Dawa ya Lowassa yapatikana

Dawa ya Lowassa yapatikana

Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hao waliotajwa wanafanana na Lowassa, yawezekana ikawa sababu ya kuchaguliwa. Wakikatwa nao watahamia upande wa pili.
 
CCM wamechelewa sana. Na chochote kiovu watakachosema juu ya Lowasa itakuwa ni ule usemi usemao " MFA MAJI......................."

Kama Lowasa ni fisadi kwanini hawajampeleka mahakamani?

Waache umbululu, maana raisi si ametoka ccm? sasa iweje Raisi ambaye ni Amiri jeshi mkuu ashindwe kumkamata mtu ambaye wanasema ni fisadi?

Au tuache ili lidiirike lile neno alilosema John Mnyika "Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa JK"
 
LUMUMBA, mtatokwa na mapovu ... EL anasubiri kuapishwa tu. LUMUMBA ni shimo la panya,nyoka,panya buku, mijusi SHIMO HILI LIMELETA HASARA KWA TAIFA HILI.
alaniwe mwenyekiti taifa wa ççm, na mke wake ! tuseme amina .
 
Leo hii wakupiga kampeni watakuwa Olesendeka, Sitta na Mwigulu...???
Vuta-Nkuvute naona CCM wanajiandaa kupoteza muda wao kumtangaza Lowassa badala ya Dr. Magufuli...
Wananchi walishajua fisadi ni nani na yupi anasingiziwa...

Karibuni uwanjani...

Sendeka jimboni kwake Milya anakula sahani moja achague moja kujitetea mwenyewe au chama
 
Kikwete analo hili.
Sisi tunakwenda na Lowassa kwa mwendo wa Mchaka Mchaka mpaka Ikulu. Lowassa ni Rais anayesubiri kuapishwa!
ama kweli dunia inazunguka,hii leo mimi na mzee wa chooni tunaongea lugha moja ya kuiondoa ccm madarakani!!!!
 
""Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye"" hawa jamaa kama Magufuli atawatumia basi atapigwa mapema tena ataanza kuzomewa katika kampeni zake.
 
Kumbe chama kinajua majizi lakini hakiwashughulikii mpaka wahame. Mimi kura yangu nitampa yeye aliyeamua kuachana na kambi ya wanaolinda majizi na kujiunga na jeshi la wokovu.
 
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hapo kwenye red mkuu utakuwa unawadanganya, wakibandua tu mguu majimboni kwao wanakuta ilishakula kwao. Nakwambia hawa kwenye majimbo yao watakuwa wanapumulia mashine, sasa sijui kama wataweza kutembea na mitungi ya gesi huko wanakoenda kumnadi mgombea wao!! Ole Sendeka yuko mikononi mwa Milya, Mwigulu mikononi mwa Mrs. Tumbili, Nape kanyea kambi kule Mtama atakuwa anapambana na UKAWA huku Mathew akipiga beki 3 sasa sijui atachomokea wapi? Kwa ufupi Magufuli atakuwa mpweke!!
 
Naam mi huwaambia vijana wenzangu mafuriko yatawarudia CCM ni strategic political party,wao wameng'ang'ana UKAWA wakati sio chama hicho bali kamakubaliano ka wapinzani."mtu mlafi hakatazwi kula,ila kushika chungu ni marufuku"(inamhusu mh.wao)!
 
CCM wamechelewa sana. Na chochote kiovu watakachosema juu ya Lowasa itakuwa ni ule usemi usemao " MFA MAJI......................."

Kama Lowasa ni fisadi kwanini hawajampeleka mahakamani?

Waache umbululu, maana raisi si ametoka ccm? sasa iweje Raisi ambaye ni Amiri jeshi mkuu ashindwe kumkamata mtu ambaye wanasema ni fisadi?

Au tuache ili lidiirike lile neno alilosema John Mnyika "Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa JK"

Nyie UKAWA hamjui mnajitukana Dk.Slaa ndo awe wa kwanza kufungua kesi,alaf CHADEMA..mmesahau ya mwembe yanga hahaa,tambua CCM sio mahakama bali chama cha siasa!..tutamsema kwa tabia yake tu ambayo hayati baba wa taifa aliwahi kuiona....uchu wa madaraka! na pesa!
 
Mkuu hiyo ndio siasa uchwara , jiuleze je Lowassa angebaki ndani ya ccm Chadema wangemsafisha.
Kweli kabisa, na ndio maana siku zote hamna mwenye nia njema na mateso ambayo wananchi tunayapata kwenye hii nchi, hawa wanasiasa wote wana malengo yao binafsi wao, familia zao na jamaa zao ila wanatutumia sisi kama mtaji tu. Huwa sipendi ninapoona wanatudanganya leo mtu fisadi kisha kesho mtu msafi au kinyume chake.
 
Nilidhani CCM inafanya kampeni za kumnadi Dr. Magufuli ikimuonesha ni bora kuliko Lowassa. Kumbe wanataka kumuonesha Lowassa ni mbaya/fisadi ili Dr. Magufuli apite. Hii inafanana kabisa na mapingamizi waliyokuwa wanaweka Uchaguzi wa serikali za vijiji na vitongoji mwaka jana.

Nilidhani sera za CCM ndizo zitashindanishwa na za UKAWA. Kuna kipindi mashabiki wa CCM walikuwa wakisema Dr. Slaa hana sera yeye kazi kusema ufisadi tu. Ni vema sasa tunapata kujua ubaya wa ufisadi, tusishughulike na Richmond tu - twende EPA na Escrow na nyingine ambazo wahusika wake wapo, tena bado ni wanachama wa CCM.
 
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

CCJ imefufuka? Hao wote walishapoteza sifa mbele ya umma
 
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa, tumeshona dalili maana tokea jana kuna vijibarua vimeanza kuzuka mitandaoni ya kumuhisisha mgombea pendwa na watu, hata Pasco anajua hili.

Haya yetu macho na masikio...

Binafsi Nampenda Pasco kwa sifa moja aliyonayo, ni kama vile Ngombe aliye wekewa Shemere ya puwa upande ana buruzwa ndio huko huko
 
Uliowataja Kama Dawa, Wanatumika Kuongeza Nguvu Za Kiume Tu Kwingine Hawafai
 
waliosema lowasa mchafu ndo wamsafisho hope walikua ni ukawa ndo kaz kwao sasa
 
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.

Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.

Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Walikua wapi mh.El akiwa ccm?kampeni zenyewe mtuhudhiria ww na hao uliowataja waTz tunataka kupiga kura tu hatutaki mboyoyo!
 
Back
Top Bottom