SOMO LA PILI (LESSON TWO).
AKILI YAKO KUFANYA VITU ISIVYOPASWA KUVIFANYA NA KUTOKUFANYA VITU IPASWAVYO KUVIFANYA.
Ni imani ya mwalimu kuwa mwanadarasa u mzma na unaendelea kufwatilia mfululizo wa masomo yetu. Endelea kufwatilia yameandaliwa masomo mengi kwa ajili yako, usisite kuuliza sehemu yoyote ambayo utakuwa haujaielewa.
Somo letu la pili
sehemu ya kwanza lina kichwa kinachoitwa;
MAHAKAMA NDANI YA NAFSI YAKO (HUMAN SPIRITUAL INNER COURT).
Mwalimu anaanza kwa kuelezea kwa maana rahisi kitu kinachoitwa mahakama, kuwa ni sehemu ambapo tunapata
HUKUMU ya tatizo lilitokea kwa kufuata haki chini ya sheria fulani iliyowekwa ili kuleta usawa, suluhu na amani katika jamii husika. Tutajikita zaidi kwenye neno hukumu kama ambavyo nimeliandika hapo juu.
Ndani ya mwili wa binadamu kuna kitu ambacho wanafilosofia tunakiita
CONSCIENS tunasema ni sauti ya ndani kabisa inayomuongoza mtu kwenye kipi sahihi afanye na kipi si sahihi asifanye
(an inner voice or feeling viewed as an acting as guide to the rightness or wrongness of one's behaviour), hii sauti mara nyingi hupuuzwa (ignored) baada ya matokeo ya kile ulichoenda kukifanya kuwa siyo hii sauti inakupeleka kwenye mahakama ambayo ni nafsi kisha unaanza kuhukumiwa
ndani, baada ya tukio lote hilo kufanyika kinakuja kitu kinachoitwa majuto (
regression). Kumbuka vitu vyote hivi vinafanyika ndani yako hapa mwanadarasa utakuwa shahidi pale muda mwingine unatembea uko peke yako lakini unajiona kama uko na mwenzako kama mnapiga stori kabisa mwisho mtu anaweza hata kucheka peke yake hivyo kipindi hayo yote yanafanyika ni ngumu binadamu mwingine kujua kwasababu kipindi vinafanyika vyote hivo mwili wa nyama huendelea na majukumu yake kama kawaida.
Majuto haya huja kujionesha kwa hali ya nje ya kimwili ambapo mtu huyo anakuwa na msongo wa mawazo (stress) na pia huwa mwenye hasira au mnyonge kitu ambacho kinaleta madhara pia kwa binadamu ya kiafya kama Magonjwa ya moyo na mengineyo. Mwalimu anatoa mfano kidogo.
Mfano huu nitautoa kwenye mlengo wa
mapenzi, inawezekana mwanaume ambae yupo ndani ya mahusiano lakini akapita sehemu na kumuona mwanamke flanI akavutiwa nae akaamua kwenda kumtongoza hiki kitendo cha kwanza lazima kitaambatana na sauti nyingine nyuma ndani yake inayomwambia
MBONA UNAE LAKINI WA KWAKO ataamua kuipuuza, baada ya kumtongoza huyo binti akiulizwa swali labda kweli hauna mwanamke mwingine? Mwanaume atakachojibu kuwa
SINA, lakini kutakuja sauti nyingine ndani yake inamwambia
ACHA UONGO MBONA UNAE kumbuka huyu mtu anafanya majibizano bila mwanamke kugundua, hivyo huyu mwanaume anaweza kukubaliwa na mwanamke sasa ikijatokea labda mwanamke ni mwathirika na huyo mwanaume amekuja kuambukizwa ugonjwa. Hapo ndipo maneno yafutayo yanapojitokeaza na maneno hayo huenda nawewe mwanadarasa umewahi kumbana nayo katika tukio lolote flanI lilikutokea maneno hayo ni kama
- Lakini Moyo ulisita sana kufanya
- Nilihisi haya yangetokea
- Nilijua tu.
Na maneno mengine mengi hivyo hufanya kwenye nafsi yako kutawaliwe na migogoro kumbuka siyo tukio moja unalopata matokeo hasi, hivyo moyoni mwako kunakuwa na mlundikano wa
Lawama na
majuto ndani yako. Sauti hii hupuuzwa katika nyanja nyingi zinazohusu maisha ya binadamu, sauti hii hupuuzwa pale binadamu anapofanya shughuli ya kumuingizia kipato. Nini sabubu ya sauti hii kupuuzwa twende tukaiangalie.
Sababu ya sauti hii ya ndani (
inner voice) kupuuzwa ni kutokana na msingi wa maisha uliojengwa kwa huo, msingi ambao unasimamia kwenye neno
kawaida yaani kila utakachokifanya ni kitu ambacho kimeshafanywa tayari kitu ambacho kinakutaka upitie hatua moja mbili tatu zilizowekwa tayari ili uweze kufika,
HUKU ukisahau hizo hatua hazikuwepo kabla isipokuwa ni mtu aliziona ndani ya ubongo wake na kuziweka hadharani leo hii inakuwa ndiyo njia (
PATHWAY) ya wewe kupita.
KAWAIDA tunayozungumzia hapa ni kawaida ambayo jamii nzima imejengwa kwa hiyo, ambapo ndani ya jamii tunakutana na kauli hii
"ili uweze kufanya hiki kitu kwa kawaida tunafanya hivi" lakini tunasahau huyo mwasisi wa hiyo inayoitwa kawaida ni mtu mmoja. Mfano wa kawaida mojawapo "
mtoto anaefaulu darasa la saba, akafaulu na form four kisha form six na kwenda chuo moja kwa moja huyo ndo mwenye akili" lakini huyu ambae ataenda kukisomea kitu ambacho ndicho amejaaliwa nacho na kukibobea kabisa na kisha kuwa mtaalamu wa hicho basi mtu huyo hataheshimiwa kama msomi wala hataheshimiwa ama kuonekana ni mwenye akili kwasababu hajapita kwenye hiyo njia ya chuo kikuu, ila tu ataonekana anajua kitu fulani, hiyo ndo kawaida ambayo jamii imejengwa kwa hiyo, na kawaida zingine unazozifahamu wewe mwanadarasa.
Sababu nyingine inayofanywa sauti hiyo ipuuzwe ni kuusikiliza mwili wa nje ambao umejengwa ndani ya dhana ya kuamini kile tu ambacho kimekwisha kutokea hivyo kuamini kile ambacho hakijatokea bado huwa ni ngumu kwasababu mwili huu huona kama unaenda kinyume na uhalisia lakini pia huu mwili wa nje unaoongozwa na milango mitano ya fahamu ambapo hujitokeza neno
tamaa kwa kuona au kusikia, pia hii nayo ni moja ya sababu inayopelekea kuipuuza hii sauti.
Mpaka hapo tunaweza tukatenganisha haya makundi mawili makubwa, la kwanza;
Kundi la kwanza Sauti hii inapuuzwa na msingi ambao umemjenga mwanajamii ambao uko juu ya neno
kawaida hapa uhusika zaidi na kupuuza sauti inayohusika na shughuli za kuyajenga maisha zinamuingizia mtu kipato.
Kundi la pili sauti hii inapuuzwa na mwili wa nje unaoongozwa na milango ya fahamu ambapo tunapata neno
TAMAA hapa panahusika na shughuli zinazohusu hisia kama
mapenzi (love affairs).
Athari ya jumla ni kwamba unaupa ubongo ubize wa kushughulika na kazi ambayo haikupaswa kushughulika nayo, ubongo wako na wa
SUPERIOR unakuwa uko bize ila tofauti ni aina ya ubize sehemu ya pili tutaangalia ubize wa superior ni upi wakati wewe mwanadarasa ubize wako ni kusuluhisha hiyo migogoro.
Hivyo baada ya Sauti hii kupuuzwa kinachokuja kufwata ni
LAWAMA na
HUKUMU ndani yako ambayo huendeshwa na mahakama ambayo ni
NAFSI yako. Lakini Lawama na Hukumu hii huwa inakubaliwa katika kundi la pili kwa maana nyingine kujutia kunakubaliwa katika kundi la shughuli za kihisia
KWANINI na pia vipi kuhusu kundi la kwanza ambalo linahusika na shughuli za utafutaji je majuto yanakubaliwa?? Na vipi kama niliisikiliza sauti na bado nikapata majibu hasi???
Tuungane sehemu ya pili ya hili somo la pili.
<H.Faraday> (0625934471).