Darasa la Sheria la Wakili Peter Madeleka

Darasa la Sheria la Wakili Peter Madeleka

Mfuatilie, maana hata kesi nyingi kampuni yake ya stalwart law chambers inazochukua, ni kesi ambazo jamhuri huwa ina maslahi kwenye hizo kesi...na siku zote Madeleka huangukia pua!

Kijana wa nyumba kubwa huyu...
Kijana wa nyumba kubwa huyu... Alikuwa police akaacha akaenda kusoma sheria.. Bado ana vinasaba...!
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeruhusu dhamana ya Wakili Peter Madeleka, ingawa linaendelea kumshikilia Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kwa maelekezo ya kumpeleka wenyewe nyumbani kwake kabla ya saa sita usiku wa leo.

Akizungumza na Sasa Live leo Agosti 17, 2026, Wakili Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), ameeleza kuwa taratibu zote za dhamana zilikamilika majira ya saa nane mchana mbele ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (ZCO), lakini polisi wameweka utaratibu tofauti wa kumwachia.

Kisabo amebainisha kuwa pamoja na kukamilisha masharti ya wadhamini watatu akiwemo yeye na ndugu wawili wa Madeleka polisi wamekataa kumkabidhi mtuhumiwa mikononi mwao na badala yake wakaahidi kumfikisha nyumbani kwake kwa carriages za jeshi hilo, bila kutoa sababu rasmi za kipekuzi au kisheria.

"Kisheria mtuhumiwa akipewa dhamana anatakiwa kuachiwa huru mara moja aendelee na majukumu yake. Wametupa masharti ya wadhamini watatu tukasaini, lakini wanasema watampeleka wenyewe nyumbani kwake kabla ya saa sita usiku. Hii ina maana bado anashikiliwa na Polisi kinyume na utaratibu," amesema Kisabo.

Jitihada za Sasa Live kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi au Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ili kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu huo zinaendelea, kwani simu zao hazikuweza kupatikana mara moja kabla ya kuchapishwa kwa habari hii.

#SasaLive #PeterMadeleka #PaulKisabo #THRDC #JeshiLaPolisi HakiNaSheria DarEsSalaam TanzaniaNews
 
Wakili , Peter Madeleka, amerejea uraiani na yupo huru mara baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumwachia bila masharti yoyote jioni hii ya Agosti 17,2026.

Mapema leo Agosti 17, 2026, akizungumza na Sasa Live, Wakili Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), alieleza kuwa taratibu za dhamana zilikamilika majira ya saa nane mchana mbele ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (ZCO), lakini polisi walipanga kumpeleka wenyewe nyumbani kwake kabla ya kumwachia kikamilifu.

Taarifa za hivi punde zilizotufikia zinaripoti kuwa Madeleka ameachiwa huru moja kwa moja bila kuwekewa sharti au takwa lolote la kisheria kwa sasa.

Jitihada za Sasa Live kumtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi au Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu jalada la shauri hilo zinaendelea, na taarifa zaidi tutawaletea.

#SasaLive #PeterMadeleka #PaulKisabo #THRDC #JeshiLaPolisi HakiNaSheria DarEsSalaam TanzaniaNews
1786982481895.jpg
 
Masaa chache baada ya kuonja tena hewa ya uraiani, Wakili Peter Madeleka, ameavunja ukimya na kuwashukuru Watanzania waliopaza sauti kupinga kile alichokiita "ukandamizaji" dhidi yake.

Akitumia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X leo Agosti 18, 2026, Madeleka ametoa ujumbe huo mzito kufuatia kuachiwa kwa dhamana jana Agosti 17, baada ya kusugua benchi la mahabusu kwa siku tatu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) Dar es Salaam.

Katika maandishi yake yaliyowatag viongozi na wanaharakati nguli wakiwemo John Heche (CHADEMA), Boniface Mwabukusi (TLS), Maria Sarungi, na viongozi wa ACT Wazalendo, Madeleka ametupa kombora la shukrani:

"NAWASHUKURU watanzania wote WALIOPAZA SAUTI ZAO na KULAANI aina zote za UKANDAMIZAJI dhidi yangu. MUNGU awabariki sana. Ingawa siwezi KUWATAJA WOTE hapa, NATAMBUA na KUTHAMINI upendo wenu," ameandika Madeleka.

Mchakato wa kupewa dhamana hiyo uliratibiwa na kuthibishwa na Wakili Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Kukamatwa kwa Madeleka kuliibua mjadala mzito tangu Agosti 14, 2026, aliponaswa na polisi katika viunga vya Mahakama ya Uhujumu Uchumi (Mikocheni B).

Jeshi la Polisi lilimshikilia kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuutuhuma zilizojiri saa chache tu baada ya kutangaza mpango wa kupinga kisheria zuio la mawakili kuhojiwa na wanahabari maeneo ya mahakama.

#SasaLive #PeterMadeleka #PaulKisabo #THRDC #TLS CHADEMA ACTWazalendo HakiNaSheria .DarEsSalaam
1787035283716.jpg
 
Wakili Peter Madeleka amekamatwa na polisi leo, Agosti 20, 2026, alipokwenda kuripoti katika Ofisi ya ZCO kama alivyotakiwa baada ya kuachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa Wakili Gideon Mathew, Madeleka alifika katika ofisi hiyo kwa ajili ya kutekeleza sharti la dhamana, lakini badala yake alikamatwa na baadaye kupelekwa katika Mahakama ya Kisutu.

“Juzi Wakili Peter Madeleka alipoachiwa kwa dhamana, alitakiwa kwenda kuripoti Ofisi ya ZCO leo. Sasa baada ya kufika amekamatwa na kupelekwa Mahakamani Kisutu muda huu,” amesema Wakili Mathew.

Ameongeza kuwa wakati huo alikuwa pamoja na Madeleka pamoja na Wakili William Maduhu katika Mahakama ya Kisutu, ambako walikuwa wakifuatilia kinachoendelea.

Taarifa zaidi kuhusu sababu za kukamatwa kwake na hatua zinazofuata katika kesi hiyo zinatarajiwa kutolewa baada ya taratibu za mahakama kukamilika.
 
Back
Top Bottom