Daudi Mwakawago afariki Dunia

Status
Not open for further replies.

- Mkuu PM sawa sawa tena 100%, hiyo revenge mode ilianza siku nyingi na ndio waliomzungukia kwa Kimiti hao, anyways ngoja msiba utulie kwanza Mzee arudi tulipotokea ndio tuchambue pumba na mchele, inasikitisha sana!

Respect.

FMEs!
 

JF kwa data, I like the place!
 

- Sikonge hapa mkuu wangu umepiga msumari mzito sana, hawa ni wazee ambao wamelitumikia taifa with honors infact akiwa CCM boss alimuwajibisha hata mkuu wa kaya wa sasa, ndio maana walimfaulo sana mwishoni, lakini malipo hapa hapa duniani!

Respect.


FMEs!
 
Inasikitisha kuna watu bado wanaona ni sawa kwa viongozi kusafirishwa kwenda kutibiwa nje huku mamilioni ya Watanzania hawana hata Asprin.

Ni mawazo mufilisi kweli na aibu kwa taifa letu. Lini tutaelewa kwamba lazima tutengeneze vyetu kwanza kabla ya kukimbilia kwenye vya wenzetu?
 

- Mawazo mufilisi ni kuacha kuwapeleka nje kabla ya kutengenza vyetu kama unavyoshauri it is simply insane yaani kuacha kazi moja kabla ya kutafuta nyingine kwanza, ndio tabia za vijana wengi wabongo majuu siku hizi, sijui hili taifa tumelogwa na nani!

Respect.


FMEs!
 

Sometimes umuhimu wa mtu haujulikani hadi akiondoka duniani na hii ndio mifano yake. Mara nyingi watu wema hufa maskini lakini majitu majizi hufa wakasindikizwa na mali zao. Inasikitisha sana lakini sishangai kwani Tanzania imegeuka sasa kama Italy (i.e. mafia style leadership) kufanyiziana tu ndio maana waswahili wanasema fanya wema uende zako usingojee shukrani maana unaweza kuambulia matusi bure!!!
 

Ni mawazo gani muflis kumpeleke kiongozi mgonjwa nje kama Tanzania hawana tiba. Mbona nyerere, ,mwinyi na mawaziri wengineo wanaenda nje sembuse kumpeleka kiongozi aliyelitumikia taifa kwa uzalendo akatibiwe nje. Mh naona ndugu utawachafua watu humu JF rekebisha kauli yako mzee
 
- Wakuu wa New York City na vitongoji vyake ni kwamba kuna tunaojitayarisha kwenda Boston this weekend kuwafariji na kulia na watoto wa marehemu ambao baadhi yao wapo kule na ndiko msiba hasa hapa US ulipo, sasa kwa wanaotaka kwenda tuwasiliane jamani,

- Na habari nilizozipata hapa mjini kutoka kwa Mwalimu, ni kwamba Balozi wetu hapa UN, naye atakwenda huko mwisho huu wa wiki kuwaona wafiwa na tarehe 6 mwezi ujao kutakuwa na kumkumbuka marehemu nyumbani kwa balozi, kuanzia saa Nane mchana.

Mungu amlaze pema marehemu na awafariji wafiwa.

Ahsante.


William.
 
Mwanasiasa Mkongwe nchini Balozi Daudi Mwakawago amefariki dunia Jijini Dar e salaam.

Mwakawago alipata kushika nyadhifa mabli mbali za Kiasiasa nchini, Ubunge Iringa Mjini, Uwaziri, Balozi wa Kudumu UN

Ama hakika sisi ni wenye kurejea kwake Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amina
 
Jaribu kumwandikia Makamba uombe interview na JK...lol
 
Jaribu kumwandikia Makamba uombe interview na JK...lol
kwi!kwi!kwi!
Hawa viongozi wetu wa kwanza walikuwa class act. Hawa waliofuata ni utapeli tu.
Lakini naamini Tanzania bado kuna vichwa.
 
kwi!kwi!kwi!
Hawa viongozi wetu wa kwanza walikuwa class act. Hawa waliofuata ni utapeli tu.
Lakini naamini Tanzania bado kuna vichwa.

Ebana Jasusi...hiyo interview yako unayo kwenye audio? Kama unayo tuwekee basi hapa....
 
Poleni wafiwa wote. Nimesikia watamzika hapa Dar. Mzee mzito kama huyu wameshindwa kumzika Iringa kwa nini? Tunaifuta historia ya Nchi hii kwa kuwazika wazee kama hawa kwenye makaburi ya jumla hapa Dar ambayo baadaye yatakuja fukuliwa kuwapisha wawekezaji.
 

- Mkuu sasa hivi nimemuuliza mzito mmoja kuhusu hii hoja nzito sana, akaniambia kijana Dodoma kuna sehemu imetengwa kwa ajili ya maziko ya marais na viongozi wa juu wa taifa, lakini hakuna familia hata moja ya kiongozi wa taifa aliyewahi kufariki iliyowahi kuomba kuzika kwenye hilo eneo.

- Kwanini hakuzikwa Iringa, ni very complicated ishu ambayo katika hii hali ya msiba na bado hajazikwa sio polite kwenda hiyo avenue!

Respect.


FMEs!
 
Ebana Jasusi...hiyo interview yako unayo kwenye audio? Kama unayo tuwekee basi hapa....
Julius,'
Ninayo kwenye cassette. Nikishatulia nitaiweka kwenye cd. Lakini si mkisikia sauti yangu identity yangu itajulikana? kwi!kwi!kwi!
 
Julius,'
Ninayo kwenye cassette. Nikishatulia nitaiweka kwenye cd. Lakini si mkisikia sauti yangu identity yangu itajulikana? kwi!kwi!kwi!

Sauti yako si inajulikana na watu wanaokujua?Ama kuna watu wanaokujua lakini hutaki wajue kama ni wewe?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…