Dawa ya ebola inatibu wagonjwa Marekani tu

Dawa ya ebola inatibu wagonjwa Marekani tu

yani unaakili wewe umehisi sawaaa utakuwa unakula ubuyu unaouza.
 
Wale manesi wawili walioambukizwa ebola wamepona! Wameruhusiwa hospital na wameenda ikulu kuonana na Obama.

Ukumbuke wameumwa sio zaidi ya wiki moja. Na ukumbuke huko nyuma kuna daktari mwingine aliambukizwa alitibiwa akapona. Ila yule mwafrika toka West Afrika aliyelazwa huko Marekani alikufa. Hawa raia wa Marekani wamepona.

Swali:
Kwanini wagonjwa wa ebola wa Marekani wanatibiwa na wanapona, ila wagonjwa wa Afrika wanakufa, tangu nimeanza kusikia huu ugonjwa huko West Africa sijawahi kusikia kuna mgonjwa kapona au Marekani wanayo dawa wanasubiria muda muhafaka waje kuuza kwa bei kubwa watengeneze super normal profit au wapo kwenye majaribio ya ugonjwa waliotengeneza?

Yule mgonjwa muafrika hakuwa na insurance ya kuweza kulipia gharama zake za matibabu. Kumbuka yule sio mmarekani.
 
miss wangu,this is a political propaganda, hawa jamaa hujui tu wanatumia mbinu nyingi sana kuhakikisha kuwa wanaendelea kututawala. hata makundi yote ya uasi yanapewa msaada na haohao kwa ahadi ya kuwa karibu na hao wanyonyaji

Hawa wenzetu wanachukulia huu ugonjwa seriously, hebu angalia hata vile wanavyovaa wakati wa kuhudumia wagonjwa. Angalia na kwetu Afrika huduma hii haiwezekani kutokana na ughali wake na 'ujinga' wetu (wale wa Liberia waliambiwa na wakawatimua mabwana afya kwa mapanga!)

Kuna waafrika wengine wamejitahidi kujihifadhi kwa kutumia mifuko hii ya plastiki na wamefanikiwa kuuguza wagonjwa wao, hebu fuatilia kwenye vyanzo tafauti vya habari.

Sio kila kitu ni siasa.
 
Hawa wenzetu wanachukulia huu ugonjwa seriously, hebu angalia hata vile wanavyovaa wakati wa kuhudumia wagonjwa. Angalia na kwetu Afrika huduma hii haiwezekani kutokana na ughali wake na 'ujinga' wetu (wale wa Liberia waliambiwa na wakawatimua mabwana afya kwa mapanga!)

Kuna waafrika wengine wamejitahidi kujihifadhi kwa kutumia mifuko hii ya plastiki na wamefanikiwa kuuguza wagonjwa wao, hebu fuatilia kwenye vyanzo tafauti vya habari.

Sio kila kitu ni siasa.
wito wako nimeupokea wa kufatilia taarifa.

lakini nataka nikwambie kuwa kiwango changu cha kufatilia taarifa za dunia hii sijui hata kama 1/30 yangu unaifikia.

nina taarifa zote unazonieleza hapa kuhusu ebola na mimi sifanyi siasa.

nachoweza kusema ni kwamba wewe tofauti yako na mimi ni kuijua historia ya dunia hii na namna inavyoendeshwa.

biological weapon ni sehemu ya silaha za kijeshi na ni sehemu ya mbinu nyingi zinazoweza kutumika kui-control nchi inayokusudiwa ama eneo linalokusudiwa. na hawa wamekuwa wakifanya hivyo mara nyingi.

maswali ya kujiuliza ni mengi na majibu hakuna.

kuna mambo mengi sana yanafanyika bila uelewa wetu na hatuelewi kabisa.

majanga duniani hayajaanza leo ni ya karne na karne, ila saizi tumeongeza majanga mengine yanayotokana na maarifa ya hawa wanaoaka kuendelea kunyonya nchi masikini kwa kuleta hofu za kila aina.

putin mwenye hivi majuzi kaeleza kuwa waasi wa IS wanameasisiwa na kufadhiliwa na marekani na marekani imekuwa ikifanya hivyo toka kundi la mujahidin , baadae alqaida nk

lengo ni moja tu la hao jamaa, ni kuleta distablization ili wapate urahisi wa kufanya wanalolitaka hasa wizi wa mali na kutaka kuwa na nguvu za kuendesha nchi zingine kisiasa.

tatizo letu sisi tumekuwa brain washed, lile tukio la watoto wa nigeria kutekwa linaumiza sana, lakini marekani ndiyo iliyoikataza nigeria kufanya mazungumzo na Boko haramu kwa kuwa ni magaidi, ikawaahidi kuwaletea UAV kuwasaka watoto lakini hapo hapo marekani hiyohiyo ikafanya mazungumzo na magaidi iliyokuwa inawashikilia na kuwaachia. hizo UAV zimekaa miezi na miezi na mwisho hao nigeria watoa taarifa ya kufanya mazungumzo na magaidi ili wasichana waachiwe.


hii dunia ukiwa na technology unaweza kupambana na ujinga wote huu wa hawa jamaa.

bado nashawishika na kuamini kuwa this is a political propaganda
 
Huyo Mliberia Duncan alichelewa kutibiwa Ebola. Alienda mara ya kwanza akapewa anti biotics tu na kurudishwa nyumbani.

Ebola ukiiwahi, ukiipiga ma IV na experimental dose za nguvu pamoja na serum inakatika yenyewe.

Kuna watu wana survive Ebola Liberia na Sierra Leone huko bila hata ya huduma nzuri sana, kwa sababu wamewahiwa kupelekwa hospitali na wanarudisha maji yanayopotea kwa kuharisha.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Dr. Mwafrika mwingine afariki marekani kwa ebola..
 
Back
Top Bottom