. Hii timu ya UKAWA sijui utaiambia nini.
 
hakika hapo ndipo EL anapo pasubiri kwa hamu kubwa.
tangu ajiunge UKAWA,mda wote ukisikiliza kauli zake,amekuwa makini sana kuchagua/kuchuja maneno ya kuongea.ila round hii,bila shaka hatachagua pa kupiga.ataongea chochote kitakacho mjia ktk akili yake.maana anaijua CCM kimk*ndu kimk*ndu.na anajua maovu wa viongozi wakubwa wa CCM kimat*ko kimat*ko.
vita ya kuchafuana sasa itaanza rasmi.acha niandae popcon za kutosha.
A%20S%20103.gif
 
VUTA-NKUVUTE

Kila chama kinatafuta mbinu ya ishind ccm ikija hivi ukawa inakuja kivingine zaidi na kwa tarifa yako ukawa kwa sasa ndio habari ya watz hatusikii wala hatuambiwi kuhusu ukawa.wape tarifa wana lumumba wenzio.
 
Last edited by a moderator:
kusema uongo ni dhambi ha km ni mzaha.... imani ya dini yangu huniambia... kwa kauli hiyo kwa ushahidi wa MUNGU aliyejuu kuwa lowasa si fisadi????
Wewe unaye sema Lowassa ni Fisadi ndio utueleze huo ukweli wa mungu wako...! Mnafiki wewe usitaje jina la mungu bure..!!
 
Lakini watafute na majibu ya swali la
1. " Kwa nini iwe sasa??!!"
2. "Je asingehama!!??"
Na wewe ututafutie majibu ya maswali haya:-
1. Kwa nini walimkata asigombee?
2. Kwa nini alisubiri akatwe ndio haondoke?
3. Kwa nini ukawa walikuwa wanasema kwa nguvu zote wana ushahidi wa yeye kuhusika na ufisadi lakini sasa wanaubishia?
4. Kwa nini wazee kama Slaa na Lipumba wanakaa pembeni?
 
Itakuwa too late maana naona kabisa watanzania hata waambiwe nini na CCM ukweli wake unageuka uongo na uongo wa CDM unakuwa ukweli. take it from me.
 
Watuwekee wazi kwanza waliochikua zile bilions za Escrow za stanbic ambapo kumekuwa na kigugumizi mpaka leo!

Pili wamsaidie magufuli kuelezea matumizi halali ya zile 252b ambazo alidanganya bunge na ukaguzi wa CAG wa january mwaka huu umegundua kuwa matumizi ya kiasi kikubwa cha hiyo hela hayaeleweki.


Tatuwatuelezee vizuri tuhuma za mgombea wao kuuzia nyumba ndugu zake waliokuwa wanafanya kazi tempo wizarani kwake! Na jewatarejeshanyumba za serikali ambazo walijiuzia kwa bei waliojipangia wenyewe! Na wawaeleze watanzania hasara iliyopatikana mpka sasa ya mawaziri kuishi hotelini kwa miaka mingi kisa hamna nyumba! Nasikia kuna waziri amekaa hoteli mpka bill ikafika 100m !

Kimsingi ccm wametosha acha wajaribu na wengine tuone jamani!

Mwisho atueleze sababu iliyomsukuma aweke taa za kuongozea magari kijijini kwake wakati hakuna msongamano hata wa baiskeli,wakati miji mingi mikubwa hapa Tz inamsongamano na hakuna hata dalili ya kuwekewa taa za kuongoza magari.
 
mwakyembe sitta wataanzia wap kumpiga lowasa...waanze kumpga kikwete kwanza mwenye richmond la sivyo tutamrudisha bilali aje awavue nguo kuanzia kikwete na wazee wa kitengo
 
Mmechelewa sana sana ...... Mlikuwa wapi miaka yote hiyo???? Watanzania wa sasa wameamka.

Shift Delete Sisiem
 
Na wewe ututafutie majibu ya maswali haya:-
1. Kwa nini walimkata asigombee?
2. Kwa nini alisubiri akatwe ndio haondoke?
3. Kwa nini ukawa walikuwa wanasema kwa nguvu zote wana ushahidi wa yeye kuhusika na ufisadi lakini sasa wanaubishia?
4. Kwa nini wazee kama Slaa na Lipumba wanakaa pembeni?

Inaonyesha kina cha hoja ya OLESAIDIMU kimekuwa kirefu kwako.
 
Last edited by a moderator:
Mhh!, Lowassa kawa mchafu leo kwa CCM vile kahamia upinzani? Jana akiwa CCM tena Kada, hawakuyaona hayo ! Ina maana CCM inafuga Mafisadi? Baada ya kuondoka mnayemwita fisadi " LEO "wamebaki wasafi wangapi? Sitaki kukuamini lakini kama ndiyo Mikakati, tutawauliza kwa nini aliendelea kuwa Kada wa Chama? Kwa hiyo ninyi mafuga Mafisadi? Je, asingekihama Chama hayo mgeyaibua? Kama ndiyo mlikuwa mnasubiri nini tangu hiyo kashfa iibuke hadi leo miaka isiyopungua 8!! Aluta Continua. Lowassa Raisi Wetu!!
 
VUTA-NKUVUTE

Labda watoe hadharani orodha ya waliogawana ESCROW kupitia stanbic bank. Hapo ndipo wataweza kumdhibiti Lowasa
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Nikunyume chake, sio dawa ya Rais Lowassa, bali ni dawa ya ccm kufungasha viragu. Niheli tuone mengine mapya. Umasikini, njaa, maji kukosekana nchi nzima. Bado wana taka kukaa kwenye madaraka. Hawana jipya ni aibu tupu na ccm. Barabara nyingi zipo chini ya kiwango ni ufisadi mtupu. Miaka yote hii barabara ya mlandizi chalinze imewashinda. Maji Dar na miji mingine ni kitenda wili. Shule zote za serikali hazina madawati miaka nenda rudi. Escrow ndo hizo, watu kupiga hela tuu. Hakuna kingine ambacho kikwete anaongopa kama sio kwenda the Hague. Rais eti anaaga nchi za nje ulishaona wapi? Yote hio ni ufisadi waku piga hela tuu kuifilisi nchi. Ni aibu yao ccm, mwaka huu waondoke wamejaza matumbo yao vyakutosha. Yeyote anaeshabikila ccm, basi jua anamrija ana nyonya huko. Ukawa hoyeeeeeeee! Sasa rais wa nchi kabakia kwenda kwenye matasha, dah! Nchi hii ni shiiiidaaaaaaaaah. Lowassa njo utuokoe.
 
Back
Top Bottom