David Kafulila: Tume inataka kunihujumu Kigoma Kusini

David Kafulila: Tume inataka kunihujumu Kigoma Kusini

Ukishinda wewe sawa,akishinda mwingine umechakachuliwa.Mbona wengine wanashindwa wanakaa kimya ina maana huko ambako UKAWA wameshinda Tume imewapendelea.Upuuzi mtupu.Maamuzi ya wananchi wengi yaheshimiwe.
 
DAVID KAFULILA

TUME INATAKA KUNIHUJUMU KIGOMA KUSINI.

Kwanza Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya Mrisho Gambo walifanya kampeni kubwa na vitisho kwa wananchi wakitumia polisi.

Pamoja na hujuma zote hizo bado majumuisho kwa fomu za mawakala nimeongoza kwa kura 2435.

Kwa kujua hilo jana mgombea wa ccm Hasna Mwilima amekuja kukataa matokeo ya baadhi ya kata na kutaka zihesabiwe upya. Nikakataa kwa nguvu zote na nikamuonya msimamizi ache kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.

Msimamizi akamua kusitisha zoezi la majumuisho na kwamba anamwandikia barua Mkurugenzi wa uchaguzi taifa kwa mwongozo.

Msingi wa kukataa kuhesabu upya matokeo ni ukweli kwamba fomu za mawakala tunazo na hazina kasoro.ccm hawana fomu za mawakala wao.

Lakini sababu ya pili sina imani na masanduku kwamba hayajachakachuliwa kwani tangu baada ya kupiga kura yalikuwa chini ya polisi na tume wenyewe bila wakala. Na hili linakuwa na uzito kwasababu ya taarifa za magari ya kura feki yaloingizwa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya

Msimamo wangu ni kwamba sipo tayar kufungua masanduku na kuhesabu upya ni bora msimamizi akili ameshindwa kusimamia zoezi na uchaguzi ufutwe kuliko kuhesabu masanduku ambayo sina hakika nayo.

Naomba umma ujue haya kwa ufafanuzi wa kinachoendelea kwani mpaka sasa wamejaza polisi eneo hili kiasi cha kutisha.

Tulianza na Mungu na Hakika tunamaliza na Mungu.

David Kafulila

- Wote waliokubali zoezi la kuhesabu upya wameanguka, hivyo usikubali!

- Kwani mkuu wa Mkoa ni nani katika Tume?

- Vyema timu iliyoshinda, Kubenea, Lissu, Mnyika, Mdee nk waje huko kukuongezea nguvu!
 
Exactly....

Akikubali tu kufungua BOX hata moja, ATAANGUKA vibaya sanaa sanaa...!!

Wenje, Kiwia, Nyerere na Lucy wa KIGAMBONI ndio mbinu iliyo tumika..!!!

Hivi inakuwaje watu wanakubali kura zihesabiwe upya wakati form za kila kituo zipo? Tume imejitahidi kuwasaidia watu lakini bado hawaelewi tu. Kinachokiwa hapo ni Calculator tu na itumike kujumlisha kura za vituoni.
 
Kafulila acheni arufdi bungeni arooooo.....au mnataka kuanzisha ESCROW PART II?
 
Ukishinda wewe sawa,akishinda mwingine umechakachuliwa.Mbona wengine wanashindwa wanakaa kimya ina maana huko ambako UKAWA wameshinda Tume imewapendelea.Upuuzi mtupu.Maamuzi ya wananchi wengi yaheshimiwe.

...kibaraka wa zzk unaumiaaaa...
 
Aache kulialia aachie tu jimbo ndivyo mambo yalivyo.

Lazima Zitto aheshimiwe.

We mata.ko nani kakwambia kwamba ameshindwa? Hii tume haiko huru ndo maana huu upumbavu unafanyika! Hivi Mkuu wa mkoa na DC wanapata wapi guts za kuiamrisha tume? Kafulila kijana wangu komaa nao mpaka.kieleweke! Kama ulimwangusha yule mwizi ije iwe huyu kaha.ba?
 
david pole. aliyeujumu upinzani nja huu ni rafiki yajo kzzkx. huyu katumika na systemna alitaka muamie ACT mkakataa sasa anataka mjanyagwe twe baada ya mkurupukaji machali kugongwa. watch oout huyo si rafiki ni nyoka. upinzan mkoa wa kigoma amuua ila yeye kajiimalisha
 
Usikubali kamanda, hawataki utinge mjengoni coz utawafichua mafisadi wao..!!
 
Huu mtego ndiyo uliomnasa Hezekia Wenje wa Nyamagana, Mwanza!

Say no kamanda, otherwise huyo mgombea wa CCM pamoja na huyu msimamizi wa uchaguzi watumie fomu za matokeo halali zilizosainiwa na mawakala wote kuhakiki kura zao kama haamini kuwa ameshindwa!!
 
Kafulila hana ubavu wa kukataa kura kuhesabiwa.ni haki ya mgombea.hata kubenea aliomba kura zihesabiwe,,,mnyika pia 2010.kafulila akubali tu badala ya kujenga mazingira ya kuonewa
 
Zitto hahusiki hapa ila tunajua hao ni wale wasiomtakia mema kafulila.pigana kufa tuko nyuma yako tunakuombea
 
mgombea ana haki ya kufanyika recount,,sababu za kafulila kukataa kuhesabu upya hazina logic....
kama zitaongezeka kura fake si hazitaona na daftari la wapiga kura,,wasiwasi wake ni ni ?
 
Back
Top Bottom