hakika amejenga hoja, labda tu kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kufuatilia niwape baadhi ya hoja alizojenga
1: kama kuna watu (ccm) ambao wanadai maoni ya watu 17000 juu ya kuwa na serikali 3 ni idadi ndogo sana ambayoyo haiakisi matakwa ya watanzania 46ml, je hawa wabunge 600 wanapata wapi nguvu ya kuwa na uwakilishi wa wananchi ili hali wao ni wachache zaidi kuliko hata hao waliotoa maoni juu ya kuwa na serikali 3?
2: Amehoji kama ishu ni kumtii mwl nyere ambae hakuta kuvunjika kwa muungano,wamesahau kuwa mwl alikuwa anabadilika kulingana na wakati. Mf mwaka 1965 mwl alifuta vyama vingivlakini kulingana na mabadiliko yaliyohitaji mageuzi mwaka 1992 ni mwl uyohuyo aliweze kuwa na vyama vingi ambavyo alivifuta hapo mwanzo. Akauliza je mwl angekufa kabla ya kuanzishwa vyama vingi inamaana mpaka sasa kungekuwa na chama kimoja tu?
3: Viongozi waliopo madarakani leo wafanikishe kuwa na muungano mzuri zaidi wa serikali 3 kwakuwa hii nafasi walionayo hawatakuwa nayo tena miaka ijayo kwani ni dhahir wingi wao (ccm) utapungua hivyo watalazimika kukubali mabadiliko kwa shinikizo kubwa kitu ambacho kitazalisha muundo mbovu zaidi . Hili alitoa kama ushauri kwa viongozi waliopo madarakani kutumia hii nafasi kufanya mabadiliko mazuri tena kwa busara kuliko kusubiri presha hapo baadae.
4: Kama ishu ni mapato ya serikali ya muungano,amependekeza mapato yatokanayo na customs yote yawe ya muungano. Akafafanua kuwa zipo hoja kuwa kuna wanaodai ikiwa hivyo bara(tanganyika) italipa zaidi,akasema hilo sio shida kwani matumizi makubwa ya hiyo fedha yataelekezwavbara pia kwenye maeneo kama ya magereza,ulinzi,uhamiaji,polis nk. Akauliza wanaodai kuwa hili likitekelezwa watu wa bara watabeba huo mzigo,je kwa sasa ni kinani wanabeba huo mzigo?
5: Akaeleza kuwa tafiti zinaonesha kuwa muungano upo kwenye maeneo matatu ambayo ni ; serikali moja, serikali ya shirikisho na ile ya mkataba. Sasa hii yetu ni ya mfumo gani mbona haieleweke inafiti mfumo gani?
6: Akauliza kuwa kwakuwa muungano huu uliopo kwa sasa umedumu kwa takribani miaka 50, na umeshindwa kutatua changamoto zilizojitokeza kwa kipindi chote cha nusu karne, Je viongozi wanataka wapewe karne kangapi zaidi ili waweze kutatua hizi changamoto zilizopo?
7: Akafafanua zaidi kwa kusema wanaomhukumu jaji warioba wanamuonea. Akaeleza kuwa ukifanya tafiti na ukapata majibu kama ya wale walikutangulia kufanya tafiti maana yake ni kwamba hayo majibu ni sahihi. Sasa kwakuwa tume zilizomtangulia jaji warioba pamoja na wataalamu mbalimbali waliwahi kufanya tafiti juu ya muundo wa muungano na kuja na majibu ya serikali 3 inakuwaje leo wakatae hoja ya warioba ilihali inaendana na hoja za watangulizi wake kwenye jambo hilo?
8:Amehoji kama ofisi ya raisi,ya makamu wa raisi na ya waziri mkuu zote zilipendekeza serikali 3 inakuwaje tena ndani ya muda mfupi watu haohao wageuke na kudai serikali 2, au walitoa hayomaoni ili mwishowe waje wamdhalilishe jaji warioba?
9: Akaeleza kuwa yeye ni kijana mdogo lakini anamuheshimu sana jaj warioba. Akadai anashangazwa na watu wakawaida sana ( ambao ni wajumbe wa bunge la katiba - kwa mtizamo wangu lakini) ambao wanamdharau jaji warioba ilihali sio level yao kabisaa kwani jaji warioba yupo next level kabisa na anaheshimika ndani na nje ya nchi, hivyo inakuwaje watu wa kawaida sana wamtreat jaji warioba kwa kiwango cha chini sana ili hali yeye sio level yao?
10: Muundo wa serikali 3 ndio utakaotatua changamoto za sasa na zijazo,kuliko kufichaficha mambo kwa kisingizio cha serikali mbili kwani huko tuendako kutakuwa kigumu sana.
11: ....................nikikumbuka mengine nitayatupia hapa.....