Dawa ni kusamehe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ni kusamehe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tabutupu, Nov 5, 2011.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Mpigie simu , mwambie umesamehe au mwombe akusamehe hata kama yeye ndoo mkosaji.

  Haitasaidia kukaa nalo moyoni jambo lisilo leta faida

  usiku mwema
   
 2. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hakuna amani inayoshinda kusamehe...samehe mara saba sabini
   
 3. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni sawa,lakini lazima iwepo RIDHAA YA MOYO!Lakini kama samahani yenyewe haina chembe ya dhati ya moyo halitoki!Litaendelea kubaki tu kwenye chemba za moyo.
   
 4. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Wewe unaye ombwa msamaha ndo unatakiwa udhamirie kumsamehe.
   
 5. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wote,muombaji awe na dhamira ya dhati na mwombwaji nae pia awe na dhamira ya dhati,yaani DHATI kwa DHATI.Tatizo linabaki palepale.MOYO!Moyo hauaminiki kabisaaa.Moyo unaweza ukaudanganya MDOMO kwamba"toa tamko la kuomba samahani" na mdomo kwa kihelehele chake ukatoa tamko kumbe moyo wenyewe wala hauko radhi.
   
 6. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  SABA MARA SABINI!! Loh!!
   
 7. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nimebarikiwa hilo..huwa nasamehe kabla ya kuombwa msamaha.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kuna mambo mengine hayasameheki na hata ukisamehe ni ngumu kusahau.
   
 9. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  ebu tupe mfano halisi wa mammbo yasiyo sameheka
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Soma hii Signature ya SMU:

  Apologizing: does not always mean you are wrong and the other person is right. It just means you value your relationship more than your ego.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  mm huwa naumia sana lakini akija ku regret nitamsamehe ..huwa sipendi dharau ...na nikipenda nimependa ..
   
 12. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hongera sana kama ni kweli.
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ufisadi.
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mhhhh!!! Ngoja nilete vipimo vya TBS kuthibitisha
   
 15. m

  mtolewa Senior Member

  #15
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mkuu yapo mengi tu hasa yahusuyo mapenzi.ebu angalia yaliyonikuta mimi.NImeoa miaka kama 2 hivi iliyopita.kwa kuwa binti alikuwa wa kilikole na alikataa kabisa nisiTBS na zaidi marafiki zangu kama amegoma ni bora nisubiri baada ya harusi.basi nikaoa ila siku ya kwanza sikupata kitu maana alilala na shangazi yake kwa madai kuwa ni mila zao.basi nikapiga moyo konde kwani nilishavumilia zaidi ya mwaka na nusu sembuse siku moja!
  kesho yake mambo yakawa shwari lakini akawa analia sana mpaka nikamuuliza kwani vp? akasema anaumia sana kwani alikuwa bikra.basi mzee baada ya mechi ikabidi hata mashuka tubadili maana damu kama kawa! kesho yake asubuhi nikaona vinyama vyembamba juu ya rpg yangu.nikauliza vp tena? akaniambia nilimchubua sana usiku! machare yakanicheza kama nikamtafuta sista yangu mtaalam wa mambo ya town.akaniambia hakuna kitu hapo nimepelekwa town na kwamba hiyo ni made in beijing! du! loh ikaniluka kweli nikaamua kujifanya FBI kusaka data za huyu wife kabla hatujakutana naye.basi nikapata msada kutoka juu na chini nikapata data kibao chachu kuliko maelezo, mpaka bwana wake wa mwisho.niakamua kumtolea uvivu na kumuuliza baadhi akakubali na zingine akazipotezea.kifupi ni kwamba alinihadaa.amenisihi sana nimsamehe kwani tuna mtoto mchanga.kwa kweli roho inaniuma sana na nimeshindwa at teast kusahau na ninatamani tuachane ila kwetu wakristo tena kwa ndoa ya kanisani kuachana au kupeleka maombi ya kuachana kwa mchungaji kama vile kupiga penalti kwa kisigino pealti ya mwisho na ya ushindi mechi ya fainali! hapo kusamehe kunataka uwe na moyo wa mwendawazimu.
   
 16. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold Isije kuwa ndo ego alokoti FF hapo juu
   
 17. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  If you keep on judging people, u'll not get time to love them(MOTHER THERESA)!!! Umeshajua alikudanganya na hiyo ndo tabia ya kiumbe anaeitwa mwanadamu. Usipoteze muda kuendelea kumjaji kwa kosa lake ambalo utaliona ni kubwa mno, mwishoe upendo wako utachuja!! Mpe msamaha wa dhati na maisha yaendelee kwa amani ya roho, hata kama hutolisahau hilo kosa ila utaliona ni dogo na ni la kawaida!!!
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Kusamehe katika maisha ni kitu muhimu sana na ukiamua kusamehe basi usamehe 100% na siyo kusamehe nusu nusu ili isije siku za usoni tena ukazusha jambo ambalo ulishasamehe, "Unakumbuka mwezi fulani, ulifanya jambo hili ambalo liliniumiza sana."
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  hahahh..mimi nikishapenda siachi sema nina wivu mbaya
   
Loading...