Darassa anajua sana kufanya interview na yuko focused

Darasa namkubali ila ameonyesha udhaifu alipoulizwa anamkubali msanii gani akajitaja mwenyewe means hakubali kazi za wenzie.

Pili naomba kuuliza hivi salama ana mwanaume? Ameolewa? Ameshawahi kuzaa?
 
Darasa namkubali ila ameonyesha udhaifu alipoulizwa anamkubali msanii gani akajitaja mwenyewe means hakubali kazi za wenzie.

Pili naomba kuuliza hivi salama ana mwanaume? Ameolewa? Ameshawahi kuzaa?
Yupo sahihi kabisaaa, hata Vanessa aliwahi kuulizwa akajitaja mwenyewe. Yeye n msanii lazma ajitaje anajikubali yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Darasa namkubali ila ameonyesha udhaifu alipoulizwa anamkubali msanii gani akajitaja mwenyewe means hakubali kazi za wenzie.
ila yupo poa sana
anakwambia hana cha kuongea kwahiyo anasalimia tuu then anakaa kusiliza mpk mweyeji wake afike, haha hana wenge
 
Darasa namkubali ila ameonyesha udhaifu alipoulizwa anamkubali msanii gani akajitaja mwenyewe means hakubali kazi za wenzie.

Pili naomba kuuliza hivi salama ana mwanaume? Ameolewa? Ameshawahi kuzaa?
Binafsi alipojibu hilo swali nilimuelewa sana..Kwanza alisema kwa Mziki anaofanya na Changamoto alizopitia ana kila sababu ya kusema Darasa ni bora..

Nakumbuka hapa aliwataja hadi Master J, Majani, na Ruge.. Na akaeleza namna gani alipata ugumu kuonana na hawa watu..

Niseme tu.. Darasa acheni ajiite Darasa.. ile interview ya jana inabaki kuwa bora kwangu.. Mwingine ninaye msubiria ni Dogo janja na Dimpoz. Nao wanajua kujieleza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nilibahatika kusikiliza interview ya Darassa aliyofanyiwa na Salama Jabir. Kwanza nikiri Salama ni bingwa wa kufanya interview maana interview zake utasikia vitu ambavyo hukuwahi kusikia wakati mhusika alipokuwa akifanyiwa interview na watu wengine.

Katika hiyo interview alimuuliza maswali Darassa ambayo yaliwezesha watazamaji kujua hustles zake na historia yake, pia alliweza kuclear allegations zilizoibuka kipindi alipoacha kufanya show wala kutokea kwenye social media na vyombo vya habari na watu wakasema amekuwa teja anabwia unga.

Jamaa anadai alikuwa anatengeneza pesa mabyo hakuwa anaipata waliikuwa wanakula wengine yeye anaambulia kidogo. Akaona kwanini aendelee kufanya kitu ambacho hakifurahii wala hakimfaidisha maana hawezi kuwa kwenye peak daima ipo siku atashuka na anaweza kuwa vile vile wakati kapiga show nyingi.

Akaamua kwanza a quit mziki na kupiga show kwa muda ajifunze jinsi ya kumanage biashara ya mziki ndipo arudi kufanya mziki. Pia akasema kipindi hicho mpenzi wake wa miaka 9 alikuwa mjamzito hivyo alichukua muda huo kulea mimba hadi mtoto anazaliwa na malezi ya mwanae.

Kaongelea hustles zake kuwa yeye katika hustles zake alikuwa anakutana na wasanii waliokuwa wana hit that time lakini hakuwahi kuomba msaada wa kuelekwa studio au chochote yeye tu alikuwa anaenda maskani yao wasikiliza tu zile story zao zilikuwa zinamuinspire ila ye hakuwa mtu wa kuzungumza wala kuomba asaidiwe yeye alikuwa anafuata motivation alipokuwa akisikia wanapiga story zao.

Akasema mfano Mwana F.A ndo msanii wa kwanza kuwa na namba yake alikuwa anamtafuta wanakutana wanazungumza na Mwana F.A alitegemea labda jamaa atamuomba support yoyote ila walipokuwa wakimaliza anamuaga anaondoka na hakuwa muomba wala msaada wa kupelekwa studio.

Jamaa kaongea mengi ya kujifunza likiwemo watu wanaosaidiwa kujua nafasi yao, mfano kasema yeye kalelewa na dada yake ambaye tayari ni marehemu, Anasema kitendo cha mtu kukukaribisha kwake wakati ana familia yake halafu akanunua nguo mpya ya mwanae ya zamani akakua wewe hiyo kwake ni bonge la love maana kajinyima hawez afford wapa nyote nguo mpya ila watu uwa wanasahau nafasi waliopewa wanaanza kulalamika.

Kamowngelea pia baba yake kuwa hakuwa naye wakati anakua ila hamlaumu ana mrespect ila siyo mshikaji wake yani hana ushikaji na mzee wake wa hivyo na hilo ndilo linamfanya asitake tengana na huyo dada aliyezaa naye kwasababu ya family aliyoyapitia amegundua kuwa family ikivunjka watoto wanateseka.

Jamaa anajua kujieleza na yuko focused kuliko nilivyo waza japo kakiri hakumaliza shule na wala halaumu mtu kwa hilo maana yalikuwa nje ya uwezo wa waliokuwa wanamsmesha
Jana hiyohiyo nikasikiliza interview ya Ali kiba, akijibu swali mpaka amaliza unakuwa umeshasahau swali lilikuwa linahusu nn.
 
We unafikiri mtu hadi anaitwa Darasa ni mchezo mchezo?
Kuna wengine dakika ya pili ya mahojiano anaanza kupaniki na vingereza mdiliko vya yu noo mi ai noo yu.
Tupa jiti hiyo ni ganja tu mwamba, Darasa bila elimu mambo ni bampa to bampa/

Hiyo verse kaichora unju

Btw nikki kwenye interview yuko vizuri sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom