Dawa ni moja tu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ni moja tu!!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mc Kihiga, Apr 13, 2011.

 1. Mc Kihiga

  Mc Kihiga Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mwanafunzi mmoja alikua ni mpemzi sana wa masomo lakini tatizo likawa ni moja tu! Kuna jamaa mmoja alikua amemganda kishenzi kisa mpenzi wake wa long time dada ni mwanafunzi wa Sec school: Alitafuta sana kuachana nae lakini ujanja ukamwishia basi akaamua kumwambia Bibi yake maongezi yalikua hivi:

  SIKUJUA: bibi mimi kuna kijana ananisubua lakini simpendi.

  BIBI: Ulishawahi kustarehe nae au? Bibi aliuliza.

  SIKUJUA: Ndiyo bibi! Ila mara ya mwisho ni mwezi ulio pita.

  BIBI: sawa inatosha sasa ngoja nikusaidie kumuacha.

  SIKUJUA: Ehee!!! Kwa shauku ya kutaka kujua?

  Kesho yake asubuhi sana J.mosi Bibi akatwanga makande kisha akayapika chap chap mara baada ya kuiva kisha akakoroga uji mwepesi sana alafu akachukua kande kidogo na uji mwingi kiasi kisha akaupooza sana na kuuchanganya na kande alikologa kwa muda kabla ya kuweka ktk plastic bag {mfuko wa rambo} akamuita Sikujua baada ya kufika akamueleza kuwa "Sasa twaenda kwa bwana etu unasikia tukikaribia mimi nitachuma fimbo alafu wewe utakunywa huu uji kiasi na mfuko wake utaendelea kushikilia pamoja na huu mchanganyiko wa kande kisha tukifika mimi nitakuchapa bakola tatu huku wewe ukitapikia kwenye mfuko wenye urojo kumbuka ni mchanganyiko wa kande na uji kama tapishi nitakubwaga hapo alafu wewe pia ubwage mfuko nitampa vipande vyake sawa?" Basi bibi akaendesha mchezo mzima bila kikwazo kumbuka Wazazi wa Sikujua hawa juikitu!!! Basi bibi na mjukuu wake wakatinga kwa jamaa alikutwa ameketi kizingitini mwa mlango wake. Bibi bila ajizi akamtia bakola mjukuu wake za kikweli kweli na kisha kumbwaga Sikujua kwa jamaa. Maongezi ya Bibi na Kijana yalikuwa hivi:

  BIBI: Wewe kijana kwanini umeniharibia mwanangu hee?

  MAJALIWA: Nani Mimi wewe Bibi umetumwa nini?

  BIBI: Sawa mimi si nimetumwa wewe baki nae alafu mimi na rudi sasa hivi ili nikuonyeshe nilicho tumwa akambwaga Sikujua miguuni kwake na wewe nisikuone nyumbani kwangu mimi si Mama yako tena!

  SIKUJUA: Mama usiniachee mimi nitaitoa hii mimba yake "Huku akitapikia kwenye fuko la rambo huku akilia kwa kwikwi".

  MAJALIWA: Haya na wewe malaya nani kakupa huo ujinga tumboni mwako haya mfuate huyo mama yako malaya ninyi toka toka.

  SIKUJUA: Sitoki mpaka mama arudi si ameenda hapo kituoni kuita police wee msubiri aje niondoke nae yeye ndio kanileta hapa sitoki utajiju.

  MAJALIWA: Wewe si mwanfunzi wewe ondoka bwana mimi nitapata matatizo Sikujua bwana.

  Mara jamaa kainuka mbio. Mpaka leo hajarudi kwao kweli hii ndiyo dawa!


  Mc!
   
Loading...