Darassa anajua sana kufanya interview na yuko focused

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,027
Jana nilibahatika kusikiliza interview ya Darassa aliyofanyiwa na Salama Jabir. Kwanza nikiri Salama ni bingwa wa kufanya interview maana interview zake utasikia vitu ambavyo hukuwahi kusikia wakati mhusika alipokuwa akifanyiwa interview na watu wengine.

Katika hiyo interview alimuuliza maswali Darassa ambayo yaliwezesha watazamaji kujua hustles zake na historia yake, pia alliweza kuclear allegations zilizoibuka kipindi alipoacha kufanya show wala kutokea kwenye social media na vyombo vya habari na watu wakasema amekuwa teja anabwia unga.

Jamaa anadai alikuwa anatengeneza pesa mabyo hakuwa anaipata waliikuwa wanakula wengine yeye anaambulia kidogo. Akaona kwanini aendelee kufanya kitu ambacho hakifurahii wala hakimfaidisha maana hawezi kuwa kwenye peak daima ipo siku atashuka na anaweza kuwa vile vile wakati kapiga show nyingi.

Akaamua kwanza a quit mziki na kupiga show kwa muda ajifunze jinsi ya kumanage biashara ya mziki ndipo arudi kufanya mziki. Pia akasema kipindi hicho mpenzi wake wa miaka 9 alikuwa mjamzito hivyo alichukua muda huo kulea mimba hadi mtoto anazaliwa na malezi ya mwanae.

Kaongelea hustles zake kuwa yeye katika hustles zake alikuwa anakutana na wasanii waliokuwa wana hit that time lakini hakuwahi kuomba msaada wa kuelekwa studio au chochote yeye tu alikuwa anaenda maskani yao wasikiliza tu zile story zao zilikuwa zinamuinspire ila ye hakuwa mtu wa kuzungumza wala kuomba asaidiwe yeye alikuwa anafuata motivation alipokuwa akisikia wanapiga story zao.

Akasema mfano Mwana F.A ndo msanii wa kwanza kuwa na namba yake alikuwa anamtafuta wanakutana wanazungumza na Mwana F.A alitegemea labda jamaa atamuomba support yoyote ila walipokuwa wakimaliza anamuaga anaondoka na hakuwa muomba wala msaada wa kupelekwa studio.

Jamaa kaongea mengi ya kujifunza likiwemo watu wanaosaidiwa kujua nafasi yao, mfano kasema yeye kalelewa na dada yake ambaye tayari ni marehemu, Anasema kitendo cha mtu kukukaribisha kwake wakati ana familia yake halafu akanunua nguo mpya ya mwanae ya zamani akakua wewe hiyo kwake ni bonge la love maana kajinyima hawez afford wapa nyote nguo mpya ila watu uwa wanasahau nafasi waliopewa wanaanza kulalamika.

Kamowngelea pia baba yake kuwa hakuwa naye wakati anakua ila hamlaumu ana mrespect ila siyo mshikaji wake yani hana ushikaji na mzee wake wa hivyo na hilo ndilo linamfanya asitake tengana na huyo dada aliyezaa naye kwasababu ya family aliyoyapitia amegundua kuwa family ikivunjka watoto wanateseka.

Jamaa anajua kujieleza na yuko focused kuliko nilivyo waza japo kakiri hakumaliza shule na wala halaumu mtu kwa hilo maana yalikuwa nje ya uwezo wa waliokuwa wanamsmesha
 
Salama Jabir ni gifted and talented sijaona mtu wa kumkuta huyo bibie katika kumfanyia mtu interview hapa bongo.

Natamani apanue wigo na upande wa Siasa na Biashara pia ahoji Moguls na Politicians mimi sio fan kiivo wa entertainment ila huyo dada namfatilia sana
 
Nafaka upo vizuri katika uhandishi wa habari. Ebu tumia kipaji chako iki.

Pili, Darasa ni mmoja ya best musician waliowahi kutokea Tanzania. Alipotea ila naona anaanza kurudi. Yote 9 kumi jamaa akubali kwamba alitumia Poda.
Yeye alisema hakuwa anatumia poda alikuwa anafanya mambo yake na anajifanya jinsi ya kumanage mziki wake. Anasema alikuwa akilea mimba na anadai mpaka mkewe anajifungua zile hustle na usumbufu wa mtoto since day one alikuwa naye bega kwa bega anaishi naye. Pia akasema hadi F.A alimfuata nyumbani baada ya kusikia jamaa eti anatumia poda, alimkuta anaendela na maisha yake hadi akashangaa na akamuuliza kwanini hajitokezi kupinga hizo allegation?

Darasa anadai alimwambia kwamba haina haja ya kupingana na uzushi kwakuwa yeye yupo na hatumii hizo mambo. Na akasema hata akijitokeza akawambia watu sababu za kutokuwa kwenye mziki kwa wakati huo, huenda hawatomuelewa wataziona ni za kipuuzi wakati yeye kwake ni za msingi.

Pia anadai yeye si mtu wa kutoka ni either yuko studio au nyumbani ni nadra sana kumkuta viwanjani.
 
Kwanza Uzuri wa Salama akikuhoji anakupa nafasi ya kujieleza hakukatishi pia maswali yake yapo direct na haya uchochezi muhojiwa unajikuta tu umeshafunguka vitu kwa usahihi na utulivu.

Salama Jabir ndo king wa interview hapa bonge yeye anaweza hoji mwana siasa anawezamuhoji mtu yeyote bila kuona upungufu kwa sababu kwanza ana data nyingi na anafanya research kabla hajauliza.

Niliangalia interview ya John Heche wakati anahojiwa na Zembwele kioindi cha Goodmorning kiukweli yule Mzee hamna kitu maswali hata anavyouliza uswahili uswahili mwingi anaingilia sana maongezi na fujo zisizokua na maana hata kipindi kile cha asubuhi Salma Dakota aliwahi mwambia atulie sio anataka kuongea yeye tu bila kusikilizana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza Uzuri wa Salama akikuhoji anakupa nafasi ya kujieleza hakukatishi pia maswali yake yapo direct na haya uchochezi muhojiwa unajikuta tu umeshafunguka vitu kwa usahihi na utulivu..


Salama Jabir ndo king wa interview hapa bonge yeye anaweza hoji mwana siasa anawezamuhoji mtu yeyote bila kuona upungufu kwa sababu kwanza ana data nyingi na anafanya research kabla hajauliza.

Niliangalia interview ya John Heche wakati anahojiwa na Zembwele kioindi cha Goodmorning kiukweli yule Mzee hamna kitu maswali hata anavyouliza uswahili uswahili mwingi anaingilia sana maongezi na fujo zisizokua na maana hata kipindi kile cha asubuhi Salma Dakota aliwahi mwambia atulie sio anataka kuongea yeye tu bila kusikilizana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee sijawahi mkubari Zembwela ila salama ni King wa interview.
 
Salama Jabir ni gifted and talented sijaona mtu wa kumkuta huyo bibie katika kumfanyia mtu interview hapa bongo, Natamani apanue wigo na upande wa Siasa na Biashara pia ahoji Moguls na Politicians mimi sio fan kiivo wa entertainment ila huyo dada namfatilia sana
Angalau Lil Ommy angekuwa kwenye level za salama ila jamaa unyamwezi mwingi twingereza twa hapa na pale ndo huwa zinaharibu interview zake.

Ila kwa kweli salama ni mtulivu sana kwenye mahojiano.
 

Similar Discussions

22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom