David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kama amejivua anadhihirisha kuwa alikuwa mnafiki na mzigo katika chama kwa hiyo wamemshtukia.
 
jamani mtu kufanya mabadiliko kwenye safu ya uongozi inakuwa tabu.....kaamua kumpa mtu mwingine ili kuandeleza yale david kayashindwa
 
Kama amejivua anadhihirisha kuwa alikuwa mnafiki na mzigo katika chama kwa hiyo wamemshtukia.

Mpwa pamoja na hilo lakini uliona wapi sehemu kusikokuwa na nidhamu? kama alivuliwa uongozi na yeye anajivua hadi uanachama ndo yale ya kumwaga mboga nimwage ugali lakini hapo anakosa yeye na sio Chadema!


Halafu nina mashaka hapa hii habari ni kutupima upepo kuona kama akijivua itakuwaje.....
and is this supposed to be news? kwani atapokelewa na JK kupewa kadi ya CCM?
 
Mkuu Masanilo habari za Kyela....

We Mzee umeanza kusahau majina yako?ujanja wa kubadili badili majina wachie vijana.sasa umeanza kujiuliza mwenyewe. Mi niko Kyela Dr. naona siasa za kyela zimemshinda..
 
Kama kweli kafanya hilo let him go! Who is he anyway?
 
Nakumbuka Hayati baba wa taifa aliwahi kusema pale jangwani kuwa upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm na chama kitachoisumbua ccm ni CUF hasa kule zanzibar,kwa mantiki hiyo kupasuka na kuyumba kwa baadhi ya vyama vya upinzani kama chadema sitoshangaa kabisa.

mkuu David karibu CCM KAMA vipi uje uchukue kadi katika kata yetu ya chang'ombe.
 
Mosi - Huyu jamaa alikuwa CCM ndani ya CHADEMA, ni vizuri kajitambulisha mapema
Pili - Kumbuka alivyotumwa Guninita; alitoka na CHADEMA ikawa imara
Nidhamu ni muhimu - hata Maximo kaliweka wazi hilo!
 
Alisema kwenye Majira Nov 8 na Mwananchi Nov 9 kuwa Mbowe na Dr Slaa wamefanya kikao kisicho rasmi cha Gheto huko Dodoma na kufikia maamuzi ya kumvua uanachama. Akaitwa na sekretariati ya chama kuhojiwa akakiri kwamba kweli amesema maneno hayo. Akaambiwa athibitishe kuwa kikao cha Dodoma kilijadili kumfukuza uanachama akasema hana ushahidi wowote ila ameelezwa maneno hayo na waandishi wa habari. Akaambiwa akanushe maneno yake, akakataa. Akaambiwa aombe msamaha, akakataa. Uteuzi wake ukatenguliwa kutokana na kukiuka maadili ya chama kifungu cha 10 kinachokataza viongozi kutoa siri za chama, kuzingatia mipaka ya kimamlaka katika kutoa kauli za chama, kuepuka kuwatuhumu viongozi wengine hadharani bila kupitia vikao halali vya chama na kuacha kutoa tuhuma za uongo

serayamajimbo
Nadhani kama tuhuma hizi ni za kweli basi alifanya kosa la msingi kutenguliwa uongozi wake na sio kuvuliwa uanachama. angombamsamaha ndani ya chama yangeisha nadhani.
 
....kwanza walikuwa CCM kabla, na pili wataenda CCM wataniacha mimi CHADEMA. CHADEMA kwangu mimi ni zaidi ya chama, ni Movement! Ni vuguvugu la harakati za kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na demokrasia pana zaidi bila kuathiri uzalendo wa Taifa letu.
Huyo kafulila aangalie asije akazunguka vyama vyote vya siasa kama Abas Mtemvu, inabidi aangalie dhamira yake katika siasa ni nini hasa, maslahi au ukombozi wa wengi!!
 
waJF,Habari za Kafulila ni za kweli. (source😀aily news)

Kafulila quits Chadema!
The former Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Information Officer, Mr David Kafulila has just announced his decision to quit from the party from today, a few hours ago.

However, Mr Kafulila who made headlines last week after the party's top leaders, led by Chadema's Secretary General, Dr Wilbroad Slaa, suspended him from his position, said that he is not planning to join any other political party.

Speaking at a press conference at MAELEZO this noon, Mr Kafulila said that his decision follows a long antagonistic movement with top party leaders who took the decision to suspend him as a technique to shut him down from raising issues of national interest especially mismanagement of fund within the party.

"In CHADEMA they do not want the member who asks anything about the direction of the party in different issues, I know what made me to be suspended was my strength in questioning some matters for the aim of making strong opposition party but the leaders there they don not want strong party" he complained.

His suspension from his position, was publicly opposed by the party's Deputy Secretary General, Mr Zitto Kabwe, who expressed his disbelief of the decision, saying he will follow up the matter and urging the party's members to stay calm during the disarray.
Source😀aily news ONLINE REPORTER, 18th November 2009)
 
Another melancholy, not for Chadema for all who want changes
 
Kama alifuata cheo Chadema na akavuliwa, basi malengo yake hayakutimia. Lakini kama alifuata mkumbo wa kujiunga na vyama ili kufanya ushushushu, bado ni mdogo na hatafika mbali. Na zaidi pia, atakuwa amepotea njia kama atakwenda CCM kwani hana mtaji wa kupendekezwa kwa nafasi ya uwakilishi. Ukishikwa, shikamana! Au hakumbuki ya Nturungeyi na Mrema TLP, Jidulama... na Cheyo UDP, CCM na Njelu?? Anaweza akawa amenyea kambi mapema mno!
 
Kama alifuata cheo Chadema na akavuliwa, basi malengo yake hayakutimia. Lakini kama alifuata mkumbo wa kujiunga na vyama ili kufanya ushushushu, bado ni mdogo na hatafika mbali. Na zaidi pia, atakuwa amepotea njia kama atakwenda CCM kwani hana mtaji wa kupendekezwa kwa nafasi ya uwakilishi. Ukishikwa, shikamana! Au hakumbuki ya Nturungeyi na Mrema TLP, Jidulama... na Cheyo UDP, CCM na Njelu?? Anaweza akawa amenyea kambi mapema mno!
Wako wengi wa aina yake wakivuliwa uongozi hutimka..mfano...LWAKATARE ..never trust this kind of people..lol
 
Kafulila quits Chadema!


Kafulila kwa maelezo yake kilichomtoa CHADEMA ni mambo mawili (1) Matumizi mabaya ya fedha za chama (2) Hakuna demokrasia ndani ya chama-viongozi hawapendi mwanachama makini anayeuliza mambo yanayousu muelekeo wa chama ktk mambo mbali mbali.

Je wana chadema wakiwemo viongozi ili mnasemaje? je ni kweli ndani ya chama internal demokrasi ni zero na kuhusu ufujaji wa pesa ili likoje? naomba kuwasilisha.
 
Saizi nanunua BigG kama mzee wa kutafuna Furgoson, 2010 jinsi wana CHADEMA watakavyokuwa wakijaribu kuzihadaa akili zao ohhhhhhhhh tumeibiwa kura oooohhhhh makomando wa wa ccm wamewapiga.

Wao kupigwa konzi tu na makomandoo kama ni kweli wanalalamika aaaaaaaa LAKINI wao kunyonga na kuwashusha watu majukwaani kwa MAKOMBEO,MAWE na SULULU wanashamgilia kweli.

Sijawahi kuona akili mbovu kiasi cha MODE hii.
 
The Following User Says Thank You to Masanilo For This Useful Post:
Shalom (Today)


Masanilo = Shalom
He he heeee !!! Halafu anajipa Thanks kwa ID nyingine!

Uko smart sana wewe ajabu umeingia mkenge mazee!
 
Kafulila quits Chadema!


Kafulila kwa maelezo yake kilichomtoa CHADEMA ni mambo mawili (1) Matumizi mabaya ya fedha za chama (2) Hakuna demokrasia ndani ya chama-viongozi hawapendi mwanachama makini anayeuliza mambo yanayousu muelekeo wa chama ktk mambo mbali mbali.

Je wana chadema wakiwemo viongozi ili mnasemaje? je ni kweli ndani ya chama internal demokrasi ni zero na kuhusu ufujaji wa pesa ili likoje? naomba kuwasilisha.

Kafulila

Kwa mfano, Mh Chacha anazungumza hadharani kuwa ruzuku ya chama haiendi mikoani. Lakini anasahau kuwa Kamati Kuu ilisha agiza kuwa kila mkoa ufungue akaunti utumiwe sh 100,000/=(laki moja kwa mwezi). Je Chacha anaweza kutoa mfano wa mkoa uliokwisha fungua akaunti na haujatumiwa pesa hiyo?..Sio hayo, kila wilaya yenye diwani na zile za makao makuu ya mkoa ziilikwishaagizwa kufungua akaunti ili zitumiwe sh 200,000/= kwa mwezi tangu mwaka 2007.

Na ikumbukwe kuwa CHADEMA kinapata ruzuku ya kiasi cha takribani milioni60 kwa mwezi,dhidi ya CCM inayopata ruzuku ya bilioni1.2 kwa mwezi(takribani mara20 ya ile ya CHADEMA). Ruzuku ya CCM kwa mwezi ni takribani sawa na jumla ya ruzuku ya CHADEMA kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.

Mkuu Majibu alishatoa mwenyewe kafulila
 
Samahani Brooklyn, hivi wewe ndiye Leila Abdul? Kuna jamaa amekuexpose ndo maana nakupa tahadhari uwe makini na maYahoo/Google group, mengine yana members wasio waaminifu. Angalia post hizi mbili:
Naamini nidhamu katika chama ni muhimu kuliko kitu kingine chochote. Kuhama chama si suluhisho la matatizo. Alihama Mrema CCM na bado CCM ikaendelea, sembuse David Kafulila Chadema!!

Slaa na Mbowe imarisheni nidhamu katika chama ili kuepuka migongano isiyo na tija kama hii inayotokea CCM sasa!!

Leila Abdul
From: Leila Abdul <hifa...@gmail.com>
Date: Wed, 18 Nov 2009 06:18:50 -0800 (PST)
Local: Wed, Nov 18 2009 9:18 am
Subject: Re: DAVID KAFULILA AJIVUA UANACHAMA WA CHADEMA




Naamini nidhamu katika chama ni muhimu kuliko kitu kingine chochote.
Kuhama chama si suluhisho la matatizo. Alihama Mrema CCM na bado CCM
ikaendelea, sembuse David Kafulila Chadema!!
Slaa na Mbowe imarisheni nidhamu katika chama ili kuepuka migongano
isiyo na tija kama hii inayotokea CCM sasa!!
 
Jamani who is this Kafulila?? I mean as a person, can we have his profile here??

Isije tukawa tunapoteza muda na mtu ambaye asingeweza kukua ka kasi ya chama [yaani mwanapropaganda tu!!]

MTM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom