David Kafulila: Tume inataka kunihujumu Kigoma Kusini

David Kafulila: Tume inataka kunihujumu Kigoma Kusini

Wanataka kufanya waliyomfanyia Wenje jana usiku wa manane?

Usikubali kufungua hata box moja!
 
david kafulila

tume inataka kunihujumu kigoma kusini.

Kwanza mkuu wa mkoa kigoma kanali issa machibya na mkuu wa wilaya mrisho gambo walifanya kampeni kubwa na vitisho kwa wananchi wakitumia polisi.

Pamoja na hujuma zote hizo bado majumuisho kwa fomu za mawakala nimeongoza kwa kura 2435.

Kwa kujua hilo jana mgombea wa ccm hasna mwilima amekuja kukataa matokeo ya baadhi ya kata na kutaka zihesabiwe upya. Nikakataa kwa nguvu zote na nikamuonya msimamizi ache kupokea maelekezo ya mkuu wa mkoa.

Msimamizi akamua kusitisha zoezi la majumuisho na kwamba anamwandikia barua mkurugenzi wa uchaguzi taifa kwa mwongozo.

Msingi wa kukataa kuhesabu upya matokeo ni ukweli kwamba fomu za mawakala tunazo na hazina kasoro.ccm hawana fomu za mawakala wao.

Lakini sababu ya pili sina imani na masanduku kwamba hayajachakachuliwa kwani tangu baada ya kupiga kura yalikuwa chini ya polisi na tume wenyewe bila wakala. Na hili linakuwa na uzito kwasababu ya taarifa za magari ya kura feki yaloingizwa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya

msimamo wangu ni kwamba sipo tayar kufungua masanduku na kuhesabu upya ni bora msimamizi akili ameshindwa kusimamia zoezi na uchaguzi ufutwe kuliko kuhesabu masanduku ambayo sina hakika nayo.

Naomba umma ujue haya kwa ufafanuzi wa kinachoendelea kwani mpaka sasa wamejaza polisi eneo hili kiasi cha kutisha.

Tulianza na mungu na hakika tunamaliza na mungu.

David kafulila
usikubali masanduku kufunguliwa tena....tumieni fomu za mawakala
 
Wanataka kufanya waliyomfanyia Wenje jana usiku wa manane?

Usikubali kufungua hata box moja!


Exactly....

Akikubali tu kufungua BOX hata moja, ATAANGUKA vibaya sanaa sanaa...!!

Sbb mabox yale yameshachakachukiwa sana baada ya kuhesabiwa... hivyo wanabadilisha haraka sana... so AKIKUBALI TU KIRUDIA kuhesabu ATUMIE FOMU ZA MATOKEO YA MAWAKALA zenye saini... ambazo ni halali na hapo HAWATAWEZA KUCHAKACHUA...!!!

Wenje, Kiwia, Nyerere na Lucy wa KIGAMBONI ndio mbinu iliyo tumika..!!!
 
DAVID KAFULILA

TUME INATAKA KUNIHUJUMU KIGOMA KUSINI.

Kwanza Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya Mrisho Gambo walifanya kampeni kubwa na vitisho kwa wananchi wakitumia polisi.

Pamoja na hujuma zote hizo bado majumuisho kwa fomu za mawakala nimeongoza kwa kura 2435.

Kwa kujua hilo jana mgombea wa ccm Hasna Mwilima amekuja kukataa matokeo ya baadhi ya kata na kutaka zihesabiwe upya. Nikakataa kwa nguvu zote na nikamuonya msimamizi ache kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.

Msimamizi akamua kusitisha zoezi la majumuisho na kwamba anamwandikia barua Mkurugenzi wa uchaguzi taifa kwa mwongozo.

Msingi wa kukataa kuhesabu upya matokeo ni ukweli kwamba fomu za mawakala tunazo na hazina kasoro.ccm hawana fomu za mawakala wao.

Lakini sababu ya pili sina imani na masanduku kwamba hayajachakachuliwa kwani tangu baada ya kupiga kura yalikuwa chini ya polisi na tume wenyewe bila wakala. Na hili linakuwa na uzito kwasababu ya taarifa za magari ya kura feki yaloingizwa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya

Msimamo wangu ni kwamba sipo tayar kufungua masanduku na kuhesabu upya ni bora msimamizi akili ameshindwa kusimamia zoezi na uchaguzi ufutwe kuliko kuhesabu masanduku ambayo sina hakika nayo.

Naomba umma ujue haya kwa ufafanuzi wa kinachoendelea kwani mpaka sasa wamejaza polisi eneo hili kiasi cha kutisha.

Tulianza na Mungu na Hakika tunamaliza na Mungu.

David Kafulila

Kama ww unauhakika kwamba mambo ni shwari kwann hautaki yafunguliwe? na kama umepigwa ni kuvumilia bro.
 
Komaa ndugu maana mkosamali keshazamishwa! Mawakala wanamalinzwa ile mbaya! Kama musoma mawakala walilambishwa mm wakaisha.
 
komaaa kafulila ukikubali imekula kwako.mwenzako wa chadema jimbo la rungwe ameshinda kisha kakubali warudie kuhesabu akabagwa
 
Kafulila anatafuta njia ya kutokea, ameshindwa vibaya hajui ataificha wapi sura yake, alilewa sifa mpaka kufikia hatua ya kuwatukana ndg zake ili kuwafurahisha mabwana zake!


Jimbo la Kigoma Kusini limerudi CCM na mshindi ametangazwa tangu jana, yeye anahangahika kwenye mitandao eti Tume inataka kumuhujumu teh teh teh mwambieni aende mahakamani!
 
Wanataka kufanya waliyomfanyia Wenje jana usiku wa manane?

Usikubali kufungua hata box moja!

Halafu huu utaratibu wa kuwepo mwanya wa kuhesabu upya lazima ufutwe! Unatucheleweshea matokeo sana! Yani ni lazima uwekwe utaratibu ambao matokeo ni lazima yatoke haraka! Mwaka huu labda tutavuka salama lakini 2020 Itakuwa shida sana.
 
naomba tu kuuliza mrisho gambo ni mkuu wa wilaya??huyu ni yupi?mana ambae namjua mimi alikua korogwe akaleta upumbavu na kutukana wazee tukamtimu sasa imekuaje huko tena yaan ccm bana hapa ndipo inapokoseaga.
Hawa wote ni wakuu wa wilaya na hata hao waliokuwa Nyamagana na Ilemela wametokea kwanye ukuu wa wilaya kwenda kugombea ubunge kama Mwakalebela, Asumpta nk.

Kwa kifupi kuna taasisi hii ya ukuu wa wilaya ambao ni karibia 180 na wote wakiwa na V8, posho na mishahara mikubwa wengi ni watu ambao ni public 'rejects' na huko ndiko wanahifadhiwa wakisubiri zali.

Ngoja tusubirie labda mzee wa Bunda na mawaziri wengine walioanguka wanaweza kuteuliwa kabla hii week haijaisha!

 
kOMAA kaka HAWA CCM WAMESHAIBA MAJIMBO MENGI SANA KWA KUKUBAILI KURUDIA KUHESABU KURA KAMA NYAMAGANA
 
naomba tu kuuliza mrisho gambo ni mkuu wa wilaya??huyu ni yupi?mana ambae namjua mimi alikua korogwe akaleta upumbavu na kutukana wazee tukamtimu sasa imekuaje huko tena yaan ccm bana hapa ndipo inapokoseaga.

Jk alimteua tena wiki 2 zilizopita kwenda huko kwa Kafulila. Kazi yake ndio hiyo umeiona.
 
Dw, cnn, bbc, na vyombo vyote vya habari vya nje milikeni uhuni unao taka kufanyika kwa mpiganaji wetu huyu david kafulila, hatuwezi kuwapotea majembe wa kukemea uchafu bungeni na selikalini na kuruhusu watu wa kupiga igelegele tutakuwa hatujaitendea haki tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom