David Kafulila ajiunga rasmi na CCM huko Mbweni jijini Dar

David Kafulila ajiunga rasmi na CCM huko Mbweni jijini Dar

Kafulila ni ^Popo^
najua kabisa yuko CCM kwa kiakili.
ila Moyo wake uko Upinzani .
Ndo maana kavaa kofia kichwani
 
Nafikiria jinsi atakapokutana na Werema, Tibaijuka, Ngeleja, Chenge nk wazee wa Escrow. Nadhani kafuata mgao huyu siyo mwanasiasa ila ni opportunist tu
 
Chadema haipo tayari kuchukua nchi, sasa hivi ni kama kikundi cha wapiga deal....

Hawana tena ajenda ya kumshawishi Mtanzania tena yaani chadema hawaaminiki tena.......
 
hongera zake ni haki yake, nasisitiza, kwa msisitizo, huyu mtu asibezwe, ana hoja za msingi, asikilizwe na hoja zake zifanyiwe kazi!.
Hili nimelizungumza hapa

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Paskali

Sehemu kubwa Paskali una tatizo fulani, unaanzisha mada ndefu, kisha ukitakiwa utoe ufafanuzi ama kujibu hoja kinzani unaishia kutoa Like. Hakuna anayehitaji Like zako kwa sana, cha muhimu ni kuona ukitoa au kujibu hoja kinzani. Jirekebishe kwenye hili kwani huwa una nyuzi ndefu hivyo kuzitendea haki shiriki mjadala.
 
Chadema haipo tayari kuchukua nchi, sasa hivi ni kama kikundi cha wapiga deal....

Hawana tena ajenda ya kumshawishi Mtanzania tena yaani chadema hawaaminiki tena.......

Mkuu ni kweli, je ni kwanini sasa polisi wanawapiga mabomu, kuwajeruhi na hata kuachia mikutano yao kufanyiwa hujuma mbele ya polisi?
 
historia ni mwalimu mzuri, ukikumbuka matendo ya kisiasa ya Kafulila hautashangaa hili la sasa.

Kafulila alijitoa Chadema kwenye kama mwaka 2009 au 2010 akajiunga NCCR, mwishoni mwa mwaka 2011 akafukuzwa uanachama wa NCCR bahada ya kuharibu, akampigia magoti hadi James Mbatia huku akibubujikwa na machozi kwenye mkutano wa NCCR kuomba msamaha, pamoja na baadaye kwenda mahakamani kupinga kufukuzwa uanachama wake ili asipoteze na ubunge wake wa jimbo la Kigoma kusini, Kafulila alimaliza tofauti zake ndani ya NCCR matatizo yakaisha.

December 2016, Kafulila akajitoa NCCR akajiunga na Chadema, akasema ameona ni vizuri upinzani uunganishe nguvu kwa wote kuwa pamoja.

November 2017, Kafulila akajitoa Chadema akajiunga na CCM akasema kwenye upinzani hakuna dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi.
 
David Kafulila amejiunga na CCM leo Mbweni jijini Dar na kukabidhiwa kadi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole. Hii inathibitisha na kuhitimisha mawazo ya wengi kua Bwana huyu alijitoa Chadema ili Kujiunga na CCM.
View attachment 637181
Polepole ameuita huu ni Usajili, ila navyojua anaesajiliwa lazima apewe chochote kitu. Nilidhani kua Biashara ya Ununuzi wa Binadamu ilishakufa enzi za Ukoloni, kumbe imerudi kwa jina jingine la "usajili".

Viva Tanzania ya Viwanda
Nyalandu mlimnunua kwa bei gani jombaa?
 
hongera zake ni haki yake, nasisitiza, kwa msisitizo, huyu mtu asibezwe, ana hoja za msingi, asikilizwe na hoja zake zifanyiwe kazi!.
Hili nimelizungumza hapa

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Paskali
Pacal hakuna hoja ya msingi ni njaa tu. wangelikuwa wabunge wa CDM wangelitoka? Pascal muda mwingine huwa unatoka nje ya weledi wako, quite astray! CCM ndiko kuna malaika? hakuna mafisadi CCM, hakuna wauaji CCM, hakuna wazinzi CCM, hakuna wachumia tumbo CCM, hakuna ndumila kuwili CCMM, CCM ni malaika? Pascal nadhani sometimes unafanya makusudi? Hao wote walikuwa wanainanga CCM, leo imekuwa safi?
Unadhani Magufuli asingelitangaza vyeo wangelikwenda? Akiacha kuwarubuni kwa fedha na vyeo unadhani watakwenda? akiacha kuwafuata kwenye biashara zao watakwenda?
 
Hawa wanasiasa sio WA kuwaamini they are only right the time of speech..wakimaliza wakashuka majukwaani wanakana walichosema..blive everybody ILA kuwa makini na mwanasiasa na wanawake..kafulila umwkwenda wanakoshughulikia mafisadi make sure andru chenge unarara nae mbele
 
hongera zake ni haki yake, nasisitiza, kwa msisitizo, huyu mtu asibezwe, ana hoja za msingi, asikilizwe na hoja zake zifanyiwe kazi!.
Hili nimelizungumza hapa

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Paskali
Mkuu Paskali natambua kua unajua na kufahamu historia na siasa za binadamu wa ulimwengu huu Wakorintho tunajua kuwa hoja ya ufisadi haijawahi kukifanya chama chochote cha siasa kushika dola kokote duniani chama hakishiki dola kwa hoja moja ya ufisadi isipokuwa kwa kuwa na ajenda ya maendeleo endelevu duniani kote mabadiliko ya kidola na kisiasa huchagizwa na kuporomoka kwa uchumi,ubaguzi wa kidini,kabila au rangi au kukandamizwa kwa haki za raia narudia tena hoja ya ufisadi ni hoja dhaifu sana ambayo kamwe haitokufanya kushika dola.

Unajua kwa nini vyama vya upinzani vilipokuwa vinajikita kwenye ajenda ya ufisadi havikuzuiliwa kufanya mikutano ya hadhara lakini kwa sababu sasa wameichana na hoja ile dhaifu wanazuiliwa hata kukutana ndani jibu ni moja tu hoja ya ufisadi haina nguvu ya kukufanya ushike dola kwa sababu 80% ufisadi uenda sambaba na ukuwaji wa uchumi na mzunguko mkubwa wa pesa hivyo hali ya maisha kwa wananchi wengi huwa Nzuri.
 
Ww ndio unajua Leo! Ununuzi wa watu ndo umepamba moto kwani umesahau Macho kumchuzi yy chapaa aliibatiza jina la kubadili gia angani
 
Back
Top Bottom