David Kafulila,na Serikali Tatu

David Kafulila,na Serikali Tatu

kwa kweli huyu jamaa yuko njema sana.

Mkuu umenena vema. Kijana ameongea mambo mazito mno tena yenye kujenga sana. Kwa wasiojua Kafulila anatoka kamati namba tano ambayo mwenyekiti wake ni yule mama mwenye kelele nyingi bungeni - ANNA KILANGO MALECELA.
 
Mimi ni Mtanzania wa kuzaliwa mama Mdengereko na Baba Muhehe, naambiwa wahehe ni wandereko waliosogea zamani. Naamini na Wazanzibar ni watanzania walio chukuliwa na utumwa zamani na kuna walio amia wenyewe hila aliondoi asili yao napigania muungano wa watu wamoja.

Wewe je unajitambua?
Unapoambiwa hujitambui si kwamba hujui kabila lako, ina maana hujui kwa nini ulizaliwa na umezaliwa ili ufanye nini na hujui umuhimu wako kwa jamii inayokuzunguka.

Kama wewe ni Mtanzania je unajua asili ya Tanzania na kwa nini iliitwa Tanzania? Je wazazi wako waliozaliwa kabla ya Tanzania watajiita Watanzania? Kama ndivyo ikitokea shirikisho la EAC likaungana na kuwa nchi moja wewe utajiitaje MEAC?
 
Unapoambiwa hujitambui si kwamba hujui kabila lako, ina maana hujui kwa nini ulizaliwa na umezaliwa ili ufanye nini na hujui umuhimu wako kwa jamii inayokuzunguka.

Kama wewe ni Mtanzania je unajua asili ya Tanzania na kwa nini iliitwa Tanzania? Je wazazi wako waliozaliwa kabla ya Tanzania watajiita Watanzania? Kama ndivyo ikitokea shirikisho la EAC likaungana na kuwa nchi moja wewe utajiitaje MEAC?
Asili ipi unayo itaka wewe ya uhamiaji wa wa holela wa wabantu kabla ya kuwa settlers, asili inayorudi kwa watemi na ufalme wa settlers au unatataka asili ya jina Tanzania ambalo limechanganya herufi za Tanganyika na Zanzibar kuzaa neno Tanzania kama heshima ya muungano au unadhani neno Tanzania lilitungwa tu from no where?

wewe ndio ujitambui na --------- sio mimi.

Jamani mods neno 'used' as in exploited kwa kiswahli linahitaji kuwa blocked, majanga.
 
Mh kafulila ameongea vema tena kwa hoja nzito nadhani wajumbe wengi hasa ccm watakuwa wamechanganyikiwa coz km ofisi ya raisi ilipendekeza serikali 3 kwa nini raisi huyohuyo anatoka hadharani anadai serikali 2 ?
 
Kwenye uzi kama huu sitegemei kuwaona watu wenye uelewa mdogo na ushabiki wa siasa zenye mlengo mufrisi kama FaizaFoxy lusungo ifweero MSALANI ManDlajr na wajinga wajinga wengine wanaoabudu pale Lumumba.
viva Kafulila viva UKAWA mwendo ni uleule nyie ndio wajenga nchi nasi tupo nyuma yenu.
 
Last edited by a moderator:
Utumwa ni kulilia mkoloni na mambo yake kuanzia majina aliyo tuachia kama tanganyika na siasa za CUF na Jamsheed wao. Mimi ni mwafrikna na proud of being one na ntapigania chochote chenye kulinda hadhi yetu including umoja wetu.

Mtumwa ni yule anaejitambulisha kinyume na hapo na kuona mambo anayofanya mwafrika na jitihada za kujikomboa hazina maana.

Unasema utampinga mkoloni na mambo yake yote. Mbona hapa unatumia kiingereza, reli, meli, ...?
Mbona huikatai mipaka ya nchi iliyoachwa na mkoloni?
Kuwa huru si kukataa kila kitu alichoacha mkoloni, na kuendeleza kila kilichofanywa na Mwafrika.
Ukweli utakuweka huru.
 
Natamani kamati zingine zilizosalia ziweke wasemaji aina ya kina Kafulila ili tupate ladha halisi ya mijadala bungeni.
 
Sasa sijui nani ni kipofu kati ya mimi na wewe, hivi kutetea serikari mbili ni kutetea CCM. Kweli CDM wamewachukua na akili nyie watu, hivi wewe kwanini unaitaka Tanganyika? wewe kama wewe na si kwa akili za kuambiwa.

Umenifanya niichukie bure movie ya Happy Feet sababu za ubazazi wako
 
Unasema utampinga mkoloni na mambo yake yote. Mbona hapa unatumia kiingereza, reli, meli, ...?
Mbona huikatai mipaka ya nchi iliyoachwa na mkoloni?
Kuwa huru si kukataa kila kitu alichoacha mkoloni, na kuendeleza kila kilichofanywa na Mwafrika.
Ukweli utakuweka huru.

Mkuu angalia usije jikuta unajadili na id inayomilikiwa na kikundi cha `wale`
 
Jameni iwekeni hapa hotuba yake mi wa huku makete njombe niione.ila yule jamaa ni mzuri kwa hoja,tatizo anaharaka kama kiongozi wa act aliyeko mafichoni
 
mi nashanngaa ccm wanaposema kuwa watu elfu17 waliotoa maoni juu ya serikali 3 ni wachache kati ya watanzania milioni 45,wakumbuke hata ridhwan kikwete alichaguliwa na watu elfu 20 tu katika jimbo la chalinze juzi,lakini wakumbuke jimbo hilo lina watu waliojiandikisha laki moja hivyo ni asilimia 20 tu achilia mbali wananchi wote wajimbo la chalinze,huyo kikwete mwenyewe je alichaguliwa na wananchi wangapi kati ya watanzania milioni 40 wa wakati huo,WATANZINIA WA WALEO SIO WALE WA ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI HATA FIKRA HIZO NI ZA KIPUUZI ZIDUMU TU
 
Asili ipi unayo itaka wewe ya uhamiaji wa wa holela wa wabantu kabla ya kuwa settlers, asili inayorudi kwa watemi na ufalme wa settlers au unatataka asili ya jina Tanzania ambalo limechanganya herufi za Tanganyika na Zanzibar kuzaa neno Tanzania kama heshima ya muungano au unadhani neno Tanzania lilitungwa tu from no where?

wewe ndio ujitambui na --------- sio mimi.

Jamani mods neno 'used' as in exploited kwa kiswahli linahitaji kuwa blocked, majanga.

Mnyalu usiye jua historia ya nchi.
 
Jameni iwekeni hapa hotuba yake mi wa huku makete njombe niione.ila yule jamaa ni mzuri kwa hoja,tatizo anaharaka kama kiongozi wa act aliyeko mafichoni

hakika amejenga hoja, labda tu kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kufuatilia niwape baadhi ya hoja alizojenga
1: kama kuna watu (ccm) ambao wanadai maoni ya watu 17000 juu ya kuwa na serikali 3 ni idadi ndogo sana ambayoyo haiakisi matakwa ya watanzania 46ml, je hawa wabunge 600 wanapata wapi nguvu ya kuwa na uwakilishi wa wananchi ili hali wao ni wachache zaidi kuliko hata hao waliotoa maoni juu ya kuwa na serikali 3?
2: Amehoji kama ishu ni kumtii mwl nyere ambae hakuta kuvunjika kwa muungano,wamesahau kuwa mwl alikuwa anabadilika kulingana na wakati. Mf mwaka 1965 mwl alifuta vyama vingivlakini kulingana na mabadiliko yaliyohitaji mageuzi mwaka 1992 ni mwl uyohuyo aliweze kuwa na vyama vingi ambavyo alivifuta hapo mwanzo. Akauliza je mwl angekufa kabla ya kuanzishwa vyama vingi inamaana mpaka sasa kungekuwa na chama kimoja tu?
3: Viongozi waliopo madarakani leo wafanikishe kuwa na muungano mzuri zaidi wa serikali 3 kwakuwa hii nafasi walionayo hawatakuwa nayo tena miaka ijayo kwani ni dhahir wingi wao (ccm) utapungua hivyo watalazimika kukubali mabadiliko kwa shinikizo kubwa kitu ambacho kitazalisha muundo mbovu zaidi . Hili alitoa kama ushauri kwa viongozi waliopo madarakani kutumia hii nafasi kufanya mabadiliko mazuri tena kwa busara kuliko kusubiri presha hapo baadae.
4: Kama ishu ni mapato ya serikali ya muungano,amependekeza mapato yatokanayo na customs yote yawe ya muungano. Akafafanua kuwa zipo hoja kuwa kuna wanaodai ikiwa hivyo bara(tanganyika) italipa zaidi,akasema hilo sio shida kwani matumizi makubwa ya hiyo fedha yataelekezwavbara pia kwenye maeneo kama ya magereza,ulinzi,uhamiaji,polis nk. Akauliza wanaodai kuwa hili likitekelezwa watu wa bara watabeba huo mzigo,je kwa sasa ni kinani wanabeba huo mzigo?
5: Akaeleza kuwa tafiti zinaonesha kuwa muungano upo kwenye maeneo matatu ambayo ni ; serikali moja, serikali ya shirikisho na ile ya mkataba. Sasa hii yetu ni ya mfumo gani mbona haieleweke inafiti mfumo gani?
6: Akauliza kuwa kwakuwa muungano huu uliopo kwa sasa umedumu kwa takribani miaka 50, na umeshindwa kutatua changamoto zilizojitokeza kwa kipindi chote cha nusu karne, Je viongozi wanataka wapewe karne kangapi zaidi ili waweze kutatua hizi changamoto zilizopo?
7: Akafafanua zaidi kwa kusema wanaomhukumu jaji warioba wanamuonea. Akaeleza kuwa ukifanya tafiti na ukapata majibu kama ya wale walikutangulia kufanya tafiti maana yake ni kwamba hayo majibu ni sahihi. Sasa kwakuwa tume zilizomtangulia jaji warioba pamoja na wataalamu mbalimbali waliwahi kufanya tafiti juu ya muundo wa muungano na kuja na majibu ya serikali 3 inakuwaje leo wakatae hoja ya warioba ilihali inaendana na hoja za watangulizi wake kwenye jambo hilo?
8:Amehoji kama ofisi ya raisi,ya makamu wa raisi na ya waziri mkuu zote zilipendekeza serikali 3 inakuwaje tena ndani ya muda mfupi watu haohao wageuke na kudai serikali 2, au walitoa hayomaoni ili mwishowe waje wamdhalilishe jaji warioba?
9: Akaeleza kuwa yeye ni kijana mdogo lakini anamuheshimu sana jaj warioba. Akadai anashangazwa na watu wakawaida sana ( ambao ni wajumbe wa bunge la katiba - kwa mtizamo wangu lakini) ambao wanamdharau jaji warioba ilihali sio level yao kabisaa kwani jaji warioba yupo next level kabisa na anaheshimika ndani na nje ya nchi, hivyo inakuwaje watu wa kawaida sana wamtreat jaji warioba kwa kiwango cha chini sana ili hali yeye sio level yao?
10: Muundo wa serikali 3 ndio utakaotatua changamoto za sasa na zijazo,kuliko kufichaficha mambo kwa kisingizio cha serikali mbili kwani huko tuendako kutakuwa kigumu sana.
11: ....................nikikumbuka mengine nitayatupia hapa.....
 
Back
Top Bottom