Dawa ya kuondoa/kupunguza ndevu

Dawa ya kuondoa/kupunguza ndevu

Mashine za kunyolea au vwembe ndo dawa Mujarabu...
 
Zuia zisiote uone madhara yake, zitaota kuelekea kinywani.
 
Kwanini hutaki ndevu zako???Siunyoe tu??Na kama unaona uvivu kunyoa mwenyewe ni kiasi tu cha kwenda saluni!
 
Naamini mtoa mada hajapata msaada wowote, hakuna madaktari humu?
Najaribu pia kufikiria kwamba mtoa mada hajaifafanua vya kutosha ili kujenga miongoni mwa wachangiaji haja ya yeye kuziona ndevu kama mzigo mzito.

Kuna watu ambao sio kwamba hawapendi ndevu, bali tatizo ni kwamba ndevu hizo kwao ni tatizo na kero kubwa sana kiasi cha kumnyima mtu raha. Mfano ni pale ambapo mtu akinyoa iwe kwa wembe, magic au kwa kutumia after shave yoyote haimsaidii bado anakuwa kwenye matatizo ya kuwashwa sana na ndevu/kidevu.

Hivyo najaribu kufikiria muamsha mada hii ni miongoni mwa hao wanaopatwa na usumbufu huu. Ila kwa majibu ya wachangiaji walio wengi siamini kama atakuwa amefaidika na chochote, ingekuwa vyema wataalamu wa ngozi na magonjwa ya ngozi wangeweza kuwa msaada mkubwa katika mada hii kwani ni ya kitaalamu zaidi kuliko kuwa ya bora nimechangia.
 
Ni vizuri wachangiaji mada, hoja ktk JF tukawa na nidhamu wakati wa kuchangia. Mtu anapotoa shida, hoja au mada unakuta ana shida ya kweli, hivyo kwa kuwa humu kuna watu wengi kutoka sehemu mbalimbali, wenye taaluma mbalimbali na ambao wanaishi na jamii inayowazunguka ni dhahiri kuwa inawezekana jambo lillilotolewa humu akawepo mmoja wetu anayejua suluhisho la tatizo hata kama aliwahi kusoma sehemu, kuona au ndugu yake aliwahi kukwamuliwa katika tatizo kama hilo. Sasa utakuta wachangiaji wengi wanatoa michango yao kwa mizaha na kejeli. Siyo lengo au maana iliyokusudiwa humu ndani. Tuisaidie jamii ndugu zanguni.......
 
Haaaahaaaaahaaahaaaha, yani ushauri mwingine humu ndani kama nguvu za giza.
 
Binafsi nina devu nyingi sana na nikinyoa mchana, zinaota usiku, tena kwa fujo. Vipele ndo usiseme. Natamani kabisa kutokuwa na ndevu. Ni kero sana!
Mwenye kujua suluhisho, atusaidie tafadhali!
 
Haaaahaaaaahaaahaaaha, yani ushauri mwingine humu ndani kama nguvu za giza.
Tatizo jukwaa limegeuzwa kuwa la utani......watu wana matatizo ya kiafya na wanaomba msaada, badala ya kuwasaidia tunaanza masihara!
 
Back
Top Bottom