Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Haber Faraday

Member
Jul 3, 2017
97
182
Chakula cha akili (Mental food) Lesson 1.

Karibu kwenye darasa ambalo mwalimu ni UBONGO (brain) na mwanafunzi ni mimi na wewe, darasa hili litakuwa na somo KUU moja (One main subject of study) ambalo ni Maisha (Life). Somo hili litagawanyika katika vipande vingi kulingana na upana wake.

Mwalimu wetu atatufundisha kuhusu vitu mbalimbali vinavyohusu maisha ya BINADAMU (human life), akiongelea maisha ya waafrika kwa ujumla kisha maisha ya watu wa taifa lake Tanzania. Hivyo atafundisha nyanja ya Uchumi, Afya, Elimu, Biashara, Kilimo, na nyanja mbalimbali zitakazokuja katika masomo ya mbele.

Mwalimu anakutaka utafute kiasi cha Tsh 0 ili ununue kitabu ambacho kitatumika, kitabu hiki kinaitwa Uzoefu (EXPERIENCE) ambacho ana imani wewe mwanadarasa wake utakipata kwa urahisi, yeye ataenda mbali zaidi kutumia vitabu vya wengine ambao watakuwa mbali na darasa letu. Kutakuwa na mfululizo wa masomo hivyo mwalimu hatopenda kuwa na mwanafunzi mtoro darasani.

Masomo yanalenga kusaidia kizazi kilichopo ambacho kina macho lakini hakioni na pia siyo kwa manufaa ya kizazi kilichopo bali kwa manufaa ya kile kijacho. Pia mwalimu anaamini mwanadarasa atakae kuwa ameelewa somo basi utakuwa ni wajibu wake kutoa funzo (vision) maono kutokana na yeye alivokielewa kitabu chake.

Mwalimu anatukumbusha kuwa darasa letu halifungamani na upande wowote wa kisiasa, halihukumu, halilaumu bali linatoa ufumbuzi (solution), darasa lina watu wa umri tofauti umri wa chini, kati na juu ni imani ya mwalimu kuwa umri wa juu utanyoosha sana mikono kujibu maswali na huku unufaikaji wao ni 20% huku umri wa chini japo si wanyooshaji sana mikono unufaikaji wao ni asilimia 80%.

Kabla ya kumalizia utangulizi mwalimu anashangazwa kidogo kwa kuona somo la maisha halipo kwenye mtaala (curriculum) wowote lakini mshangao wake unakoma baada ya kuona Vipande vya somo la maisha vipo katika mitaala yote, Wasomi wote na watu wenye IQ kubwa wameshindwa kutupa formula ya maisha naam Hakuna formula ya maisha. Lakini kwanini hili Somo watu wanafeli sana lakini pia kwanini tutofautiane kufeli baina ya nchi na nchi au familia na familia wakati wote Somo hili halipo kwenye mtaala kuna nini nyuma ya pazia??.

kwa utangulizi huo tutaenda kuangalia somo la kwanza lenye kichwa

LESSON ONE 1.

☆JITAMBUE na KUTAMBUA ni nini Umebeba na una NGUVU na UWEZO kiasi gani (self esteem).

•Sehemu ya kwanza

●WEWE NI NANI (who are you)?.

Somo hili linahitaji utulivu wa mawazo ili uweze kulielewa, katika somo hili linaanza kwa kutuuliza mimi au wewe ni nani majibu ni marahisi sana unaweza jibu mimi Ni mtanzania, au mimi ni mwafrika au vyovyote utakavoona sawa
LAKINI
mwalimu wetu anasema ukiulizwa hivo jibu mimi ni kiumbe Hai kinachoitwa Binadamu, mwanadarasa anaanza kujiuliza kuwa kwanini nitangulie kujiita kiumbe Hai? Jibu ni kwasababu "unaishi" ambapo ndani ya huo mzizi wa neno tunapata neno MAISHA.

Mwanadarasa anawaza kwanini nisiseme tu mimi binadamu? mwalimu anajibu kuwa kwasababu neno HAI linatupa mwanga wa neno ishi hivyo ukisema mimi ni binadamu tu unaweza kuwa wewe ni binadamu ambae UPO Lakini Hauishi tutaangalia tofauti ya KUWEPO na KUISHI (Existing and Living). Hivo basi kwa kuwa wewe ni binadamu kama kiumbe hai upo kwenye kundi ambalo kibaiolojia linaitwa KINGDOM-ANIMALIA-MAMMALIA lakini hauko peke yako kuna wanyama wengine pia ambao mna sifa sawa.

Sasa ni nini tofauti yako wewe na hao wanyama wengine? mwanadarasa atawaza utofauti wa kila aina anaoujua
LAKINI
Mwalimu anatuambia utofauti mkubwa uliopo ni kitu kimoja kinachoitwa REASONING "•Nafsi inayoishi ndani yako inayokuwa nyuma ya kitendo au tukio lolote ambalo kabla ya kufanyika nje ya mwili wako nafsi inakuletea swali la KWANINI•?" baada ya nafsi hii kuuliza kwanini, basi akili yako itatoa sababu hivyo hupatikana neno lingine linaloitwa KWASABABU, hivyo kuishi kwetu kupo ndani ya haya maneno mawili kwahiyo kila jambo ulilonalo au unalolifanya ni matokeo ya Reasoning.

Kisha tunahitimisha kuwa utofauti wa kuishi tulionao huanza kwa kutofautiana REASONING, hii process ya Reasoning huwa inaipa kazi ubongo utumie akili kujibu, mwalimu anazidi kueleza kuwa kiwango cha akili kinachokubaliana na ubongo kufanya hii process kinatofautiana kati ya mtu na mtu, hahaha mwalimu anacheka kidogo kuona watu wanatumia kiwango kidogo chini ya 20% huku kiwango kikubwa cha ubongo kinachoifanya akili itumike kinachobaki kinafukiwa kwenye udongo.

Mwalimu anatoa homework ya kwanza ambayo ni kujiuliza ni asilimia ngapi unazotumia kukamilisha kitendo (process) ya Reasoning?, mpaka hapo tumemaliza kisehemu cha kwanza kwenye somo letu la kwanza sehemu yetu ya kwanza inayotuuliza sisi ni nani.

Sehemu ya pili.

Sehemu ya pili katika somo letu hili la kwanza inatuuliza

●KWANINI UKO HIVYO ULIVYO?.

majibu hapa ni marahisi sana ambayo mwanadarasa atafikiria kuyajibu nayo ni niko hivi kwasababu Mungu kapenda niwe hivi au niko hivi kwasababu nimependa kuwa hivi au nimejikuta tu niko hivi yote ni majibu
LAKINI
mwalimu anatuambia tujibu hivi niko hivi kwasababu ya misingi niliyoikuta na kuifuata kwa kuiiga, ni misingi gani hiyo na ilianzishwa na nani?
kabla ya kujibu swali hili tuangazie kidogo kitu kinachoitwa MAPINDUZI YA KIMFUMO (system revolution).

Koo (Clan) zetu 90% zimetokea katika chimbuko la hali duni lakini siyo zote mpaka leo zina hali duni, kwanini maendeleo yanaonekana kwenye baadhi ya koo? kitendo kilichotokea ni mapinduzi ya kimfumo mapinduzi haya hayafanywi na kundi la wana ukoo bali yanafanywa na mtu mmoja (a single person) huyu atafanya REASONING process tofauti na wanaukoo wenzake, swali atakalojiuliza linaturudisha kwenye kichwa cha sehemu ya pili kuwa KWANINI SISI tuko hivi na sio vile. Nguvu ya ubongo kusukuma akili nyingi ili isitumie tena 20% kwa ajili ya REASONING inampelekea kupata majibu mazuri ambayo nje ya mwili ni utekelezaji wa vitendo.

Mwalimu anawaangalia wanadarasa wake anaona sio wao tu wana hali duni na pia mpaka wale wanaowazunguka, anaamua kuuliza kuwa nani yuko tayar kuishi nje ya mfumo alioukuta wote wananyoosha mikono.

Mwalimu anaamua kuongezea mfano kuwa kwa wale waumini wa dini ya kikristo wanaamini "MUNGU aliuliza kuwa nimtume nani akaokoe wanadamu Yesu akasema Nitume mimi baba" Leo hii Mungu anakuuliza mwanadarasa kuwa amtume nani kuokoa ukoo /familia yako kwanini usiseme nitume mimi??. Hivyo basi misingi na mifumo tuliyoikuta hatufanyi REASONING itayotoka nje ya mifumo na misingi hiyo. Baadae tutakuja kuangalia aina za mifumo jinsi ya kuiboresha au pia kutoka kabisa nje ya mifumo na misingi hiyo.

Mwalimu anaanza kuona wanafunzi wamechoka kusoma anaamua kuaga.

Sehemu ya tatu 3# ya somo letu la kwanza itaendelea ambapo tutakutana na mojawapo ya kitu hiki "waafrika walio wengi hususani wataanzania wana majukumu matatu 3 katika maisha wakati wazungu walio wengi wana jukumu moja" ni majukumu gani hayo endelea kuingia darasani bila kutoroka.

<H.Faraday>

UZI NI MREFU USIUQUOTE PLEASE.

Bonyeza hapo kupata sehemu ya tatu.

sehemu ya tatu chakula cha akili (Mental food).

Kupata sehemu ya nne bonyeza hapa

Darasa: Chakula cha akili (Mental food) sehemu ya nne

Somo la pili sehemu ya kwanza (lesson two part one) bonyeza hapa
Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Mwendelezo wa sehemu ya pili katika somo la pili bofya hapa Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Sehemu ya tatu somo la pili bofya hapa Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

sehemu ya nne somo la pili bofya hapa Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

sehemu ya tano (A) somo la pili Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

sehemu ya tano (B) somo la pili Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

sehemu ya tano (C) somo la pili Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Sehemu ya mwisho somo la pili bonyeza hapa
Darasa: Chakula cha akili (Mental food)
 
Chakula cha akili (Mental food) Lesson 1.

Karibu kwenye darasa ambalo mwalimu ni UBONGO (brain) na mwanafunzi ni mimi na wewe, darasa hili litakuwa na somo KUU moja (One main subject of study) ambalo ni Maisha (Life). Somo hili litagawanyika katika vipande vingi kulingana na upana wake.

Mwalimu wetu atatufundisha kuhusu vitu mbalimbali vinavohusu maisha ya BINADAMU (human life), akiongelea maisha ya waafrika kwa ujumla kisha maisha ya watu wa taifa lake Tanzania. Hivyo atafundisha nyanja ya Uchumi, Afya, Elimu, Biashara, Kilimo, na nyanja mbalimbali zitakazokuja katika masomo ya mbele.

Mwalimu anakutaka utafute kiasi cha Tsh 0 ili ununue kitabu ambacho kitatumika kitabu hiki kinaitwa Uzoefu (EXPERIENCE) ambacho ana imani wewe mwanadarasa wake utakipata kwa urahisi yeye ataenda mbali zaidi kutumia vitabu vya wengine ambao watakuwa mbali na darasa letu. Kutakuwa na mfululizo wa masomo hivyo mwalimu hatopenda kuwa na mwanafunzi mtoro darasani.

Masomo yanalenga kusaidia kizazi kilichopo ambacho kina macho lakini hakioni na pia siyo kwa manufaa ya kizazi kilichopo bali kwa manufaa ya kile kijacho. Pia mwalimu anaamini mwanadarasa atakae kuwa ameelewa somo basi utakuwa ni wajibu wake kutoa funzo (vision) maono kutokana na yeye alivokielewa kitabu chake.

Mwalimu anatukumbusha kuwa darasa letu halifungamani na upande wowote wa kisiasa, halihukumu, halilaumu bali linatoa ufumbuzi (solution), darasa lina watu wa umri tofauti umri wa chini, kati na juu ni imani ya mwalimu kuwa umri wa juu utanyoosha sana mikono kujibu maswali na huku unufaikaji wao ni 20% huku umri wa chini japo si wanyooshaji sana mikono unufaikaji wao ni asilimia 80%.

Kabla ya kumalizia utangulizi mwalimu anashangazwa kidogo kwa kuona somo la maisha halipo kwenye mtaala (curriculum) wowote lakini mshangao wake unakoma baada ya kuona Vipande vya somo la maisha vipo katika mitaala yote, Wasomi wote na watu wenye IQ kubwa wameshindwa kutupa formula ya maisha naam Hakuna formula ya maisha. Lakini kwanini hili Somo watu wanafeli sana lakini pia kwanini tutofautiane kufeli baina ya nchi na nchi au familia na familia wakati wote Somo hili halipo kwenye mtaala kuna nini nyuma ya pazia??.

kwa utangulizi huo tutaenda kuangalia somo la kwanza lenye kichwa

1.WEWE NI NANI (who are you)?.
Somo hili linahitaji utulivu wa mawazo ili uweze kulielewa, katika somo hili linaanza kwa kutuuliza mimi au wewe ni nani majibu ni marahisi sana unaweza jibu mimi Ni mtanzania, au mimi ni mwafrika au vyovyote utakavoona sawa LAKINI mwalimu wetu anasema ukiulizwa hivo jibu mimi ni kiumbe Hai kinachoitwa Binadamu, mwanadarasa anaanza kujiuliza kuwa kwanini nitangulie kujiita kiumbe Hai ni kwasababu "unaishi" ambapo ndani ya huo mzizi wa neno tunapata neno MAISHA.

Mwanadarasa anawaza kwanini nisiseme tu mimi binadamu? mwalimu anajibu kwasababu neno HAI linatupa mwanga wa neno ishi hivyo ukisema mimi ni binadamu tu unaweza kuwa wewe ni binadamu ambae UPO Lakini Hauishi tutaangalia tofauti ya KUWEPO na KUISHI (Existing and Living). Hivo basi kwa kuwa wewe ni binadamu kama kiumbe hai upo kwenye kundi ambalo kibaiolojia linaitwa KINGDOM-ANIMALIA-MAMMALIA lakini hauko peke yako kuna wanyama wengine pia ambao mna sifa sawa.

Sasa ni nini tofauti yako wewe na hao wanyama wengine? mwanadarasa atawaza utofauti wa kila aina anaoujua lakini Mwalimu anatuambia utofauti mkubwa uliopo ni kitu kimoja kinachoitwa REASONING "Nafsi inayoishi ndani yako inayokuwa nyuma ya kitendo au tukio lolote ambalo kabla ya kufanyika nje ya mwili wako nafsi inakuletea swali la KWANINI?" baada ya nafsi hii kuuliza kwanini basi akili yako itatoa sababu hivyo kutapatikana neno KWASABABU, hivyo kuishi kwetu kupo ndani ya haya maneno mawili kwahiyo kila jambo ulilonalo au unalolifanya ni matokeo ya Reasoning.

Kisha tunahitimisha kuwa utofauti wa kuishi tulionao huanza kwa kutofautiana REASONING, hii process ya Reasoning huwa inaipa ubongo utumie akili kujibu, mwalimu anazidi kueleza kuwa kiwango cha akili kinachokubaliana na ubongo kufanya hii process kinatofautiana kati ya mtu na mtu hahaha mwalimu anacheka kidogo kuona watu wanatumia kiwango kidogo chini ya 20% huku kiwango cha ubongo kinachobaki kinazikwa kwenye makaburi.

mwalimu anatoa homework ya kwanza kujiuliza asilimia ngapi zinatumika kukamilisha kitendo (process) ya Reasoning, mpaka hapo tumemaliza kisehemu cha kwanza kwenye somo letu la kwanza linalotuuliza sisi ni nani

Sehemu ya pili katika somo letu hili la kwanza inatuuliza KWANINI UKO HIVO ULIVO?.
majibu hapa ni marahisi sana niko hivi kwasababu Mungu kapenda niwe hivi au niko hivi kwasababu nimependa kuwa hivi au nimejikuta tu niko hivi yote ni majibu
LAKINI mwalimu anatuambia tujibu hivi niko hivi kwasababu ya misingi niliyoikuta na kuifuata kwa kuiiga, ni misingi gani hiyo na ilianzishwa na nani?
kabla ya kujibu swali hili tuangazie kidogo kitu kinachoitwa MAPINDUZI YA KIMFUMO (system revolution).

Koo (Clan) zetu 90% zimetokea katika chimbuko la hali duni lakini siyo zote mpaka leo zina hali duni kwanini? maendeleo yanayoonekana kwenye baadhi ya koo, kitendo kilichotokea ni mapinduzi ya kimfumo mapinduzi haya hayafanywi na kundi la wana ukoo bali yanafanywa na mtu mmoja (a single person) huyu atafanya REASONING process tofauti na wenzake, swali atakalojiuliza linaturudisha kwenye kichwa cha sehemu ya pili kuwa KWANINI SISI tuko hivi na sio vile. Nguvu ya ubongo kusukuma akili nyingi isitumie tena 20% kwa ajili ya REASONING inampelekea kupata majibu mazuri ambayo nje ya mwili ni utekelezaji wa vitendo.

mwalimu anawaangalia wanadarasa wake anaona sio wao tu wana hali duni na pia mpaka wale wanaowazunguka, anaamua kuuliza kuwa nani yuko tayar kuishi nje ya mfumo alioukuta wote wananyoosha mikono.

mwalimu anaamua kuongezea mfano kuwa kwa wale waumini wa dini ya kikristo wanaamini "MUNGU aliuliza kuwa nimtume nani akaokoe wanadamu Yesu akasema Nitume mimi baba" Leo hii Mungu anakuuliza mwanadarasa kuwa amtume nani kuokoa ukoo /familia yako kwanini usiseme nitume mimi??.

mwalimu anaanza kuona wanafunzi wamechoka kusoma anaamua kuaga

Kuwa sehemu ya tatu 3# ya somo letu la kwanza itaendelea ambapo tutakutana na mojawapo ya kitu hiki "waafrika walio wengi hususani wataanzania wana majukumu matatu 3 katika maisha wakati wazungu walio wengi wana jukumu moja" ni majukumu gani hayo endelea kuingia darasani bila kutoroka.

<H.Faraday>
shusha vitu
 
shusha vitu
Ujaelewa maelezo mkuu
Chakula cha akili (Mental food) Lesson 1.

Karibu kwenye darasa ambalo mwalimu ni UBONGO (brain) na mwanafunzi ni mimi na wewe, darasa hili litakuwa na somo KUU moja (One main subject of study) ambalo ni Maisha (Life). Somo hili litagawanyika katika vipande vingi kulingana na upana wake.

Mwalimu wetu atatufundisha kuhusu vitu mbalimbali vinavohusu maisha ya BINADAMU (human life), akiongelea maisha ya waafrika kwa ujumla kisha maisha ya watu wa taifa lake Tanzania. Hivyo atafundisha nyanja ya Uchumi, Afya, Elimu, Biashara, Kilimo, na nyanja mbalimbali zitakazokuja katika masomo ya mbele.

Mwalimu anakutaka utafute kiasi cha Tsh 0 ili ununue kitabu ambacho kitatumika kitabu hiki kinaitwa Uzoefu (EXPERIENCE) ambacho ana imani wewe mwanadarasa wake utakipata kwa urahisi yeye ataenda mbali zaidi kutumia vitabu vya wengine ambao watakuwa mbali na darasa letu. Kutakuwa na mfululizo wa masomo hivyo mwalimu hatopenda kuwa na mwanafunzi mtoro darasani.

Masomo yanalenga kusaidia kizazi kilichopo ambacho kina macho lakini hakioni na pia siyo kwa manufaa ya kizazi kilichopo bali kwa manufaa ya kile kijacho. Pia mwalimu anaamini mwanadarasa atakae kuwa ameelewa somo basi utakuwa ni wajibu wake kutoa funzo (vision) maono kutokana na yeye alivokielewa kitabu chake.

Mwalimu anatukumbusha kuwa darasa letu halifungamani na upande wowote wa kisiasa, halihukumu, halilaumu bali linatoa ufumbuzi (solution), darasa lina watu wa umri tofauti umri wa chini, kati na juu ni imani ya mwalimu kuwa umri wa juu utanyoosha sana mikono kujibu maswali na huku unufaikaji wao ni 20% huku umri wa chini japo si wanyooshaji sana mikono unufaikaji wao ni asilimia 80%.

Kabla ya kumalizia utangulizi mwalimu anashangazwa kidogo kwa kuona somo la maisha halipo kwenye mtaala (curriculum) wowote lakini mshangao wake unakoma baada ya kuona Vipande vya somo la maisha vipo katika mitaala yote, Wasomi wote na watu wenye IQ kubwa wameshindwa kutupa formula ya maisha naam Hakuna formula ya maisha. Lakini kwanini hili Somo watu wanafeli sana lakini pia kwanini tutofautiane kufeli baina ya nchi na nchi au familia na familia wakati wote Somo hili halipo kwenye mtaala kuna nini nyuma ya pazia??.

kwa utangulizi huo tutaenda kuangalia somo la kwanza lenye kichwa

LESSON ONE 1.

☆JITAMBUE na KUTAMBUA ni nini Umebeba na una NGUVU na UWEZO kiasi gani (self esteem).

•Sehemu ya kwanza

●WEWE NI NANI (who are you)?.

Somo hili linahitaji utulivu wa mawazo ili uweze kulielewa, katika somo hili linaanza kwa kutuuliza mimi au wewe ni nani majibu ni marahisi sana unaweza jibu mimi Ni mtanzania, au mimi ni mwafrika au vyovyote utakavoona sawa •LAKINI
mwalimu wetu anasema ukiulizwa hivo jibu mimi ni kiumbe Hai kinachoitwa Binadamu, mwanadarasa anaanza kujiuliza kuwa kwanini nitangulie kujiita kiumbe Hai? Jibu ni kwasababu "unaishi" ambapo ndani ya huo mzizi wa neno tunapata neno MAISHA.

Mwanadarasa anawaza kwanini nisiseme tu mimi binadamu? mwalimu anajibu kuwa kwasababu neno HAI linatupa mwanga wa neno ishi hivyo ukisema mimi ni binadamu tu unaweza kuwa wewe ni binadamu ambae UPO Lakini Hauishi tutaangalia tofauti ya KUWEPO na KUISHI (Existing and Living). Hivo basi kwa kuwa wewe ni binadamu kama kiumbe hai upo kwenye kundi ambalo kibaiolojia linaitwa KINGDOM-ANIMALIA-MAMMALIA lakini hauko peke yako kuna wanyama wengine pia ambao mna sifa sawa.

Sasa ni nini tofauti yako wewe na hao wanyama wengine? mwanadarasa atawaza utofauti wa kila aina anaoujua •LAKINI
Mwalimu anatuambia utofauti mkubwa uliopo ni kitu kimoja kinachoitwa REASONING "•Nafsi inayoishi ndani yako inayokuwa nyuma ya kitendo au tukio lolote ambalo kabla ya kufanyika nje ya mwili wako nafsi inakuletea swali la KWANINI•?" baada ya nafsi hii kuuliza kwanini, basi akili yako itatoa sababu hivyo hupatikana neno lingine linaloitwa KWASABABU, hivyo kuishi kwetu kupo ndani ya haya maneno mawili kwahiyo kila jambo ulilonalo au unalolifanya ni matokeo ya Reasoning.

Kisha tunahitimisha kuwa utofauti wa kuishi tulionao huanza kwa kutofautiana REASONING, hii process ya Reasoning huwa inaipa kazi ubongo utumie akili kujibu, mwalimu anazidi kueleza kuwa kiwango cha akili kinachokubaliana na ubongo kufanya hii process kinatofautiana kati ya mtu na mtu, hahaha mwalimu anacheka kidogo kuona watu wanatumia kiwango kidogo chini ya 20% huku kiwango kikubwa cha ubongo kinachoifanya akili itumike kinachobaki kinafukiwa kwenye udongo.

Mwalimu anatoa homework ya kwanza ambayo ni kujiuliza ni asilimia ngapi unazotumia kukamilisha kitendo (process) ya Reasoning?, mpaka hapo tumemaliza kisehemu cha kwanza kwenye somo letu la kwanza sehemu yetu ya kwanza inayotuuliza sisi ni nani.

•Sehemu ya pili.

Sehemu ya pili katika somo letu hili la kwanza inatuuliza

●KWANINI UKO HIVYO ULIVYO?.

majibu hapa ni marahisi sana ambayo mwanadarasa atafikiria kuyajibu nayo ni niko hivi kwasababu Mungu kapenda niwe hivi au niko hivi kwasababu nimependa kuwa hivi au nimejikuta tu niko hivi yote ni majibu
•LAKINI

Back
Top Bottom