Dawa ya kutibu UKIMWI

Dawa ya kutibu UKIMWI

Nimetafakari sana kisha nikajiuliza, inakuwaje leo hii Teknolojia imekua sana kuliko hata miaka hiyo ulipogunduliwa UKIMWI lakini bado dawa ya kutibu kabisa UKIMWI haijapatikana?
Naomba mchango wenu wa fikra.
Hakuna mtu anaweza kuua virus.Tofautisha virusi na wadudu wengine.

Ndio maana virus ni tatizo duniani.Ila kwa sasa wanaweza kuzibitiwa tu ila kuondolewa kwenye mwili ukishapata ni ngumu
 
NI sababu tuu kiswahili hakina misamiati ya kutosha.
Yes mkuu, kuuita UKIMWI " upungufu wa kinga mwilini" hauuelezei vya kutosha ugonjwa. Upungufu wa kinga mwilini unasababishwa na vitu vingi mfano lishe mbovu, magonjwa kama kisukari,msongo wa mawazo etc. Upungufu wa kinga mwilini unaoletwa na virusi vya UKIMWI wenyewe ni wa tofauti kwa sababu unatokana na kushambuliwa kwa seli maalum nyeupe za damu ( T- helper cells) . Kutokana na kuuita UKIMWI upungufu wa kinga mwilini, madaktari uchwara wakajipatia point, utasikia mtu anasema fanya vitu vinavyopandisha kinga kama kula vizuri,kupumzika,kufanya mazoezi wakati hivyo vyote haviwezi kurudisha zile T helper cells zilizoshambuliwa.
 
Hakuna mtu anaweza kuua virus.Tofautisha virusi na wadudu wengine.

Ndio maana virus ni tatizo duniani.Ila kwa sasa wanaweza kuzibitiwa tu ila kuondolewa kwenye mwili ukishapata ni ngumu
Yes mkuu, virus ni viumbe wa ajabu,uzima wake unategemea seli za binadamu. Ili umuue inabidi uue na seli za binadamu. Hata mafua huwa ni mwili unajiponya wenyewe( correct me if I am wrong here) na sio zile dawa tunazokunywa.
 
Kuna daktari mmarekani anaitwa Dr,. Sebi inasemekana aligundua natural remedies za kuondoa magonjwa mengi ikiwemo diabetes, ukimwi hadi aina kadhaa za cancer. Hiyo ilikuwa in the 90's

Mwaka 1993, alishtakiwa New York na kuamrishwa asidai kuponya magonjwa.

What does this tell us about power and control?
Dr Sebi wasnt an american
 
Kuna homa ya Ini
Hatari kuliko ngwengwe.


Samia anaongoza wapiga kavu wengi
Na watu hawajali. Ila mi nashangaaga sana nikisikia mtu anafanya ngono nzembe karne hii, tena sasahivi ndo magonjwa ya ngono yamezidi kwa tabia ya watu kujipima HIV basi majibu yakija negative wanapiga kavu. Wakati kama mtu kapata HIV karibuni kile kipimo hakioneshi. Hapo bado kuna Gono,na kuna Mzee wa kazi anaitwa Syphilis ukiumwa hadi uso na mikono vinatangaza ugonjwa wako na matibabu yake ni mateso. Ila watu hawajali wala hawaogopi.
 
Back
Top Bottom