FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,819
Pole sana mpiganaji wetu, usirudi nyuma, shikiria msimamo huo, tuko pamoja.
= shikilia
Pole sana mpiganaji wetu, usirudi nyuma, shikiria msimamo huo, tuko pamoja.
DAVID KAFULILA
TUME INATAKA KUNIHUJUMU KIGOMA KUSINI.
Kwanza Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya Mrisho Gambo walifanya kampeni kubwa na vitisho kwa wananchi wakitumia polisi.
Pamoja na hujuma zote hizo bado majumuisho kwa fomu za mawakala nimeongoza kwa kura 2435.
Kwa kujua hilo jana mgombea wa ccm Hasna Mwilima amekuja kukataa matokeo ya baadhi ya kata na kutaka zihesabiwe upya. Nikakataa kwa nguvu zote na nikamuonya msimamizi ache kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.
Msimamizi akamua kusitisha zoezi la majumuisho na kwamba anamwandikia barua Mkurugenzi wa uchaguzi taifa kwa mwongozo.
Msingi wa kukataa kuhesabu upya matokeo ni ukweli kwamba fomu za mawakala tunazo na hazina kasoro.ccm hawana fomu za mawakala wao.
Lakini sababu ya pili sina imani na masanduku kwamba hayajachakachuliwa kwani tangu baada ya kupiga kura yalikuwa chini ya polisi na tume wenyewe bila wakala. Na hili linakuwa na uzito kwasababu ya taarifa za magari ya kura feki yaloingizwa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya
Msimamo wangu ni kwamba sipo tayar kufungua masanduku na kuhesabu upya ni bora msimamizi akili ameshindwa kusimamia zoezi na uchaguzi ufutwe kuliko kuhesabu masanduku ambayo sina hakika nayo.
Naomba umma ujue haya kwa ufafanuzi wa kinachoendelea kwani mpaka sasa wamejaza polisi eneo hili kiasi cha kutisha.
Tulianza na Mungu na Hakika tunamaliza na Mungu.
David Kafulila

Kubali matokeo Kafulila afadhali ya nusu shari kuliko shari kamili,Filikunjombe yuko wapi leo?
Kama ww unauhakika kwamba mambo ni shwari kwann hautaki yafunguliwe? na kama umepigwa ni kuvumilia bro.
we mata.ko kweli
kazi kweli kweli sasa zitto anaingiaje hapa.
Aache kulialia aachie tu jimbo ndivyo mambo yalivyo.
Lazima Zitto aheshimiwe.
Muulize huyo ndugu yenu Kafulilla