Dawa ya fungus za miguuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya fungus za miguuni

Discussion in 'JF Doctor' started by MlongaHilo, Jan 14, 2011.

 1. MlongaHilo

  MlongaHilo Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Wapendwa,

  Kwa muda mrefu nasumbuliwa na fungus za vidole vya miguuni (hasa kile cha pembeni kwa kila mguu). Hali hii imenifanya nishindwe hata kuvaa viatu kwa raha.

  kama kuna anayejua dawa ya kunisaidia, tafadhali naomba anielekeze.

  NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA AWALI
   
 2. L

  Lady JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ukitoka kuoga futa maji miguuni vizuri mpaka kwenye vidole, usivae soksi zaidi ya mara moja.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  1) Suguwa ndimu kwenye miguu sehemu zilioathirika na nzima za karibu yake, hii ni kutwa mara tatu.

  2) Viatu vyote ulivyotumia wakati una hii fungus, usivivae, visugulie ndimu, ndani ya viatu, vianike juani kwa muda mrefu, siku mbili mpaka tatu, kabla hujaanza kuvitumia tena.
   
 4. M

  Mzaa chema Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Paka dawa ya mswaki aina ya colgate. sina uhakika wa siku ngapi inategemea umeathirika kiasi gani, lakini baada ya siku tatu utaona effect. fungus zitaanza kukauka.
  otherwise nenda kwenye pharmasy kubwa wataweza kukusaidia dawa ya kupaka au na vidonge.
   
 5. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  tumia mycota powder kila unapovaa viatu, hii dawa inauzwa TSH 10,000 hadi 15,000. unanyunyizia kwenye miguu pamoja na sox
   
 6. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kuna wakati mwingine vidole vinaweza vikawa vimelika mpaka nyama ya ndani, halafu ikafuatiwa na bacterial infection. Kama ni hivyo, nyunyizia dettol kwenye maji safi, weka chumvi kwa kukadiria tu kuwa chumvi itakuwa kali kama ungeonja. Tumbukiza miguu yako ndani ya maji hayo kaa, kama dk 10 hivi. Ukishatoa, hakikisha unakausha hiyo sehemu kwa pamba safi, halafu paka dawa ambayo ina antibacterial and antifungal activity. Fanya hivyo mara mbili kwa siku, ndani ya wiki utaanza kufurahi. Socks pamoja na viatu ulivyowahi kutumia ukiwa unaumwa, vioshe na dettol, anika kwa muda mrefu juani.

  Hata hivyo ni vizuri ukaenda hospitali ukakutane na wataalamu. Ukiwakosa au ukipewa dawa bila kuchunguzwa vizuri, ndio ufuate hili desa la hapa.
   
 7. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi hii powder bado hipo?Ha ha ha ha...kitambo sana!
   
 8. Willy

  Willy Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 78
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Fungus hupenda unyevunyevu sana, ndiyo maana fungus vipo zaidi kwenye sehemu za joto ukienda sehemu za badiri kama Mbeya huwa hamna fungus ukilinganisha va pwani. Ushauri wa kitaalamu (mimi ni daktari) ni huu.
  Hakikisha usafi unazingatiwa, jaribu sana kuwa na wakati ambao unakaa with open shoes. Tumia dawa ya fungus, hasa ile ya powder kama mycota kwa kipindi kirefu 6-8 weeks. Matibabu ya fungus huchukua muda mrefu, na hakikisha kwamba kuna ukavu katikati ya vidole. Soksi zako zibadilishwwe kila baada ya siku chache. Achana na huu ushauri uliotelewa kama kutumia dawa ya mswaki au vingine mabyo nimeviona hapo juu. havisaiidi.
   
 9. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  tafuta mycota (treatement for athletes' foot) iliyo kwene hali kama ya dawa ya mswaki, [inauzwa sh 4500/5000]
  tumia baada ya kuoga/kunawa miguu na kuikausha (kwa tissue sio taulo kuepusha kusambaza maambukizi) kila asubuhi na jioni kabla ya kulala,
  paka katikati ya vidole vilivyoathirika alafu uhakikishe miguu haipati unyevu kabisa,
  na kama unavaa soksi usivae soksi ambazo sio safi...
  kama baada ya kutumia dawa kwa wiki mbili hujapona,unahitaji maombi.
  nilikuwa na tatizo kama lako.
   
 10. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  TUMIA SABUNI YA MWAROBAINI
  Hii mie imenitibu, ni hivi, kila jioni ukishaoga paka povu la sabuni ya mwarobaini then iache ikauke. Asubuhi pia fanya hivyo hivyo.
   
 11. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Doctor Willy,
  Kama ni Doctor wa ukweli nafikiri ungemshauri huyo mtu aende hospitali.
  Kitu kimoja nafikiri unafahamu Doctors wanaweza ku-differ opinion on the same issue. Mimi naamini kuwa ushauri uliotolewa na watu wengine hapo juu ni kutokana na experience yao (pamoja na yangu) ambapo tulifuata maelezo tuliyotoa kutokana na tulivyoshauriwa na Madaktari wengine, na tukapona.
  Nafikiri pia unafahamu kuwa fungus zinaweza zikala sana halafu kukawa na secondary infection by bacteria. Huyu mtu amesema ametumia dawa za aina nyingi lakini bado hajapona. Ushauri tunaompa hapa including uliotoa ni wa kumuongezea list ya matibabu na dawa atakayokuwa ametumia kutatua tatizo hilo. Hivyo nafikiri ni vizuri Daktatri aone kwa macho kiwango cha athari za fungus kwa mgonjwa ndipo atoe ushauri muafaka.
   
 12. r

  ral Senior Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mlonga,

  pamoja na michango ya wadau kitu ninachojua kuwa ni effective, kila jioni kwa muda wa siku 5, osha miguu kwa sabuni halafu chukua chombo kama ndoo ndogo, loweka hivyo vidole kwenye WHITE VINEGAR, vinegar nafikiri ni TShs. 1500 chupa ya lita moja, fanya bila kukosa hata siku moja you will come and tell me

   
 13. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Pole sana ndugu yangu. Tafuta asali mbichi ya nyuki wakubwa, nenda kariakoo ununue abdalasi iliyosagwa (powder). Changanya vijiko vikubwa vitatu vya asali na kijiko kimoja cha abdalasini powder, changanya vizuri halafu paka miguuni usiku wakati wa kulala halafu vaa soksi; lala mpaka asubuhi osha vizuri miguu yako endelea na shugulu zako kama kawaida. Fanya hivyo kwa siku tano utakuwa umepona.
   
Loading...