David Kafulila ajiunga rasmi na CCM huko Mbweni jijini Dar

David Kafulila ajiunga rasmi na CCM huko Mbweni jijini Dar

Sura za wote wawili i.e mpokelewa na mpokeaji, hazina ushirikiano na nafsi na mioyo yao. wote wawili wanaonesha kama hawaamini kama wanachokifanya ni sahihi, kwa wanaojua kuangalia sura mnaweza kuliona hili.
 
hongera zake ni haki yake, nasisitiza, kwa msisitizo, huyu mtu asibezwe, ana hoja za msingi, asikilizwe na hoja zake zifanyiwe kazi!.
Hili nimelizungumza hapa

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Paskali
Mkuu, Vyama vyote vina shida. Jiulize leo hii huko waenakohamia/hamishiwa hakuna wenye uwezo wa kupewa nafasi ila wao? Mfano Kitila/Mgwira na wengineo. unataka kuniambia jamaa alikosa kweli mtu ndani ya chama chake?
Kumbeza huyu kuna uhalali pia. Moja Ikumbukwe aliishitaki CCM kumuibia kura za ubunge, je, Mahakama ingempa ushindi angehama?
Pili, upinzania ni dhaifu kweli, sasa wanategemea nani auimarishe ikiwa wanaingia na kutoka? Mfano Bwana yuleee. oo safari ya upinzani kushika dola ni ndefu mnoo. Sasa alitegemea akihamia tu awe mwenyekiti/katibu wa chama?
Hapa tunapata picha hawa tunaowaona vijana wa kimapinduzi si lolote bali njaa tu zinawasumbua. hawana msimamo,hawana subira, hawawazi nje ya pale walipo na ni waoga wa maisha nje ya siasa.
 
Sura za wote wawili i.e mpokelewa na mpokeaji, hazina ushirikiano na nafsi na mioyo yao. wote wawili wanaonesha kama hawaamini kama wanachokifanya ni sahihi, kwa wanaojua kuangalia sura mnaweza kuliona hili.
Hiyo inaitwa "wacha wafu wazike wafu wao!!"
 
kafulila-jpg.637181

Halafu watu wanaapishana kienyeji tu mitaani, yaani kihuni huni tu, hivi sheria ya viapo inasemaje??
Nani anaeruhusiwa kisheria kumuapisha mwengine?
Na Kiapo hicho kinakua na impact gani??
 
Last few Years kafulila was a hero of a Nation, while Polepole alikua akipiga piga kelele mitaani tu,
Leo Kafulila katulia anaapishwa na "Boss wake" mpya ambae pengine ndie anaemuweka Mjini kwa hela za usajili alizomlipa.
Makarai mengine yanafaa kuwa uchafu, yaani unaapishwa na polepole?
 
aisee..hivi haoni aibu!!!!!
Swala si kuhama Chadema kuingia CCM, ila kuhama chama kimoja kwenda chengine. Sasa kwa nini aibu iwe kwa Kafulila tu, na siyo kwa Mrema, Sumaye, Lowassa, Msindai, Zitto, Wema, Mama yake Wema .........?
 
David Kafulila amejiunga na CCM leo Mbweni jijini Dar na kukabidhiwa kadi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole. Hii inathibitisha na kuhitimisha mawazo ya wengi kua Bwana huyu alijitoa Chadema ili Kujiunga na CCM.
Wenyewe wanajuana kwa mikia laki DAvida mkia wake uko kipande hilo asije akasahau
 
Swala si kuhama Chadema kuingia CCM, ila kuhama chama kimoja kwenda chengine. Sasa kwa nini aibu iwe kwa Kafulila tu, na siyo kwa Mrema, Sumaye, Lowassa, Msindai, Zitto, Wema, Mama yake Wema .........?
unajua kuna baadhi ya wanasiasa akihama kutoka upinzani kwenda ccm lazima ushangae
sio wapinzani wote wako sawa,wanatofautiana katika kuikosoa serikali na ccm,mfano nitashangaa mtu kama zitto,mnyika,lema,mbowe,lisu wakihamia ccm(nitasema hiv hivi..."hawaoni aibu!!!")
 
Mamluki wote warudi nyumbani. Sasa vyama vya upinzani viko safi, ni njia nyeupe kwenda ikulu.

Tanzania mpya naiona mita mbili toka guu langu.
 
hongera zake ni haki yake, nasisitiza, kwa msisitizo, huyu mtu asibezwe, ana hoja za msingi, asikilizwe na hoja zake zifanyiwe kazi!.
Hili nimelizungumza hapa

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Paskali
Sawa tumekusikia Njaa, kwa hiyo wenye hoja ni wanaohama kutoka upinzani kwenda ccm bali wanaokuja upinzani hawana hoja?! Kweli Mr Njaa sasa you have stooped too low, too low unatia kichefuchefu!
 
David Kafulila amejiunga na CCM leo Mbweni jijini Dar na kukabidhiwa kadi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole. Hii inathibitisha na kuhitimisha mawazo ya wengi kua Bwana huyu alijitoa Chadema ili Kujiunga na CCM.
View attachment 637181
Polepole ameuita huu ni Usajili, ila navyojua anaesajiliwa lazima apewe chochote kitu. Nilidhani kua Biashara ya Ununuzi wa Binadamu ilishakufa enzi za Ukoloni, kumbe imerudi kwa jina jingine la "usajili".

Viva Tanzania ya Viwanda
Waache wafu wawazike wafu wenzao
 
Back
Top Bottom