Mkuu,nikiri kwanza kuwa mimi ni Wakili ingawa sijui kama ni mzuri au la. Mkuu,masuala la kijamii huongozwa na sheria. Zaweza kuwa Sheria zitungwazo na Bunge au zile ndogondogo. Masuala haya hayapaswi kuendeshwa kwa kauli za viongozi.
Kimsingi,serikali ina wajibu wa kujenga miundombinu mbalimbali kwa wananchi. Kisheria,mwananchi hana wajibu wa kujenga miundombinu kwa njia ya kuchanga. Sababu ni kuwa mwananchi si mkusanya kodi,mtunza fedha na mpanga mipango.
Hatahivyo wananchi wanaweza kuridhia kuchanga michango mbalimbali. Si kwa njia ya kushurutishwa. Wanapaswa kushawishiwa na kuombwa kuchanga.
Asante Mkuu