Dawa ya kuondoa chelewa (hangover)

Dawa ya kuondoa chelewa (hangover)

Mimi nasikitika kukupoteza mchungaji wa kondoo; itabidi kondoo tujichunge wenyewe
 
<br />
<br />
Sigmaaaaa acha uchokozi bana

Ulianza mwenyewe kumzodoa mtumishi wa mungu. Hasa baada ya Merciless Messi kumsahaulisha nafasi yake ya kiroho kwa jamii we unamkurupusha.
 
Wapwaz

Msaada wa kuondoa hangover! Jana baada ya kuona uchawi wa Genius Messi, nimejitunga kilaji na jamaa Mpaka asubuhi. Nipo Kama mgonjwa supu haipandi natamani kuendelea na unywaji. Dawa nifanyaje?

...ongeza 'ugimbi,' ...itazimua!
 
Kuna comments hapa nacheka sana! Maziwa ya na supu ya Samaki vimeniokoa
 
Kama dawa ya moto ni moto hii concept iwe applied hadi kwenye mengine...dawa hapa ni kuongeza kilaji na kuachana na Man U...kwanini upate presha kila mara wakati alternative ipo? Ndugu wanaachana kwanini isiwezekane kwa timu?
 
Kuna comments hapa nacheka sana! Maziwa ya na supu ya Samaki vimeniokoa
Umeona ee, ushagundua sasa siku ingine unawahi asubuhi unachukua samaki sato, anakatwa vipande vitatu, vitunguu vitatu, hoho moja, karrot moja, ndimu mbili au limao, ngogwe mbili na viazi viwili mafuta kizibo cha chupa ya kili water,ukiweka maji hapo kama lita moja na nusu mpaka kuiva kama dk 20 hv, weweeeeeeee!!!!!!!! pobe yote inakutoka baada ya hapo unapata bia zako mbili tu unarudi kwenye chati
 
Hawa wachungaji wa dot com watata kweli!!
Kula ndizi mbivu kisha kunywa maji kwa wingi Baba Mchungaji..
 
Wapwaz

Msaada wa kuondoa hangover! Jana baada ya kuona uchawi wa Genius Messi, nimejitunga kilaji na jamaa Mpaka asubuhi. Nipo Kama mgonjwa supu haipandi natamani kuendelea na unywaji. Dawa nifanyaje?
Mambo masa,nashangaa mzoefu wa kilaji wa long time kama wewe kusumbuliwa na hangover,kuna hatua kadhaa za kuchukua kuondokana na tatizo hili na itakuwa unaisikia kwa watu tu. 1.kula ushibe kabla ya kunywa, 2.pata glasi ya maziwa nusu saa kabla ya kuanza kunywa pombe hii hupunguza athari za pombe, 3.usichanganye vinywaji, 4.ukiwa unakunywa usisahau maji kila baada ya chupa 2, 5.ukimaliza kunywa kabla hujapumzika pata ndizi mbili mbivu na dawa ya kichwa, 6.kama ulikunywa kupita kiasi multivitamin/minerals pia husaidia(kabla ya kulala), 7.upate usingizi usiopungua masaa 6, 8.ukiamka kunywa maji ya uvuguvugu glass 2 na upate aidha supu au breakfast inayojumuisha angalau mayai 2.
 
Wapwaz

Msaada wa kuondoa hangover! Jana baada ya kuona uchawi wa Genius Messi, nimejitunga kilaji na jamaa Mpaka asubuhi. Nipo Kama mgonjwa supu haipandi natamani kuendelea na unywaji. Dawa nifanyaje?

kapige KIMPUMU ukimalizia na MAHELA.....hapo haina hangover wala hangstart...
 
Wapwaz

Msaada wa kuondoa hangover! Jana baada ya kuona uchawi wa Genius Messi, nimejitunga kilaji na jamaa Mpaka asubuhi. Nipo Kama mgonjwa supu haipandi natamani kuendelea na unywaji. Dawa nifanyaje?

Hahahahah lol! Pole sana usirudie siku nyngine kujitunga kilaji kiasi hicho hahahah lol!. Kuna supu ya utumbo wa mbuzi iliyotiwa limau nyingi na pilipili mbuzi (kama ni mtumiaji) kama una ubavu wa kuweza kupita huku karibu sana labda itakusaidia katika kurudia hali ya kawaida. Messi na wale BARCA kiboko jana nimewavulia kofia, sijui kwa nini katika mechi zao na Real Madrid waliamua kucheza mieleka na sio kandanda safi kama waliyotuonyesha jana.
 
Umeona ee, ushagundua sasa siku ingine unawahi asubuhi unachukua samaki sato, anakatwa vipande vitatu, vitunguu vitatu, hoho moja, karrot moja, ndimu mbili au limao, ngogwe mbili na viazi viwili mafuta kizibo cha chupa ya kili water,ukiweka maji hapo kama lita moja na nusu mpaka kuiva kama dk 20 hv, weweeeeeeee!!!!!!!! pobe yote inakutoka baada ya hapo unapata bia zako mbili tu unarudi kwenye chati

Hujawahi niangusha ila Leo nimepata supu ya Kamongo! Na vyote ulotaja
 
Hahahahah lol! Pole sana usirudie siku nyngine kujitunga kilaji kiasi hicho hahahah lol!. Kuna supu ya utumbo wa mbuzi iliyotiwa limau nyingi na pilipili mbuzi (kama ni mtumiaji) kama una ubavu wa kuweza kupita huku karibu sana labda itakusaidia katika kurudia hali ya kawaida. Messi na wale BARCA kiboko jana nimewavulia kofia, sijui kwa nini katika mechi zao na Real Madrid waliamua kucheza mieleka na sio kandanda safi kama waliyotuonyesha jana.

Unakumbuka ile thread ya Ms Juddy....nilimaliza Kila kitu......Man U jana walikuwa Kama West Ham Utd
 
Wakuu naomba msaada wenu kuhusiana na hili tatizo la mtu kunywa sana halafu asubuhi ukaamka na mnin'gio wa ziada (HangOver), je ukienda hospitali watakupa dawa gani? kwakua ukiwa kwenye ile hali unakua kama unataka kufakufa! asanteni sana kwa ushauri wenu kupata tiba yake.
A-man-with-a-hangover-001.jpg
 
Ukiamka nazo unazimua kwa kuendelea kunywa hadi utaanza kuona kijasho chembamba hapo unastop. Halafu unakula vizuri, then life goes on. Usinywe dawa sijui tylenol ama hedex etc utaharibu ini lako buree. Dawa ya moto ni moto. Mimi hiyo ndio inanisaidia.
 
niliwahi kusikia kuwa, unapaka asali ya kutosha kwenye kipande cha mkate unakunywa na chai ya rangi.
 
Back
Top Bottom