Dawa ya CHADEMA yapatikana

Dawa ya CHADEMA yapatikana

hiyo ni dawa ya chadema au dawa ya kuwahi kujimaliza? hivi kwani watanzania hawaoni? au hawayajui mafanikio/ mengine ni matusi ya mchana! haya watuonyeshe tuone hiyo dawaaaaa
 
Hii Forum imejaa watu wanaowaza uasi, hata wazo zuri kwa namna ipi wataingiza vichekesho vyao, sometimes huwa nasoma ili nicheke sio nielimike.
 
Wanasubiri kufa hawana jipya yaani mwinyi aliuza loliondo laana ya wamasai itawatafuna daima.
Shame upon them
 
Tangu lini vuta nikuvute akapost mada yenye akili? Ujinga mtupu
 
Lakuvunda

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

No wonder Milembe ikawa dodoma....na NEC ni Dodoma...

Kuna kuonyesha kwa vitendo na kwa nadharia?Wenye akili hawawezi jadili ....Mwendawazimu akiwaambia mwenzie anataka muonyesha marehemu alivyouwawa kwa vitendo.Wakati hisia za marehemu zinahitaji kutumika kuliko matendo ya muuzaji ili marehmu feel.

Sasa maCCM yote yamenunu ujinga kirahisi sana....Vitendo vipi watakavyofanya vya kumuonyesha mwananchi walichofanya km nadharia yao haikutosha mwambia mwananchi aone, au kumwambia alichokiona kilifanywa na CCM.

Mambo ya jamii huwa hazihitaji mtu kuambia au kufanyiwa matendo ili aone matunda ya kazi fulani,...kwanza anaona, km hayapo upande wake wa kuonda huambiwa aone, asipoona, huku akiwa na macho, asifeel wakati ametumia huduma basi atakuwa na shida ya hisia, huwezi ingiza machoni.......YASIJEKUWA MATENDO YA KULAZISHA WATU WAKUBALI YASEMWAYO NA CCM NA SI WALIYOPASWA TENDA.
 
na maendeleo ynyewe yaendane na muda waliokaa madarakani...mfano maendeleo ya elimu baada ya miaka 50, udhibiti wa ujangili na madawa ya kulevya baada ya miaka 50 ya utawala wao.
 
Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Ndo mjue kwamba kweli kichaa kashika usukani kwenye scramble road. Yaani hilo wanaligundua leo!?? Najua wanajua hakuna cha kuwaonesha wananchi na ndio maana wanatumia mbinu MBADILIKO ...
 
Kama wameamua hivyo kwanini waliwakamata Viongoz wa chadema juzi????? ccm hawana cha kujitambia ukilinganisha kwa miaka 50 waliokuwa madarakani.

m4c
 
Alaaa!! kumbe CCM wanakiri kutumia vyombo vya dola dhidi ya wapinzani. OK
Halafu wakati wa kuonyesha mafanikio msisahau muhimbili na hospitali zingine.

Mkionyesha mafanikio msisahau taarifa ya CAG ya wizi na hizi za kamati za bunge.
Msisahau madawa ya kulevya yalioshamiri wakati wa utawala wenu, ni sehemu ya mafanikio
Nawakumbusha meno ya tembo yanavyomaliza rasilimali etu
Pia ongezeko la vitendo vya mauaji, tindikali na 'kuvamiwa' kwa akina Uli na Kibanda.
Kuna kufeli kwa wanafunzi na matokeo kupangwa na kamati kuu ya CCM, hilo nalo ni sehemu ya mafanikio

Ili muweze kuonyesha mafanikio zaidi ningeshauri mueleze mulivyomaliza Deep Green, Meremeta,EPA na Richmond kwasababu tunakiu ya kusikia matokeo ambayo siku hizi mnaita big results.
 
Dah?
Bahati mbaya zaidi ni kwamba hayo maendeleo wanaotaka kutuonyesha yalipaswa yawepo tangu 1990 huko.
 
Mafanikio huwa yanaoneshwa au yanaonekana?!
Wanataka kutuonesha barabara siyo?
Sisi tunajiandaa kuona elimu bora ya wanetu, mishahara ikituna kwenye mifuko yetu, chakula kikijaa majumbani mwetu, Vyombo vya dola vikiacha unyanyasaji, mafisadi wakichukuliwa hatua!
Haya na mengine inabidi tuyaone, kutaka kutuonesha ni kuficha wasichotaka tukione....!
 
Ha ha ha ha ha ha .......... Sisi hatuna chuki binafsi na ccm ..... Tunataka vitu .... Ila hawawezi .... Hata umpe panya chakula haoacha kukuibia .... Ukoo wa panya ni hatari eti .... Wewe unafikiri huo ukweli hawaujui? Issue ni kwamba ni ngumu kuutekeleza ....
 
Big results kwa Trillion 22!!!?? Maprofesa wengine vituko tupu! Big results inapimwa kwa kitu mfu au kwa kitu hai!! sijawahi ona hii iko TZ tu!! Life cycle ya TAnesco iko mfu halafu unakuja na BIG results??!!
 
Hivi vile vipindi vya kutangaza mafanikio ya serikali ya ccm viliishia wapi!
 
Hata sasa chadema hawana la kusema ila wanaropoka tu mambo ambayo hata msingi hayana.
 
Back
Top Bottom