Dawa ya fungus za miguuni

Dawa ya fungus za miguuni

Hizo njia zote ukizoshauriwa hazitaweza kukusaidia kama hautoweza kubadilisha kula vyakula vyenye acids na kula vyakula vyenye alkaline. Tatizo lako sio la nje, ni la ndani kwenye damu\ cells. Ukianza kula vizuri utapona kabisa tena bila kugusa dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuvaa viatu

Vaa sandals au open shoes
Kama ni mfanyakazi andika batua ya hilo ombi

Au nenda kwa dr mwaka
 
Kuna dawa ya fungus ipo kama sprit namaanisha kuwa inakaa kwenye chupa, kimiminika ina rangi, ni dawa nzuri Sana inatoa matokeo mazuri kwa muda mfupi, imenisaidia Sana wakati naumwa fungus niliwapata kwenye guest.
 
Kuna ushauri umepewa huko juu kwanza ni kuwaona madaktari wa ngozi.

Pia uchunguzi wa sukari na HIV

Pia usafi wa mwili na kupakaa mafuta ya mgando baada ya kuoga.

Kila fungus ina dawa kulingana na sehemu ilipo kuwa makini na hilo.

Mfano miguuni tunatumia sana Mycota powder,cream n.k
 




Mara nyingi ngozi ya miguuni hasa katika ngozi ngumu ya nyayo na katikati ya vidole, ndizo zinazopatwa sana na vimelea wa fangasi.

Uwapo wa unyevunyevu, joto na giza huwa ni mazalia mazuri ya fangasi wa miguuni.
Wanaume ambao wako katika hatari ya kupata fangasi za miguuni ni wale wenye dosari ya nyayo ya miguu kuwa na kiasi kikubwa cha tezi zinazotoa jasho nyayoni.

Vilevile wenye kinga dhaifu, wanaugua kisukari, wanaoishi maeneo yenye joto kali na wale wanaovaa viatu muda mwingi. Maambukizi haya yanaweza kuwa chanzo cha kupata fangasi maeneo mengine ikiwamo katika sehemu za siri, viganja vya mikono na mwili mzima.

Uwapo wa fangasi miguuni unaweza pia kumhatarisha mwathirika kuvamiwa na bakteria rafiki wa juu ya ngozi ambao wakipenya kwa ndani ya ngozi huleta madhara.

Vimelea wa fangasi ni mojawapo wa vimelea wanaoweza kusambaa na kumpata mwanadamu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kugusana na vitu vilivyotumiwa na mwenye vimelea wa fangasi.

Katika maisha ya kila siku mara nyingine watu huweza kuvaliana soksi na viatu; hii ni mojawapo ya njia zinazoweza kueneza maambukizi ya fangasi wa miguuni kwa wanaoishi mazingira ya pamoja.

Dalili kubwa ya fangasi ni muwasho unaokulazimisha kujikuna na kujihisi raha au utulivu unapojikuna, harufu nzito ya kuoza katika miguu, kumomonyoka ama kulika kwa ngozi yenye fangasi.

Pia kuvuja kwa majimaji yenye kuteleza na harufu nzito, maumivu au kuhisi kuchomachoma baada ya kuchubuka na pia mara nyingine kuhisi kuwaka moto.

Ugunduzi wa fangasi wa ngozi ya miguu ni rahisi, huhitajiki kwenda maabara, wahudumu wa afya wanaweza kugundua kwa kupata historia ya dalili na kutazama kwa macho.

Mara nyingine unaweza usihitaji kupewa dawa za kukabiliana na fangasi wa miguu, elimu ya afya inaweza kukubadili tabia na ukadhibiti fangasi wa ngozi ya miguuni bila dawa.

Njia ya kukabili fangasi
Moja ya njia rahisi za kukabiliana na kujikinga na fangasi ni kubadili mienendo ya kimaisha ikiwamo kupenda kuwa msafi wa kimwili pamoja na kufua nguo zinazovaliwa ikiwamo soksi ambazo wengine huzivaa kwa muda mrefu bila kuzifua. Tumia soksi zenye asilimia nyingi ya pamba ili kuweza kunyonya jasho la miguuni, kutumia kitambaa safi au taulo dogo kwa ajili ya kukaushia maji baada ya kuoga au unapotoka kazini, matembezini na mchezoni.

Mara tu baada ya kutoka katika shughuli zako vua viatu vya kufunika na tumia viatu vya wazi, kausha kwa kitambaa kikavu maeneo ya miguuni katika upenyo wa vidoleni.

Matibabu ya dawa za fangasi za kupaka zilizo katika mtindo wa poda zinaweza kutumika kutibu, kwa fangasi sugu, dawa za kumeza zinaweza kutolewa. Kama kukiwa na maambukizi mchanganyiko na bakteria dawa za antibiotic zinaweza kutolewa.

Mara nyingine fangasi zinaweza kupata nyufa za vidoleni zikatengeneza vidonda ambavyo vinaweza kupata maambukizi wa bakteria ikiwamo wale wa tetenasi.

Hakikisha pia ukiwa una tatizo hili kiasi cha kufikia kupata vidonda miguuni, hakikisha unapata chanjo ya tetenasi kama hukuwahi kuchomwa.

Fangasi za miguuni ni ugonjwa kama magonjwa mengine, hivyo wanaogua wasipuuze wakidhani ni tatizo dogo.

Wanaogua tatizo wafike katika huduma za afya mapema kwa ajili ya ushauri na matibabu


Muungwana
 
Nasumbuliwa na fungus kwa Muda mrefu sana huwa navumilia na kwenda nao kibishi. Kwa sasa Hawa fungus wananisababishia vidonda kwa juu ya mguu na vikipona vinahama sehemu nyingine.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati.
 
Katika majibu yake asisahau pia fungus sugu za katikati ya mapaja na korodani
 
Binafsi ninakushauri hivi:
Chukua vitunguu swaumu(garlic) punje kadhaa saga au twanga ,bandika sahemu iliyoathilika .
Baada ya siku moja iondoe safisha kwa maji.
Baada ya siku mbili tuletee mrejesho hapa.
 
Nasumbuliwa na fungus kwa Muda mrefu sana huwa navumilia na kwenda nao kibishi. Kwa sasa Hawa fungus wananisababishia vidonda kwa juu ya mguu na vikipona vinahama sehemu nyingine.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati.
Fungus za miguu ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine wa ngozi hivyo bhasi wala usikose furaha maana kwa dawa hizi hapa chini na imani zitaweza kukutatulia tatizo lako la fungus....

Chaguo la kwanza:

Tumia whitefield lotion kwa muda wa week nne (paka asubuhi na jioni) Hakikisha umeoga na kukausha miguu yako vyema kabla ya kupaka

Chaguo la pili:

Tumia Miconazole cream 2% au Tolnaftate 1% Hii pia unapaka baada ya kuoga OR

Clotrimazole cream 1% powder kwa muda wa wiki nne pia na tatizo lako litakuwa limetatuliwa.

Hizo dawa zikishindwa kutatua tatizo lako then last option naomba utumie dawa za kumeza na dawa yenyewe ni Griseofulvin kwa muda wa wiki6 mfululizo

* kwa wakubwa 500mg kidonge kimoja kwa siku pia

*kwa watoto 10mg kidonge kimoja kwa siku pia

Mwisho:
• kumbuka kubadili viatu na socks mara kwa mara hapa namaanisha ya kwamba jitahidi kuwa na socks na viatu zaidi ya pair moja

•Vaa socks nzito

•kila baada ya kuoga jaribu kukausha miguu yako hasa vidole vyako vizuri kabisa....
 
Back
Top Bottom