Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Leo nisinge zamahumu ingekula kwangu darasa zr hv
 
Sehemu ya tatu.

Kengele
imeshagongwa tayari kwa kipindi kuanza ni imani ya mwalimu kuwa mwanadarasa yu buheri wa afya.


Katika sehemu ya tatu ya hili somo letu la kwanza tutaenda kuangalia kitu kinachoitwa;

NINI MAANA YA NENO MAISHA? (what does the word life mean?).

Lakini kabla ya kulianza somo hili tujikumbushe kidogo kuhusu ni nini mwalimu alitufundisha kipindi kilichopita, mwalimu alitupa utangulizi wa somo letu (introduction), pia mwalimu katika sehemu ya kwanza akatuuliza kuwa sisi ni akina nani tukapata kutambua kuwa msingi mkubwa unaotufanya tujione sisi ni viumbe hai vinavyoitwa binadamu ni kuwa na uwezo wa kumudu kitendo kinachoitwa (Reasoning).

Mwalimu hakuishia hapo kwenye sehemu ya pili akatuuliza tena kuwa kwanini tuko hivi? Ndipo alipotupeleka kwenye vitu vinavyoitwa mifumo ya maisha (systems of life), na mapinduzi ya kimfumo (system revolution). Kwa kujikumbusha hapo tutakuwa tunaenda na mtiririko mzuri kama kusudio la mwalimu linavyotaka, kama haukuelewa kitu usisite kusoma upya kwenye post ya kwanza maana hatutakuwa na tunzo ya mtu aliyewahi kumaliza kusoma bali utatunukiwa tunzo na moyo+akili yako kwa kuelewa Somo.

Cha kujikumbusha cha mwisho ni mwalimu aliweka baadhi ya vipande vya masomo kama kiporo (pending) ambayo moja (1) litaongelewa katika somo la leo na la pili (2) litaongelewa katika masomo ya mbeleni, vipande hivyo ni
  1. Tofauti ya kuwepo na kuishi (Existing and Living).
2. Mifumo na misingi, jinsi ya kutoka au jinsi ya kuikabili kwa kuirekebisha (systems modification).

Baada ya kujikumbusha hayo mwalimu anatutaka tulianze hili somo letu ambalo ni sehemu ya tatu katika somo la kwanza.

Somo hili lenye kichwa nini maana ya neno maisha?.

Mwanadarasa atajibu tu maisha ni kitendo cha kuwepo hai hapa duniani kabla mtu hajafukiwa na udongo, MWALIMU anafurahi kuona mwanadarasa hayuko mbali sana na maana halisi ya maisha, Mwalimu anamtaka mwanadarasa awe makini kusikiliza maana ya neno maisha na maneno yanayolizunguka neno maisha ambayo yanaonekana kuwa sawa LAKINI si sawa kuna utofauti ndani yake, ni maneno yapi hayo na utofauti wake nini twende tukayaangalie.

Maisha (life), tukianza na muhusika mkuu ambae ni neno maisha mwalimu anatuambia maisha ni hali inayowatofautisha wanyama (ambapo hapa binadamu yupo ndani yake) na mimea kutoka kwenye viumbe visivyo hai (organic matters) hali hii ikihusisha kitendo cha kuweza kukua (growth), kujizalisha au kuzaliana (reproduction), uwezo wa kufanya kazi au vitendo mbalimbali (functional activity) na kuweza kupata mabadiliko ndani au nje ya mwili kukielekea kifo (continual change preceding death). Mwalimu anatuambia kuwa pamoja na kuwepo kwa maana nyingi lakini hii ni sahihi zaidi.

LAKINI mwalimu kwa kujua wanadarasa ni wavivu wa kutaka kuishika na kuijua maana ya maisha yenye maelezo mengi anaamua kuwarahisishia kuwa mtu akikuuliza nini maana ya maisha mwambie ni hali ya uwepo wa binadamu au mnyama (existance of an individual human being or animal) hawa ndo wahusika wakuu katika somo letu hivyo weka mbali kidogo mimea.

Baada ya kupata tafsiri ya neno maisha twende tukaangalie maneno yanayolizunguka neno maisha pamoja na utofauti wake, Tukianza na maneno haya KUWEPO na KUISHI (Existing and Living) ambayo ni kiporo chetu cha kwanza yana maana au uhusiano gani mwalimu anasema

Existing (kuwepo) ni pale mlengwa wetu (mnyama-binadamu) ambapo anakumbana na vitendo mahususi au muhimu vinavyofanywa au kufanyika ili kumuwezesha kuwa hai au mzima (doing necessary to stay alive). Vitendo hivyo mahususi au muhimu ni kama kula (Eating), kupumua (breathing), kulala (sleeping), usafi au usalama wa afya (hygiene). Hapa sasa wengi wa wanadarasa ndipo walipo kuhakikisha wanaendelea kuliona jua, Reasoning inafanyika ili aweze kuwa hai tu au kuwa mzima ubongo utasukuma akili yake ilete maarifa ya kuweza kula, kuweza kuwa na pakulala.

Mwalimu anawaangalia wanadarasa anaamua kuwashangaza kidogo, unajua ubongo wako unasukuma akili ya asilimia 2.6% katika kuwaza kula, asilimia 3.4% kuwaza kuwa na pakulala na asilimia 15% zikikamilishwa na vitendo vingine vinavyokamilisha Existing, asilimia 80% badala ya kuzipeleka zinakotakiwa ziende zinaendelea kupunga upepo kichwani, mwalimu anaona kweli vichwa vya wanadarasa wengine ni sehemu ya kuhifadhia ubongo, mwalimu anatoa mfano kidogo mtu akisema piga push-up 10, ukifika ya 8 mpaka ya 9 utakuwa umechoka, vivyo hivyo akisema piga push-up 20 ukifika ya 18-19 mikono itakuwa inatetemeka KWANINI? Kuna kitu kinaitwa "set of mind".

Mwalimu anatutaka tuandike pembeni ya daftari kiporo hiki kuwa tutakuja kuangalia kitu kinachoitwa set of mind pia tutaangalia kitu kinachoitwa asilimia 80% za ubongo za nini? Zina kazi gani na zitumikeje.

Living (ishi) hapa ndipo watoto wa kisasa wanaita kujiongeza, ambapo inamaanisha kwamba ni ubora (savour) wa kila dakika unayokuwepo (exist), "to savour every moment of your existence" vitendo vinavyofanyika hapa ni kuweza kuona (taking in the sights), kuweza kunusa (taking in the smells) na kuyaweza mazingira yanayokuzunguka (taking in the environment around you).

Mwalimu anaona hapa panahitaji maelezo zaidi anaamua kuelezea kwa kina kidogo kuwa kwanza ni lazima ujue kuwa living ipo ndani ya existing ila ni kujiongeza au kujiboresha zaidi kutoka kuishia kwenye existing tu kisha kufika kwenye hatua nyingine ambayo ni living hivyo wanadarasa 100% wana exist wakati asilimia chache wako kwenye living, huku kujiongeza au kujiboresha (savour= quality by taste or/and smell) tunakoongelea hapa kwa kila dakika unayokuwepo (exist) unatokana na uwezo unaofanywa na ubongo wako kwa akili yako huo uwezo uliofichika ndani ya vitendo vinavyofanywa na milango ya fahamu.

Tunaposema uwezo wa kuona (Taking in the sights) kuweza kuona vitu ambavyo haviwezi kuonwa na mtu mwingine kwahiyo si kwa macho haya nje bali kwa macho ya ubongo. Hivyo kwa kuwa kila binadamu ameumbwa tofauti ina maana kwamba kila binadamu anacho cha kwake cha kukiona tofauti na mwingine kwasababu hata ubongo wa mapacha haufanani, mwalimu anaamua kuuliza wanadarasa nani ambae ameshakiona cha kwake? Na je huyo aliyekiona cha kwake anakifanyia kazi? Au unafanya cha mwenzako? Hivyo hii ni homework yako ya kwanza leo kukiona cha kwako na kama ulishakiona je unakifanyia kazi na kama unakifanyia kazi ni unakifanyia kwa asilimia ngapi?.

Mwalimu anamuona mwanadarasa yule umri umekwenda kidogo anajiona hata akikiona saizi hawezi kukifanyia kazi muda umeenda anasikitika sana LAKINI anasahau kuwa ana watoto ana nduguze ambao umri uko mahala pake kukiona hicho kilichoumbwa kwa ajili yake, hivyo mwalimu anakumbusha tena hili darasa ni kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho, mwalimu anacheka kidogo kuona kwamba hiki alichokiona cha kukuambia mwanadarasa haya kitatumika vizazi na vizazi hata akifukiwa leo chini ya udongo moyo wake una amani kwa kutua mzigo mzito kwa faida ya wewe mwanadarasa na yeyote atakae yasikia haya ni wajibu wako kuwafahamisha wanaokuzunguka waweze kuona vilivyopo ndani ya ubongo wao maana wana macho lakini hawaoni wanasubiri neno la kwamba ONA.

Sio hivyo tu pia Tunaposema uwezo wa kunusa (smell) hapa mwalimu anamaanisha kuweza kunusa harufu ambayo iko mbali ambayo mpaka wengine wanakuja kuinusa wewe ulishainusa mile tano kabla yao.

Hapa kwenye kuyaweza mazingira mazingira yanayokuzunguka mwalimu anamaanisha nini, mwalimu anaamini kila mwanadarasa ana mazingira tofauti toka anavyoamka kutembea mpaka anapofika darasani mwalimu anauliza je mazingira uliyonayo yanakutumia au wewe unayatumia? Je unaona nini kwenye mazingira ambacho wengine hawakioni au unanusa nini katika mazingira uliyopo ambacho wengine wameshndwa kunusa? AU WEWE NI SEHEMU AU UNATUMIKA KAMA MAZINGIRA YA MWENZAKO? Hiyo ni homework ya pili kwako wewe mwana darasa katika somo letu la leo.

Mwalimu anaendelea kusema tunapozungumzia ubora kwa njia ya ladha (taste) mwalimu anamaanisha ni ile ladha ya maisha unayoipata wewe kama wewe katika maisha yako je inapaswa kuendelea nayo na je ni chachu, chungu au tamu? Jibu analo mwanadarasa maana akifungua tu kitabu chake kinachoitwa experience anaikuta.

Lakini siyo maneno hayo tu yanayolizunguka neno maisha kuna neno lingine linaloitwa hai au uzima (being alive) lina tofauti sana na neno ishi (living) tunapozungumzia neno hai (alive) ni pale mtu anapokuwa zaidi ya kuishi, mtu ambae amejifunza jinsi ya kuishi (those who have actually learned how to truly live), watu ambao wanafanya zaidi ya kupumua (those who do more than just breath in and out) huyu mtu tunamuita yuko alive ana uhai wa akili, amekiona alichokuja nacho duniani na ana kifanyia kazi kwahiyo alive inakamilisha kitendo cha living "uhai unakamilisha ishi".

Mwalimu anasema wale ambao walikiona kitu chao na kukifanyia kazi ndio walio na ufaulu wa angalau wa maisha na kwa macho haya ya nje hicho atakachokiona mtu na kukifanya na kisha kikajulikana ndipo hapo washuhudiaji watakitamka kuwa kile ni kipaji, ufaulu wa asilimia kadhaa wa maisha uko ndani ya hiki kinachoonekana kipaji,

mwalimu anawakazia macho wanadarasa kisha anauliza kama wanawajua watu waliotumia kitu cha pekee walichoumbwa nacho na kama kweli wanamafanikio, wale walioitumia sauti kwa kuiona ni kitu cha pekee na hamna mwingine aliye nacho kama cha kwake na akatumia sauti yake na kama je imempa mafanikio, yule aliyoona miguu yake si kwa ajili ya kutembelea tu kama wengine watjmiavyo yeye akaenda mbali zaidi na kama je amepata mafanikio!!??

Mwalimu anasikitika kwa kuona pamoja na yeye kuhangaika na chemistry yake katika level ya chini mpaka ya juu ya elimu akiupa ubongo ushike kile kilichoonwa na mwenzie, mwalimu anakuwa mnyonge kabisa kwa kuona hajafanikiwa hata robo kuyafaulu maisha yake. Mwalimu anakutaka upaweke akilini hapa maana tutapaongelea kwa kina katika masomo yajayo yatakayohusu ELIMU katika maisha ambapo mwalimu atatujulisha mengi.

Lakini pia mwalimu aligusia katika somo lilopita kuwa tutajua kwanini mzungu ana jukumu moja na huku wewe mwanadarasa una majukumu matatu katika maisha ni yapi hayo kwa kugusia tu ni kwamba mzungu mfumo alionao tayari ni mfumo unaokiwezesha kila kizazi kinachokuja "huyu aliyepo ni kwa ajili ya yule ajae" hivo huyu aliyepo jukumu lake ni kuandaa kwa ajili ya kizazi kingine kwahiyo nguvu yote itaelekezwa kwa ajili ya kizazi kijacho kwasababu yeye alikwisha andaliwa na kizazi kilichopita lakini huyu mwenye jukumu moja ndiye anaetumia zile 80% za ubongo.

Huku upande wa pili mwanadarasa majukumu yake yakiwa matatu yaani wewe mwanadarasa hapo ulipo jukumu lako la kwanza ni kusaidia kizazi kilichopita hahaha na (na ole wako usisaidie uachiwe laana) jukumu la pili ni kuhakikisha wewe unajimudu au umudu familia yako au kwa lugha nyingine ndo ujiandalie maana haukuandaliwa hahaha (ole wako ushindwe kujimudu ukimbiwe na mke, uchukiwe na ndugu na uwe kero kwa ajili ya shida zako) jukumu la mwisho ukiandalie kizazi chako kijacho watoto wako hahaha (ole wako ushindwe watoto wako waje wauane na kukuombea ufe haraka ili warithi kakibanda kako. Cha ajabu huyu mwanadarasa ndo anatumia 20% ya ubongo wake.
Hivyo tutakuja kupaangalia kwa upana hapa katika mfululizo wa masomo yetu.

Endelea kuhudhuria darasani bila kutoroka.

Pia usisahau ku-subscribe au ni-follow kabisa ili iwe rahisi kwenda sawa.

Ungana nami sehemu ya nne ya somo letu la kwanza


<H.faraday>
 
UZZIMMA

hahahaha umenfanya nicheke mpaka majiran wameskia. Umenkumbusha darasa la kwanza. Nouma sana.
 
Back
Top Bottom