Dawa ya CHADEMA yapatikana

Dawa ya CHADEMA yapatikana

Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Ni Rahisi kwa Ngamia kupenya katika Tundu la Sindano kuliko CCM kuacha kutumia Vyombo vya Dola kutawala......
 
Hata mimi nikionyeshwa Mafanikio nitaridhika ! Kwi! Kwi! Kwi! Kwi!
 
Kuna maendeleo gani ya kujivunia hawa CCM wanaloweza kuwaonesha watanganyika wenye akili na macho ya kuona-? Hawana jipya kamwe!
 
Mafanikio tunayaona kama kuzalisha ARV fake, ufisadi wa RICHMON,EPA,MEREMETA na kushuka kiwango cha elimu, CCM hoyeee!
 
Watuonyeshe pia namna mnavyoharibu na kugawana rasirimali zetu.
 
Hivi watu hata kama kusoma hawajui kusoma, ina maana hawewezi kuona shule zenye walimu, watoto wao wakiwa shuleni wamekaa kwenye madawati, vitabu mshuleni kama vipo, hospitali ambazo ukifika tu unapimwa na kupatiwa dawa kulingana na ugonjwa wako, umeme hadi vijijini, Wagonjwa hospitalini kila mmoja anlala kwenye kitanda chake tena anahudumiwa na Nesi mwenye huruma, barabara zenye lami na madaraja mazuri hadi vijiji ambazo sio za mikopo na uhusiano mzuri na wawekezaji hasas kwenye vijiji vinavyozunguka migodi kama kule North Mara.
 
...a dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.
...
Wananchi waonyeshwe maendeleo!
Kama maendeleo yapo watayaona wenyewe.
Hawayaoni kwa sababu hayapo.
Kama hayapo hata ufanyeje hawatayaona.
 
Wanasiasa bongo naona wote vichwani hakuna, kila siku statements za kitoto zinatoka tu, sasa hata huyu em muangalie ati "ni muda wa kuonyesha kwa vitendo ili kushinda wapinzani" mbona maneno yake yanasema wazi kua yuko hapo kushindana na wapinzani na sio kwa akili ya wananchi, bado yanasema kua walikua wamelala hadi sasa wameona wanashindwa ndio wanataka waanze kufanya kazi, na bado yana maana wanataka sasa waonyeshe kwa vitendo since hapo nyuma walikua wanafanya kwa maneno.. Duh sijui raia kama hua zinafikiria speech kabla hazijatamka, huyu nani alimpitisha kwenye uchaguzi huyu? Ndio wasomi tubaochagua hawa? Hahahaha
Mwanza Mayor wa jiji na viongozi wake wooote wamelala kuna barabara moja nikipita na gari posta mpya imebomokabomoka jijini kati huu ni mwaka wa tatu sasa iko vilevile, kile kipande hata milioni 50haifiki maana ni kurekebisha, hadi mtu akifa ndio msela anasubiri afanye kazi.. Afu mnasema tuna wasomi kwenye siasa! Haha wasomi au masela tu wako kulipwa hela na kuonea wananchi... Kila nikifikiria bongo huu uchizi hua nafyonza tu, inakera kinoma nchi zote nlizoishi wako systematic mbaya, siku moja tu kitu kinarekebishwa hata kama ni kikubwa au kidogo kiac gani kina maana kubwa mno,
 
Hii ni ngonjera nyingine kwa wezi hawa na chama chao
 
nani anikumbushe ile orodha ya ahadi za kikwete kisha tuanze kupima kwa haki zipi kaekeleza zipi kachemsha
 
eti kuwaonyesha watanzania mafanikio ya serkali yao ! sasa kama ni maendeleo yanahitaji kuonyweshwa , yaani wananchi wetu ni vipofu wakiwango hicho ?
 
siku umeme kwetu usipo katika....dawa....zikiwapo...shule kama zamani ilboru ilikuwa bora...nguzo za umeme zikiwepo...trafik na police na tkukuru na hakimu na afisa ardhi na naiihi wakiacha kuchukuwa rushwaa aaaa hapo nitajadili
 
Kwa mm hata kama wataonyesha hayo mafanikio kama yapo, ila wamechokwa haijalishi wameleta au hawajaleta. Hulka ya mwanadamu ikifika mahali akachoka hata ufanye zuri gani yeye haoni maana amechoka. Dawa ni kukaa pembeni na kuachia wengine waendelee. Kwani hicho chama kililetwa na Mungu ili kitawale hadi kiama? Si mjifunze kwa Gadafi? Kwani ni mema mangapi alioyafanya? Ilifika mahali walichoka wananchi, haijalishi walisaidiwa na nani ila walichoka wakatafuta kingine hata kama hakiwasaidii. Cc isijidanganye yatosha.
 
Kuna kitu kama kujivua magamba, na mwenyekigoda alituambia anawajua kwa majina wazungu wa unga. Ukafika wakati wezi wa hela ya EPA wakaambiwa wazirudishe kimya kimya, hatujui kama zilirudi au la. Kila siku tutasikia mapya huku maendeleo hatuyaoni.
 
nyie mnaongea hivi mtaandoni mnapiga kura kweli? au ndiyo ule umati unaoyeyuka wakati wa kupiga kura...mimi ningekua mkubwa ndani ya CCM nisingekosa usingizi na hawa wanaharakati wachanga wa kisiasa na kaNGO kao aka CDM..ningekosa usingizi na vita ya ndani kwa ndani ya Urais inayoweza kumega chama ndani ya vipande viwili au kupeleka viongozi wangu kwenye haka KanNGo na kufufua hivi vyama vingine mfu....

CDM bado sana kupewa JMT,,wananchi hawawezi fanya kosa hilo kuwapa nchi wanaharakati wasio na uzoefu wowote wa uongozi taifa lenye changamoto kwa watu watakaokuja kuunga unga kazi na kujaribu jaribu ndani ya karne hii ya 21...wakomae ndani ya kamati za bunge, wakae bungeni miaka mingi na wakusanye zaidi proffessionals na viongozi wenye uzoefu toka vyama vingine labda 2025 au 2030, 2035 watapewa nchi kama watasurvive 2015 na beyond.
 
Huyo Mjumbe atakuwa anamatatizo makubwa, na kama hoja yake imekubaliwa basi ccm itakuwa ina matatizo makubwa tofauti na tunavyofikiria.

sisi tumekuwa wageni hadi aje mtu kutuonyesha mafanikio ya ccm?
 
Huyo mjumbe aliyetoa huo ushauri atakuwa haishi Tanzania, kwa hiyo hajui hali halisi ya umaskini Tanzania na haijui CCM vizuri.

Mafaniko mafanikio utawaoneshaje? Wananchi wakienda hospitali wanakuta hakuna dawa, mazingira machafu ya hospitali, vitendea kazi havipo, wataalamu wachache, wengine hawakidhi vigezo, hapo utaonesha mafanikio yapi? Ukija upande wa elimu, watoto wanakaa sakafuni, wengine wanasomea chini ya mti, watoto wasiojua kusoma na kuandaika hujiunga na elimu ya sekondari, matokeo mabovu ya kidato cha nne, upungufu mkubwa wa waalimu, wengine ni wa vodafasta, ukosefu wa vitabu vya kiada na ziada, shule nyingi hazina maabara, mafanikio gani utaonesha hapo?

Ukija kwenye siasa ni dhulma tupu; matumizi ya polisi mwanzo mwisho. Upande wa uchumi ndiyo kabsaaaaa; mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu, umaskini uliotopea vijijini n.k. Huduma za kijamii zikoje? Wananchi hawana maji salama kunywa, elimu duni katika shule za kayumba, magonjwa sugu kutokana na umaskini uliokithiri. Ni vigumu kuonesha mafanikio Tanzania katika mazingira haya.
 
Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

ushindi Kama mlopata huku Arusha mjini juzi ktk kata za elerai,kimandolu, KALOleni na hiyo kata nyingine ee! Ccm bana.
 
CCM wana mengi ya kuonyesha wananchi ila sio mafanikio bali ni umaskini,kama huyo mjumbe alimaanisha hayo basi naungana naye......
 
Back
Top Bottom