Somo la pili, sehemu ya nne (Lesson two part four).
Karibu tena leo twendelee kuelimika, katika sehemu ya nne tutaenda kujifunza kitu kinachoitwa;
FANYA MAAMUZI SAHIHI NA SIYO MAAMUZI YA KUPENDEZA.
kuna misingi miwili msingi wa KUPENDA na msingi wa KUWEZA. Maamuzi yanayotokana na msingi wa KUWEZA huwa ni SAHIHI lakini maamuzi yanayochipukia kwenye msingi wa KUPENDA huwa 90% si sahihi na wanadarasa wengi wako hapa na huu ndo msingi unaokuwa wa kupendeza matokeo yake mwanadarasa anaenda kaskazini huku mafanikio yakienda kusini.
Moja ya kosa kubwa ambalo wanadarasa walio wengi hulifanya ni kushindwa kutofautisha maneno haya mawili KUPENDA na KUWEZA katika kuwaongoza kufanya maamuzi juu ya shughuli gani watakayoifanya itakayowaingizia kipato. Ni 10% tu ya watu ambao hufanikiwa kwa kuanza na msingi wa maamuzi wa KUPENDA kwa maana nyingine ni 10% tu ya wale wanaofanya shughuli fulani kwasababu wanaipenda na wakajikuta ndiyo shughuli haswa wanayoiweza lakini 90% ya watu hawafanikiwi kwasababu licha ya KUPENDA kwao huwa hawawezi.
Lakini watu wanaofanya shughuli fulani ya kuwaingizia kipato kwa kufuata msingi wa maamuzi wa KUWEZA ni 80% wanaofanikiwa pasipo kujalisha kama hicho kitu walikuwa wanakipenda au laah.
Kwanini 80% hii ni kwasababu KUPENDA na KUWEZA ni maneno ambayo yamezaliwa kutoka katika nyanja mbili tofauti, tukianza na KUWEZA hili limetokana na chimbuko la uumbaji au uweza aliopewa binadamu ndani yake na ni tofauti na aliopewa binadamu mwingine, lakini neno KUPENDA linatoka katika nyanja ya HISIA hivyo ni kitu kinachoweza kujengwa au kubomolewa wakati wowote.
Baada ya watu kuanza kufanya shughuli fulani kwa maamuzi ya KUWEZA huwa wanaanza na kutokuipenda hiyo shughuli lakini kwasababu KUPENDA ni kitu cha HISIA huanza kujijenga na kisha mtu huanza kuipenda hiyo shughuli, tofauti na aliyeanza KUPENDA hataweza kufanikiwa kwasababu kuweza hakuji njiani sio kitu cha hisia bali ni kitu cha uweza Hivyo huyo mtu hatafanikiwa kwasababu ataishia kuiga jinsi ya kukifanya kitu hicho kwa kuwa hana uwezo nacho.
20% zinaenda wapi kwa watu wanaoanza na msingi wa KUWEZA? hawa wanashindwa kufanikiwa kwasababu hushindwa kukuza hisia za KUPENDA wanachokiweza hivyo huwa ngumu kufanikiwa , kwasababu watafanya pasipo uhuru wa akili na nafsi na pia watafanya chini ya uwezo wao kwa kukosa ARI ya kukifanya hicho kitu. Hivyo tuna mifumo miwili ambayo ni
- KUWEZA-----> KUPENDA hapa ndipo mtu atakapofanya kitu kwanza kwasababu anakiweza kisha kupenda kutajijenga baadae kwasababu hisia hujengeka katika pande mbili furaha na huzuni hivyo hisia ya kupenda itakuja kutokana na furaha ya mafanikio.
- KUPENDA-----> KUWEZA huu mfumo wa pili 10% tu ndio watakao fanikiwa na hiyo itatokea endapo mtu pamoja na kuamua kukifanya kitu kwa kukipenda lakini ni kitu ambacho ndicho alicho na uwezo nacho, 90% hatafanikiwa kwasababu hawatakuwa na uwezo nacho hivyo wataishia kuiga.
Msingi wa KUWEZA mara nyingi hupuuzwa kwasababu mara nyingi kile mtu anachokiweza kinakuwa hakimpendezi machoni pake au hakipendezi machoni pa wanajamii, Hivyo hakitamfanya aheshimike au kitamfanya jamii imdharau hivyo atakikwepa na kwenda kung'ang'aniza kile anachokipenda, kwasababu 100% ni lazima atakipenda kitu chenye taswira nzuri mbele yake na jamii kiujumla. Mwanadarasa unaweza kuona wewe ni mtanashati ama mrembo hivyo kuuza juice au matunda kitakufanya usiheshimike mbele ya jamii na kikakushushia hadhi lakini ni kitu ambacho UNAKIWEZA kwa 100% yani ukiongea tu mteja kesho atakuja tena kwasababu uweza wako umejengeka katika kauli.
Inawezekana umejengwa uweza ndani yako ukamfundisha au kumwelekeza mtu mpaka akaelimika lakini kwasababu tu hutaki ualimu basi hautakuwa tayari kukifanya hicho kitu huku uking'ang'aniza kuwa mfanyakazi wa benki kwasababu hata jamii ikikuona kuwa upo sehemu ya kiyoyozi itasema ndiyo yule, ndo mtu fulani, lakini kuwa mwalimu kama FARADAY hapa jamii itakudharau.
Na hii misingi ndiyo ambayo hujengwa mpaka kwa watoto wetu na hivyo kuwaelekeza katika mwelekeo wa vitu vinavyoonekana na wanajamii vyenye kupendeza sana, Lakini tunasahau msingi wa kuwaelekeza watoto wetu katika mwelekeo wa vitu wanavyoviweza.
Mwanadarasa utakuwa shahidi hapa pale inapoinuka misemo kama
1."Napenda sana kufanya hiki lakini sifanikiwi nimetumia nguvu na akili yote lakini wapi" mwalimu anakwambia hapo akili haitumiki bali kivuli cha akili, ubongo hauwezi kusukuma akili ikafanye kitu ambacho hauna uwezo nacho, hapa utatumia akili inayotokana na nguvu ya macho kwa kuiga kile unachokiona.
2."Sipendi kufundisha" lakini matokeo kila yanapokuja somo lake ndilo ambalo la kwanza kufaulisha au wanafunzi wanajivunia kuwa nae kwasababu wanamwelewa" hapa ni pale unaposhindwa KUPENDA unachokiweza.
Msaada wa ASILIA (nature).
Asilia au nature kama wengi wanavyoelewa kwa urahisi husaidia sana kumlazimisha mtu arudi afanye kile anachokiweza hapa ni pale kauli hii hutokea
"Nilikuwa najaribu tu kufanya hivi lakini nimefanikiwa hata siamini nahisi nimebahatisha" hapo mwalimu anakuambia umeongozwa na nature kukusaidia kukuonesha kile unachokiweza ili uache kuhangaika na kile usichokuwa na uwezo nacho, lakini mtu hataendelea kukifanya kitu hicho kwa ufanisi zaidi akiamini ni bahati.
Hivyo mwalimu anakwambia mwanadarasa fanya kitu unachokiweza, KUKIPENDA kutakuja tu kwasababu kupenda ni HISIA, utakapofanya unachokiweza ndipo ambapo ubongo utasukuma akili nyingi zaidi na kukuonesha kile ambacho wengine hawakioni juu ya shughuli hiyo. Haijalishi hicho kitu unachokiweza hakina heshima sana mtaani au hakina heshima mbele ya macho yako lakini amini wewe ndiye utakaeenda kubadilisha taswira nzima ya hiyo shughuli na kuifanya iheshimike mbele ya jamii.
Usiende kuimba kwasababu Unapenda muziki nenda kwasababu unaweza muziki, Usifanye kitu kwasababu ya jina lake ambalo lilijengwa na watu waliokuwa wameumbwa na uwezo wa kukifanya hicho kitu, bali fanya kwasababu unaweza hatakama ni kidogo, kuna huyu jamaa anaitwa Napoleon Hill anakwambia "do small things in a great way"
Pia wewe umechelewa kukifanya unachokiweza mwanao hajachelewa tutakuja kuchambua vizuri tukifika katika nyanja ya Elimu lakini Usishangae Ronaldo pamoja na kuwa na hela nyingi za kuweza kumpeleka mtoto wake shule yoyote ile hata ikianzishwa sayari nyingine Lakini atampeleka Akademiki ya mpira kwasababu anampeleka kwenye kitu ambacho anaweza.
Tukutane sehemu ya tano na ya mwisho ya somo letu hili la pili ambapo tutakuwa na kichwa kinachosema "NJIA ZA KUSAFISHA UBONGO NA AKILI" muhimu sana hapa.
PIA USISAHAU KUMCHEKI MWALIMU KUPITIA NAMBA YAKE KWA AJILI YA KUUNGANISHWA WHATSAPP KWA MASOMO MENGINE YATAKAYOKUWA YAKIENDELEA HUKO.
<H. FARADAY> (0625934471).