Dawa ya CHADEMA yapatikana

Dawa ya CHADEMA yapatikana

Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kama kuonesha ni dili nenda Mtwara. Barabara zote zinajengwa lakini wanchi wana hasira na CCM na Serikali yake usipime.
 
Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo
Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

We tupatupa kichaa nini? Tatizo nyinyiemu akili hamna kabisa, miaka hamsini cha kuonesha hamna, ugomvi sio kidogo tulichonacho ugomvi ni huo ukoo wa panya!
 
Wazo zuri sana, umeme wa uhakika na bei nafuu, maji ya uhakika na bei nafuu, gesi bei chini kwa domestic use, gas ya magari bei iwe chini.....haya yakifanywa mie roho kwatuuuu
Haya yakiboreshwa kutakuwa na nafuu kubwa sana kwenye mifuko ya familia, mtu mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla wake hivyo akiba itakayopatikana baad ya matumizi ya bei nafuu/rahisi itaboreshe makundi hayo katika elimu na afya lakini.....

Serikali iboreshe huduma ya afya iboreshwe kwa asilimia 99% (maana yake iliyopo inaridhisha kwa asilimia 1)
Then Elimu iangaliwe kwa mapana

Na hayo yakifanyika, wawekezaji wandani wataongeza mitaji, familia za kati zitakuwa nyingi, jamii itakuwa bora, uhalifu utaenda chini, amani itakuwa tele....Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
 
ebu nionyesheni mimi hata kimoja tu ambacho mtaweza kumdanganyia wanakijiji kule mtera,etc nao wakakubali!!
 
Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam


Hawa watu bana!

Tangu hapo wananchi wa nchi hii walichokuwa wanalilia ni ustawi wao na unafuu wa maisha! Kwani nini jipya hapo? Wananchi wanaomba nini kila siku? Ni yaleyale ya tangu miaka ya 60....Maji, matibabu, barabara, umeme na uthibiti wa bei!

Na tatizo limekuwa ni lipi? Lilelile....Serikali na chama fisadi. Mapato ya taifa kwa asilimia kubwa yanapotelea kwenye mifuko ya watendaji wa serikali binafsi, rushwa imekithiri kila kona , haki imepotea na uhuru unatoweka kwa kasi ya kutatanisha!

Sasa tuongelee kuonyesha mafanikio kwa vitendo!...

Kwamba CCM itaonyesha jinsi ilivyofaulu kuwaibia wananchi kwa kuongeza kodi na bei za mafuta, hivyo kuwasababishia ongezeko kubwa la gharama za maisha??!

au CCm ionyeshe wananchi jinsi inavyochukulia mzaha suala la maendeleo vijijini kiasi kwamba pembejeo hakuna, na zikipatikana zinakuwa kwa uchache na kwa kuchelewa...masoko hakuna na inafikia sehemu hata mazao hayana bei elekezi. Mafanikio yanaextend mpaka mpaka kwenye kuwazuia wananchi wasiuze mazao nje ya nchi ambako kuna maslahi kwao! Yaani masoko ya ndani ovyo bei kila mlanguzi awanyonye anavyojua na nje ya nchi Msiuze. Sawa na kusema wakulima ni haki yao kuwa maskini!

au CCM ionyeshe mafanikio ya kushindwa kusimamia rasilimali zetu mpaka wanyama wanatoroshwa nje ya nchi kupitia viwanja vya ndege vyenye ulinzi masaa yote...au mafanikio katika kuwapa misamaha ya kodi wawekezaji kwenye sekta za madini na utalii hii ikiendana na kuwaachia wamiliki wa makampuni hayo na mahoteli kubadilisha majina kila muda wa kulipa kodi unapofika, sawa na kusema CCM na serikali yake inazidi kufanikiwa katika kupokea rushwa!

au CCM na serikali iwaonyeshe wananchi jinsi ilivyoweza kuwabaini mafisadi, kutangaza vua gamba na hatimaye kufeli jumla katika hilo? kimevuliwa kipi ? mikwara yote nani kashughulikiwa? So mniwie radhi ntakaposema ni sera isiyo rasmi ndani ya CCm kuwalinda wahalifu na wahujumu uchumi nchini!

au labda CCM ionyeshe mafanikio ya serikali yake katika kujiteulia Makandarasi wa kujenga barabara ambazo zimetokea kuwa chini ya kiwango mpaka kufikia kutomaliza mwaka mmoja kabla hazijayeyuka na kubanduka na kisha kuwalipa kwa gharama za juu,..gharama zinazohusisha ukaguzi wa barabara zenyewe......Mafanikio?

au CCM na serikali yake ionyeshe mafanikio ya kutumia Vyombo vya dola kwa maslahi ya kisiasa kuwatishia wapinzani na kuwadhuru wanaoipinga? ni mafanikio ya kuacha watu wafundishwe namna ya kudhuru wenzao kwa mapanga, visu na tindi kali eti kwa sababu tu ni wapinzani au wanaoikosoa serikali? ...au kuwaua waandishi na kuwang'oa kucha na meno huku polisi wakilazimisha kujichunguza ili kupindisha haki na ukweli?

CCM na serikali vionyeshe nini kwa watanzania? Jinsi kulivyopatikana mendeleo ya kutisha kwenye sekta ya elimu huku wanaofeli ni sawa na wanaofaulu( kwamba ukifelei umefaulu na ukifaulu umefaulu)? kwamba ukifanya mtihani na usipofanya unafaulu tuu hata kama umeshindwa kuandika hata jina lako??! ..kwamba kuna shule kibao za kata,walimu, madawati na maabara hakuna? jinsi rushwa hasa za ngono zinavyoamua viwango vya ufaulu wa vyuo vikuu huku wahadhiri wake na wasaidizi wao wakiachiwa uhuru wakusema nani kafaulu na nani kafeli bila kujali ufaulu umepatikanaje?

Ni hivi, CCM haina sauti ya kuonyesha wala kusemea chochote ambacho kitaitwa mafanikio ndani ya nchi. Labda kitu pekee ambacho CCM inawezafanya ni kuwa wakweli kwa wananchi wa Tanzania....Kuwa imewadanganya kwa muda mrefu, imewasababishia adha na madhila kwa muda mrefu na imeshindwa kuongoza, hivyo inaomba radhi kwa wananchi wa Tanzania kwa yote hayo na iahidi kutorudia tena, pia iahidi kuachia nchi haraka sana na kwa amani ili wanaoweza waiendeshe mpaka wao watakapojifunza kuwajibishana bila kuangaliana sura, kuwa WAZALENDO NA WAKWELI, ndiyo warudi kuomba ridhaa ya wanachi wa Tanzania tena. Hapo tutakuwa tunaelekea kuelewana kidogo. Vinginevyo mimi naona "ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI NA KASI YA HATARI KUELEKEA KUZIMU YA HAPAHAPA DUNIANI, KAMA CCM HAITAONDOKA MADARAKANI!

Nisamehewe kama kuna asiyenielewa! Mimi naishi uswazi, wazazi wangu na washkaji wengine wako kijijini na nayaona kwa macho!
 
Nina imani sasa hata masheikh wetu wanweza kuwa salama sasa, kama hilo wazo litapita.
Naamini kuwa risasi zitakuwa ni historia.
 
KWA vitendo?????!!!! ha! ha! CCM BWANA SASAHIVI hao wanafukuzana kama paka na a m ***bwa. lazima kijue kuwa MUDA wao haupo tena
 
Mbinu ya Mwigulu (Savimbi) ni sahihi zaidi, ni kuwauwa wapinzani woote, kama Al Asad wa Syria afanyavyo. Tena kupotezea kabisa CDM hao ndo wenye kiherehere.

Kwa mwenye njaa, mafanikio hawezi kuyaona,mafanikio hayataonekana kwa watu ambao shida zimewabana hawana amani tena:
  1. kwa yule akosaye huduma za afya,
  2. watoto na wajukuu zake kufeli mitihani,
  3. wajawazito 4 kulala kitanda kimoja,
  4. wafugaji kukosa malisho na kuvurumshwa popote waendapo;
  5. wakulima kukosa mazao kwa sababu wafugaji wamelisha mashambani mwao;
  6. wakulima wamekosa mapato na masoko ya bidhaa zao, kwa sababu vigogo wa CCM na serikali kupitia makampuni yao feki ya kilimo wamewaumiza kwa kuwauzia pembejeo feki na kulazimisha kuuziwa mazao kwa bei za chini;
  7. familia na koo zikilia kwa vijana wao kubambikizwa kesi na polisi;
  8. wafanyakazi wakila mkong'oto kila wanapodai haki zao
  9. wanafunzi qwa vyuo vikuu kukosa mikopo kwa ajili ya masomo yao;
  10. wazazi masikini wakishuhudia watoto wao wakitupwa nje ya mfumo wa elimu kwa kupewa elimu feki isiyo na mitaala; shule za kina kayumba wakisomav TEHAMA huku hawajawahi kuona kompyuta.
  11. Hawawezi ona mafanikio zaidi ya mafanikio ya ujangiri wa akina kinnaana na vijana wake kutoka alshababu, El, riz na jeshi lao la genge la mazungu ya unga.
  12. wakulima wakiporwa na kupokwa ardhi yao kwa kigezo cha wawekezaji, wao wakibaki mafukara wasio na mtetezi.
Kwa hayo yote, mafanikio ya CCM na serikali yake yako wapi? Au mafanikio ya jeshi kubaka vibinti kwa kuwa wazazi wao wanatetea haki zao.

Hapa ni mbinu za Mwigulu( the great savimbi) ndizo zinazoweza kuwa bora zaidi. JK alishaliona hili mapema, alisema pale idodomya,"Mwigulu ndiye anawaweza wapinzani (CDM)."

Matangazo ya ugaidi ya savimbi wa tz si tu yanaichora vibaya Tanzania mbele za jumuiya ya kimataifa, bali yanahatarisha hata uwepo wa serikali ya JK. Pamoja na hayo hakuna jipya kwa CCM ya JK.
 
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu atakayekuwa tayari kusubiri beyond 2015!
 
Back
Top Bottom