Dark days 17/03/20...

Hakuna kitu kama hicho, hayo mambo ya kujiongezea muda yalipigiwa chapuo na watu waliokuwa na agenda ya kumchafua ili aonekane alikuwa na tamaa ya madaraka lakini naamini asingeongeza hata sekunde moja ya utawala.

Nakuhusu third CEO waliomuondoa ni walewale ili kupunguza nguvu za kufuatilia nini kimetokea iwapo wangemuua na kumuacha mzee wa kusini. Kila aliyeonekana atakuwa kikwazo baadaye walihakikisha anaondoka hasa wenye madhara.
Mwamba mambo mengi sana alipandikiziwa ili aonekane hafai, ndiyo maana hata sasa udhaifu wa new CEO unafichwa kwa kumchafua JPM.

Ila tukiondoa madhaifu machache ya kibinadamu Magu alikuwa analipenda sana taifa lake, ila kwa kuwa watu wapo kazini kumchafua atachafuliwa sana mitandaoni lakini ukiutaka ukweli anasemwaje ingia uraiani ndiyo utajua nguvu ya mwamba.
Mkuu hizi ni hadithi tuu, wala hakuna mtu anajua ukweli, ila usitaje majina ya watu
 
Ni kweli huwezi kumuua rais kirahisi lakini kama system ikiamua kumpoteza ni dakika chache sana unasahaulika.
Upo sahihi lakini ukifuatilia wengi humu wanadai ni maadui zake yaani wapinzani, mabeberu, na kina Msoga gang!! Ndio maana nawaza kivipi mtu utoke nje ya system umuue Rais? Ni kitu hakiwezekani maana wanalindwa kiroho na kimwili yaani hata ukija na uchawi wa aina Gani utadakwa tu kwa dark arts.

Na kama kweli system ingemuua issue ingevuja mapema vile? Kiasi media za Kenya zifahamu na hata waTanzania walio nje kama Lissu na Jasusi wa uskochi kufahamu?
 
Kwa hiyo was it a natural death?
 
Hatari.... huu uzi huu huyu mtu kama mimi tu anayoyajua km nayoyajua hizi code bora msiwe mnajua mazee mtakufa siku sio zenu ndo maana huwa naskia hasira napost nyuzi kwa kupanick ni haya madude ya huko duniani...najuta kwanini niliingizwa kwenye mfumo
Usiwe na hasira sana tengeneza mikakat na vijana wachache sana wasio zid 5 muwe imara kwel kwel af muanze kuufukunyua uo mfumo silent had wabak wanajiuliza ninani uyu walambe mchanga inav takiwa ili sstem iwe salama

Au ni vbaya.
 
Mbona JPM alipelekwa JKCI kabla ya Mzena kamuulize dokta yoyote pale JKCI sababu ya JPM kufariki ni Nini, mbona inafahamika randomly tu kuwa alikua na shida ya moyo na alikua na pacemaker. Sasa why mtu wa hivyo ionekane kauwawa wakati wote mnafahamu alikua na matatizo ya afya? Kampeni tu alishindwa kufanya tukawa tunasema Rais hayupo fiti hamkuona ajabu ila miezi 7 baadae ndio kauwawa?? Hampo serious.
Kuwa na shida flani ya kiafya kunazuia mtu kuuwawa?

Tena hiyo inaweza kutumika kama uchochoro katika kutekeleza dhamira yao.

Silent killers hutumia mbinu hizo.
 
Mnaoamini hii propaganda huwa nawashangaa sana, yaani mtu akatae umeme Ili auze majenereta? Hivi hao mafisadi si ndio wanamiliki viwanda vikubwa eti kweli akate umeme uathiri uzalishaji wa mabilioni kwa ajili ya kuuza majenereta ya million kadhaa?

Duh no wonder ulikua mfuasi wa Jiwe, brainwashed mindset!
Sidhani kama uko sawa!

Simply kabisa, umeme ukikatika lazima generator zinunuliwe. Na watu wanajua aliyepo nyuma ya hiyo biashara.

Kwani hukusikia mkanganyiko kuhusu mabwawa ya maji kukauka?

Hata hivyo hiyo ni road way kuelekea kulibinafsisha shirika.

Hao unaodai wanamiki viwanda vikubwa ndo watalimiliki pindi likibinafsishwa.

Yaweza kuwa unamchukia Magufuli ila sasa umepitiliza.
 
Kuwa na shida flani ya kiafya kunazuia mtu kuuwawa?

Tena hiyo inaweza kutumika kama uchochoro katika kutekeleza dhamira yao.

Silent killers hutumia mbinu hizo.
Why umuue wakati angekufa irrespective? Aliwahi kuanguka Zanzibar huko nyuma Hadi watu wakazusha amefariki. Huko kusini Nako alidondoka akapotea kama wiki 2 Nako wakazusha amefariki.... So sio mara ya kwanza, tokea 2017 mashine ilikua na hitilafu hata akazuiwa asisafiri masafa marefu na ndege.

So kama Kuna mtu anadhani ameuwawa basi atuambie why mara zote hizo alikua anadondoka wasiseme ni sumu ila 2021 ndio sumu??
 
Simply kabisa, umeme ukikatika lazima generator zinunuliwe. Na watu wanajua aliyepo nyuma ya hiyo biashara.
Mkuu wewe ni mtu makini kabla ya kuamini kitu basi utafute taarifa kamili.
1. Umeme wa nchi hii kwa zaidi ya 60% unazalishwa kwa gesi, hayo Maji ni 30%+ pekee.
2. Ukihujumu gesi Ina maana Tanzania nzima itaenda gizani.
3. Sasa kama ni kuuza majenereta why wahujumu 30% ila wasihujumu 60+%?
4. Kingine umedai umeme ukikatika watauza jenereta? Sasa twende taratibu.
5. Kwa siku mahitaji ya umeme wa viwanda ni makubwa na tukubali tu wenye mamlaka ndio wanamiliki viwanda vikubwa. Sasa hasara ya umeme kukatika kwa kiwanda ni kubwa sana je utaifidia kwa kuuza majenereta mangapi?

Ningeona mnamaanisha kama mngesema wanahujumu Maji Ili wapewe Hela ya maintenance au wauze umeme wa dharura ila kitendo Cha kusema majenereta ni kituko Cha Karne. Ni sawa na mtu atengeneze corona Ili auze sanitizer na Barakoa za buku buku!! Ndio Nini Sasa?
 
Kwani hukusikia mkanganyiko kuhusu mabwawa ya maji kukauka?
Mkanganyiko upi? Huyo kikwete mnanyemshutumu ndio aliachana na umeme wa Maji na kutupeleka kwenye gesi Ili hata mabwawa yakikauka tusikose umeme. Cha kushangaza ndio huyo huyo mnadai anahujumu TANESCO? Kwanini atengeneze gesi ambayo anajua itakua suluhu ya umeme?

Tupunguze propaganda za Facebook, hii ni jamii forums tujaribu ku reason kama watu tunaojitambua. Mtu mzima kuamini unaweza risk kukata umeme wa matrillion kwa ajili ya kuuza generator la million 5 ni utoto wa ajabu sana.
 
Kama ilitokea kwa JF Kennedy na kwa Yitzhak Rabin pamoja na ukubwa wa mataifa yao, ingeshindikana kwa Magufuli?
Sasa hao waliuwawa na system humu ndani wanasema ameuwawa na wapinzani and CEO wa zamani!!! Ndio tujiulize hivi mtu uliye nje ya system unaweza muua aliyemo ndani ya system more so, Rais? More so kwa sumu ya Polonium? Hivi mnajua ulinzi wa Rais kweli? Yaani hata ukiwaza tu kummaliza Kuna exorcists wanasoma akili Yako popote ulipo!! Kingine JPM alitumia narrow management yaani anaserikali ndani ya serikali so kwa style hiyo huwezi panga kitu asijue. Hushangai voicenote za kina Membe na January zilivuja? Ina maana hata ndani Yao alikua na mole.

It's not easy kumuua Rais, Nyerere alikua na maadui kuliko JPM ila hakuuwawa. Same to Moi au Kagame wote walikua na Wana maadui wengi mnoo ila hawakuuwawa. Ni ngumu mnoo maana ulinzi wake ni wa kiroho zaidi na kimwili kidogo sana.
 
1. Umeme wa nchi hii kwa zaidi ya 60% unazalishwa kwa gesi, hayo Maji ni 30%+ pekee.
2. Ukihujumu gesi Ina maana Tanzania nzima itaenda gizani.
3. Sasa kama ni kuuza majenereta why wahujumu 30% ila wasihujumu 60+%?
Anyways, hapa tunaenda na ushahidi wa kimazingira... taarifa za ndani hatuna access nazo na hata tukizipata sio rahisi kuziweka hapa kwa sababu mtambuka .

Maana hapa itabidi ujue walioko nyuma ya hiyo 60% na nguvu, vivyo hivyo kwa hao tunaosema ni wamiliki wakubwa wa viwanda.
4. Kingine umedai umeme ukikatika watauza jenereta? Sasa twende taratibu.
5. Kwa siku mahitaji ya umeme wa viwanda ni makubwa na tukubali tu wenye mamlaka ndio wanamiliki viwanda vikubwa. Sasa hasara ya umeme kukatika kwa kiwanda ni kubwa sana je utaifidia kwa kuuza majenereta mangapi?
Kuna utaratibu wa kumfidia mwenye kiwanda iwapo umeme utakatika?
Hata ingekuwa hivyo, anayekata umeme anakuja na sababu ambazo inakuwa ngumu kumtia hatiani.
Ningeona mnamaanisha kama mngesema wanahujumu Maji Ili wapewe Hela ya maintenance au wauze umeme wa dharura ila kitendo Cha kusema majenereta ni kituko Cha Karne. Ni sawa na mtu atengeneze corona Ili auze sanitizer na Barakoa za buku buku!! Ndio Nini Sasa?
Kuuza majenereta ni moja tu ya faida, ila zipo nyingine. Sababu kuu nimeitaja katika post iliyopita
 
Mbona JPM alipelekwa JKCI kabla ya Mzena kamuulize dokta yoyote pale JKCI sababu ya JPM kufariki ni Nini, mbona inafahamika randomly tu kuwa alikua na shida ya moyo na alikua na pacemaker. Sasa why mtu wa hivyo ionekane kauwawa wakati wote mnafahamu alikua na matatizo ya afya? Kampeni tu alishindwa kufanya tukawa tunasema Rais hayupo fiti hamkuona ajabu ila miezi 7 baadae ndio kauwawa?? Hampo serious.

Kingine sio serikali tu media za Kenya zilishaanza kuhoji afya ya JPM kipindi ambacho huku Tanzania hata serikali ilikua kimya. Media zilisema ka paralyse upande mmoja n.k hakuna rumour yoyote iloyosema kapigwa sumu au kauwawa zote zilionyesha ni tatizo la moyo. Kumbuka muda huo Tanzania wafuasi wa JPM mlikua busy kutukana wapinzani kwa kuhoji afya ya JPM. Cha kuchekesha amekufa ndio mmekua wakali kuhusu kifo chake??

Huwezi kumuua Rais kirahisi hivyo, especially kwa JPM aliyekua anajihami kiasi kile.

Whatever the reason for his death, he was supposed to die
 
Mkanganyiko upi? Huyo kikwete mnanyemshutumu ndio aliachana na umeme wa Maji na kutupeleka kwenye gesi Ili hata mabwawa yakikauka tusikose umeme. Cha kushangaza ndio huyo huyo mnadai anahujumu TANESCO? Kwanini atengeneze gesi ambayo anajua itakua suluhu ya umeme?
Kwanza hakuna mahali nimemtaja Kikwete mkuu, muache mwamba ale mafao yake.

Pili, sipendi kuingia deep kuhusu suala la gesi ila ninachojua ni kuwa liliwahi kunisikitisha sana... hivyo tuliache kama lilivyo.

Kuhusu Facebook kama ilivyo JF watoa maudhui ni walewale.
Hivyo sio kila kilichopo FB ni cha uongo na sio kilichopo JF ni cha ukweli , ni wajibu wa mtumiaji kuchuja kila taarifa anayolishwa.

Hivyo sioni sababu ya kuikasirikia Facebook.
 
Anyways, hapa tunaenda na ushahidi wa kimazingira... taarifa za ndani hatuna access nazo na hata tukizipata sio rahisi kuziweka hapa kwa sababu mtambuka .

Maana hapa itabidi ujue walioko nyuma ya hiyo 60% na nguvu, vivyo hivyo kwa hao tunaosema ni wamiliki wakubwa wa viwanda.
Hapana hakuna Siri, hiko nachosema unaweza hata google tu ni public knowledge kabisa kwamba 60+% ni umeme wa gesi. Kama kweli wanataka kuhujumu basi natarajia wangetoboa Bomba maana mpaka uliunge ni mamilion yanatumika na itachukua hata wiki kadhaa mgao nchi nzima. So hakuna logic katika madai haya.

Kuna utaratibu wa kumfidia mwenye kiwanda iwapo umeme utakatika?
Hata ingekuwa hivyo, anayekata umeme anakuja na sababu ambazo inakuwa ngumu kumtia hatiani
Hapana umesema hizo cartel ndio zinataka kuifilisi TANESCO Ili ibinafsishwe. Ndio nasema Sasa Cartel ziko tayari viwanda vyao vife ilimradi tu mtu Fulani auze jenereta? Kwanza waTanzania wangapi Wana jenereta kama sio hao hao cartels peke Yao? Mtaa naokaa sijawahi ona jenereta kabisa Sasa hao wateja wa majenereta ni kina nani kiasi biashara iwe na faida kuzidi viwanda!!
Kuuza majenereta ni moja tu ya faida, ila zipo nyingine. Sababu kuu nimeitaja katika post iliyopita
Sababu kuu ni kubinafsisha TANESCO right? Sasa hata Maji yakidorora ila TANESCO inategemea gesi kwa Sasa. Kwa hiyo kuhujumu mabwawa hakuipunguzii chochote TANESCO unless siku wahujumu gesi. Ni sawa na kusema Simba inahujumiwa na TFF sababu tu wachezaji wake walio benchi wamepewa kadi nyekundu mfululizo. Yaani usimpe red card Chama au Baleke alafu unasema umehujumu timu? Kweli inaingia akilini mkuu?
 
Pili, sipendi kuingia deep kuhusu suala la gesi ila ninachojua ni kuwa liliwahi kunisikitisha sana... hivyo tuliache kama lilivyo.
Ni kweli Kuna ufisadi mwingi ila ndio Roho ya umeme wa Tanzania. So kutohujumu gesi alafu ukahujumu mabwawa basi jua ni sawa na kusukuma tembo kwa kidole.
Kwanza hakuna mahali nimemtaja Kikwete mkuu, muache mwamba ale mafao yake.
Ndio narrative ya Uzi huu mzima kuwa huyo OLD CEO ndio amemuua the Late CEO sababu alizuia Dili zake. Na comments humu ni kupitia logic hiyo hiyo. Ndio Sasa nashangaa kivipi anyeshutumiwa kuhujumu Maji Ili auze majenereta ndio kaleta umeme wa gesi ambao ndio tegemeo?? Hivi unaweza hujumu kitu alafu ukaleta tiba mbadala? Si inakua kazi sifuri.

Hakuna Rais au kiuongozi mkubwa wa serikali anayeuwawa na watu wa nje ya system.
Huu ndio ukweli unfortunately humu ndani story ni kuwa mtu aliye nje ya system ndio alimuua aliye ndani ya system.
 
Back
Top Bottom