Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Darasa: Chakula cha akili (Mental food)

Somo la pili Sehemu ya pili (lesson two, part two).

Leo mwalimu ameamua kukuletea huu mwendelezo bila kuchelewa akiamini kuwa mwanadarasa una kiu na njaa ya kujifunza mengi.

Katika sehemu hii ya pili ya somo la pili tutaenda kuendelea kuangalia baadhi ya vitu tulivyovianza katika sehemu ya kwanza leo tutaenda kuanza na kundi la kwanza kwenye sababu za kupuuza sauti ya ndani (inner voice).

Sehemu ya kwanza kuna AYA ililitaja kundi hilo la kwanza nayo ilikuwa hivi;

"Kundi hili la kwanza sauti hii inapuuzwa na msingi ambao umemjenga mwanajamii ambao uko juu ya neno KAWAIDA hapa uhusika zaidi na sauti inayohusika na shughuli za kuyajenga maisha zinazomuingizia kipato"

Ni imani ya mwalimu kuwa Aya hiyo unaikumbuka vyema na kama haukumbuki rejea kusoma sehemu ya kwanza ili uweze kwenda sawa na mwalimu.

Hapa tuliongelea kwamba mwanadarasa amejengwa katika msingi ambao shughuli zake azifanyazo kila siku ili aweze kuwa hai (alive) basi shughuli hizo ni zile za KAWAIDA ambazo tayari zipo na zinafanywa katika jamii, au kwa lugha rahisi zinafanywa kwa mazoea au zimezoeleka kufanyika katika jamii, hebu tazama kulia na kushoto mwanadarasa hicho unachokifanya kikoje au nawewe unakifanya kwasababu umekuta kipo kinafanyika? Basi hapo utakubaliana na mwalimu kuwa unalitukuza neno KUIGA kama mwalimu alivyolizungumzia katika masomo yaliyopita, na kwa njia hiyo unazidi kumpa raha SUPERIOR.

Jinsi ya kutoka kwenye huu msingi uliojengeka kwenye neno KAWAIDA au mazoea ni kuiruhusu akili yako iende mbali zaidi kufanya REASONING nje ya zile 20%, kwasababu kuendelea kudumu katika msingi wa neno KAWAIDA au mazoea REASONING inayofanyika hapo ni chini ya 20% kwasababu akili inaenda kwa KUIGA ambapo hapo kutajitokeza neno lingine linaloitwa "ULIZA"

Neno ULIZA ni kijimsingi kidogo ndani ya msingi KAWAIDA kijimsingi hiki kinaenda kinyume na REASONING, wakati kitendo cha reasoning kimesimamia neno KUJIULIZA huu msingi unaenda kijimsingi kinachosimamia neno ULIZA haya ni meneno mawili tofauti ambayo moja linakutaka wewe utumie uwezo wako huku lingine likikutaka utumie uwezo wa mwingine na nirahisi kutumia uwezo wa mwingine kwasababu kitu ni KAWAIDA kimezoeleka hapa ndipo mwanadarasa anapokuwa na utegemezi wa kifikra na utumwa wa kifikra.

Mwalimu anakukumbusha mwanadarasa kuwa mtu tunaemzungumzia hapa ni yule ambae anataka kufaulu maisha kwa njia halali (legal ways) hivyo mwalimu hahusiki na wale ambao kuyamudu maisha ni kwa njia ambazo ziko zaidi ya UBINADAMU.

Kutokana na kuwepo ndani ya msingi KAWAIDA mwanadarasa lazima ufeli maisha, wote unaowaona ambao wako ndani ya msingi huu hawapo hata kwenye 10% ya kufaulu maisha yao mwanadarasa anaweza kuona kuwa mbona wapo ambao wapo kwenye huu msingi ambao wanajishughulisha na ualimu kwasababu walikuta kuna kitu kinachoitwa ualimu au ni polisi kwasababu walikuta kitu kinachoitwa polisi na wana nyumba na usafiri wa kutembelea mwanadarasa ukaona hawa watu wamefaulu,

Mwalimu anakwambia mwanadarasa kuwa hawajafaulu hivyo kipimo cha kufaulu maisha ni nini???..................

Itaendelea

<H.FARADAY> (0625934471)
Tuko pamoja mwalimu.asante
 
Mimi nazidi kukuombea kwa Mungu azidi kukupa afya tele ili uendelee kutupatia elimu. Usisahau kunitag kweny somo lijalo
 
Somo la pili, sehemu ya pili (lesson two, part two) mwendelezo

Leo twendelee kutoka pale tulipoishia sehemu iliyopita ambapo huu ni mwendelezo wa sehemu ya pili katika somo hili la pili.

Lakini kabla ya kwendelea mwalimu anakutaarifu mwanadarasa kuwa mwisho wa kila somo kuna namba ambayo unaweza kuitumia kuwasiliana na mwalimu endapo utakuwa na tatizo binafsi ambalo hutotaka kuliweka hadharani na linalohitaji msaada wa mwalimu.

Twendelee katika sehemu yetu hii ya pili somo la pili tuliishia pale mwalimu aliposema kuwa "mwanadarasa anaweza kujiuliza kuwa mbona kuna watu wapo juu ya msingi wa KAWAIDA lakini wamefaulu maisha kwa maana ya kuwa wana nyumba za kuishi na usafiri wa kutembelea mwalimu akasema la hasha hawajafaulu maisha hata kwa asilimia 20 mwalimu akaacha swali kuwa sasa kumbe kufaulu maisha ni nini??."

Leo tutaenda kupachambua hapa vizuri hivyo umakini wa ziada unahitajika.

Kabla ya kujua kufaulu maisha ni nini na anaposema yule anaefanya kazi kama alivyotoa mifano mwanzo wa sehemu hii ya pili, kwamba iwe ya ualimu au upolisi kwasababu tu amekuta kuna kazi inaitwa hivyo, kwa maana yuko juu ya msingi KAWAIDA na amefanikiwa kujenga na kuwa na usafiri, lakini mwalimu anakwambia bado hajayafaulu maisha twende tukajifunze kitu hiki kwanza.

Mwanadarasa anaweza kujiuliza swali hili kuwa sasa nitafanya nini ambacho kweli kitakuwa cha peke yangu? Mbona kila nikitazama kwenye ubongo naona kuna kitu lakini hiki kitu tayari kinafanyika katika jamii nitakitoa wapi cha peke yangu? Kwamba hiki kitu kweli ninachokiona ni sahihi au si sahihi niendelee kukitafuta kwenye ubongo??.

Hapana huenda hicho ulichokiona japokuwa tayari kinafanyika katika jamii kikawa sahihi, lakini utofauti utakuja katika namna ya ufanyaji, kuna vitu ambavyo tunaviita mizizi na wanaobahatika kuikita ardhini hii mizizi huwa katika kundi tofauti, huwa wanacho kingine cha ziada mbali na kuwa na kitu cha tofauti hawa watu kwa lugha iloyozoeleka wanaitwa (majiniasi), wachache wanakuwa na uwezo huo wa ziada na mara nyingi hawa ndio wanaokuja kuwa waasisi wa shughuli mbalimbali tunazozifanya katika jamii.

Mizizi hiyo ni nini? Katika shughuli yoyote ifanyikayo ni lazima iwe na mzizi au chimbuko, mpaka kikaitwa kilimo cha mahindi kuna aliyesababisha mpaka kikaitwa hivyo, aliyesema hiki kiitwe kilimo cha mahindi ndiye aliyekita mzizi huo ardhini, baada ya mzizi huo kuwekwa ndipo watu wengine hujaa hapo kuunda shina, hapa sasa kila mtu ataangalia kwenye ubongo wake ataona kitu tofauti na wenzake kutoka kwenye hilo shina walipolundikana huku wakishikiliwa na mzizi huo, baadae huyu/hawa walioona kitu tofauti kutazaliwa kitu kinachoitwa matawi, hapa kwenye matawi ndipo mwingine ataamua kuweka tu mbegu ardhini akaenda zake kisha aje avune gunia 1 hilo ni tawi pia, mwingine ataamua kumwagilia apate gunia 10 nae ni tawi tofauti, tawi lingine litaamua kuweka mbolea apate gunia 30 na matawi mengine.

Mfano wa mzizi wa pili kuna mtu alikita ardhini mzizi wa kufuga ng'ombe, watu wakajua kuwa kumbe kuna kitu kinachoitwa kufuga ng'ombe, vivyo hivyo watu wengine wakaja kulundikana kwenye shina baada ya hapo kukaanza kutokeza matawi, tawi moja likaenda mbali zaidi kuwa huyu ng'ombe siyo kwamba alishwe tu majani bali aongezewe pumba na mashudu pamoja na madini ili atoe lita 20 kwa siku, tawi lingine likaona kwenye ubongo wake kuwa mbona wote kwenye shina tupo kwa ajili ya maziwa? Hili tawi likaenda mbali zaidi kwa kuona kuzalisha SAMADI ni bora zaidi nalo likawa tawi la pili na matawi mengine ambayo mwanadarasa yatakujia kichwani.

Hivyo siyo tu kwenye kilimo ama ufugaji bali nyanja zote iwe biashara, iwe ni uongozi serikalini kuna mizizi na waasisi wa hiyo mizizi na pia kuna matawi, shina huwa ni kokoro linazoa kila aina ya binadamu lakini matawi yatatofautiana, hivyo utaona tawi lingine lina rangi nzuri ya kijani huku lingine likiwa limenyauka.

Kwa maana hiyo kuona ndani ya ubongo wako kitu ambacho tayari kinafanyika kisikuogofye ndo maana huyu jamaa anaeitwa bill gates anasema "if you can't make it good, at least make it look good" tutaona tawi lako linachanua vipi, je litakuwa na afya nzuri ama na afya mgogoro? Kutokana na utofauti wa kile mtu atakachokiona ndanI ya ubongo wake ndicho kitakacholeta utofauti wa muonekano wa matawi. Kuweza kuona mzizI na ukaukita ardhini hapa sasa ndipo unapovuka mipaka ya mwanajamiI wa Tanzania, mwanajamiI wa Afrika na kuwa katika level moja na SUPERIOR, usije ukachanganya siyo kila aliye nje na Tanzania, ama Afrika basi ni SUPERIOR la hasha yeye ni kuwa tu yuko jirani na SUPERIOR kuliko wewe hivyo ataiga kwa kasi kuliko wewe hivyo hata kufeli kwake kwa maisha kutakuwa na asilimia ndogo zaidi.

Mwalimu anaendelea kusema kuwa na uhakika wa kula, kulala au labda na usafiri huko siyo kufaulu maisha kwasababu mpaka uwe umeyaanza kuyafaulu maisha inatakiwa ufikie ngazi ya tatu ambayo ni kuwa HAI (being alive), lakini unapokuwa na hvyo vitu ni umeanza kuigusa kidogo ngazi ya pili ambayo ni ISHI (living) umetoka kidogo tu kwenye ngazi ya kwanza ambayo inahusisha vitu vinavyokufanya uendelee kuliona jua ngazi hii ya kwanza inayoitwa KUWEPO (existing). Hivyo huyo mtu atakuwa kwenye kundi ambalo lina vyanzio vya kuweza kusonga mbele zaidi katika safari ya kuyafaulu maisha yake japo hatafikia akayafaulu kwa 100% usimuulize mwalimu lakini hapa ndipo wanafizikia wanasema "efficiency is less than 100%" kwanini tunaviita vyanzio kwasababu swala la nile nini halitakuwepo hivyo ataifanya REASONING yake iende kwenye mambo makubwa.

Hivyo huyu anafanya kazi ya ualimu au polisi kama mifano yangu ilipojikita kumiliki hivyo nilivyovitaja ni moja ya mahitaji yake ambayo kidogo yanamsogeza katika ngazi ya pili na huyu anaeweza kumudu hivi ni yule ambae ameutumia mzizi wa ualimu ama upolisi kutengeneza tawi lake na siyo yule anaefanya kwasababu amekuta kuna kitu kinaitwa hivyo au kwasababu ndo sehemu pekee iliyokuwa na nafasi au ndo sehemu pekee aliyokuwa na vigezo "do things not by chance but by choice" kwasababu mshahara wa laki 5 mpaka million moja utakufanya ujimudu wewe tu kitu ambacho ni kuhakikisha uwepo wako tu duniani (existing). Kumbuka kigezo kingine kikubwa cha dalili ya kuanza kuyafaulu maisha;

Ni kuweza kujimudu na kumudu jamii (society) inayokuzunguka, bila kuharibu mfumo mzima wa kuyaendesha maisha yako wewe binafsi na hauitwi mtu pasipo jamii na jamii inaundwa na msingi wa neno unaoitwa mahusiano (interrelation) na jamii ya kwanza ni ukoo wako wewe. Ndio maana SUPERIOR anaweza kukupa msaada wewe wa kiasi chochote.

Tukutane sehemu ya tatu ya somo hili la pili


<H.FARADAY> (0625934471).
 
Samahan mwalimu kwenye somo la pila title zote zimeandikwa lesson two inaweza changanya watu

makinikia
 
Mwalimu kuna sehemu umesema utegemezi wa kifikra na utumwa wa kifrika lakina kwenye maisha kuna kitu kinaitwa kushare idea unakizungumziaje?

makinikia
 
Asante sana mwalimu. Nahisi mimi ni muhudhuriaji namba moja wa darasa!
Mwalimu anakupongeza kwa hilo endelea kukaa dawati la mbele, akitaka kuchagua monita wewe hata kusahau pia usisahau kumtafuta kwa namba hiyo kwa masomo yatakayokuwa yanaendelea whatsap.

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu kuna sehemu umesema utegemezi wa kifikra na utumwa wa kifrika lakina kwenye maisha kuna kitu kinaitwa kushare idea unakizungumziaje?

makinikia
Angalau mwalimu anafurahi kupata maswali ya akili kidogo kutoka kwa mwanadarasa wake anaukumbuka msemo wa mwanafilosofia mmoja anaeitwa "Voltaire" <anakwambia judge man by his questions rather than his answers>.

Tunapozungumzia neno UTEGEMEZI ina maana huwezi kufanya kitu fulani pasipo msaada wa kitu au mtu fulani, utegemezi wa kifikra hauwezi kufanya maamuzi kwa fikra zako mwenyewe isipokuwa fikra za mtu fulani, unaposema "utumwa" ni pale unapolazimika kufanya kitu kama agizo (command) pasipo uhuru binafsi.
Utumwa wa kifkra, fikra zako zinakuwa na utumwa wa kukuruhusu kufanya maamuzi bila zenyewe kuhusika mchango wake kwasababu unatumia fikra zingine hivyo za kwako kukosa uhuru.

kila binadamu anazaliwa akiwa na ubongo mweupe kujaa kwa ubongo kunatokana na neno kujifunza, na ulikosema ku-share ideas ni msingi wa kuongeza ufahamu na si msingi wa kuongozwa kufanya maamuzi, kwasababu mpaka unasema tuna-share ni kwamba tayari kuna kitu niko nacho hatakama ni kidogo pengine kinahitaji maelezo zaidi au sikijui kama ni sahihi hivyo nitaenda kujifunza, na maamuzi yatakayopatikana pale si fikra za mtu hapana ni fikra zangu zilizoboreshwa.

All the best katika kulielewa hilo.

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu nimekuelewa sana

makinikia
You're welcome.
Pia usisahau kuivaa hiyo namba mwisho wa somo kwa ajili ya masomo mengine yatakayokuwa yanaendelea whatsap.

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
 
You're welcome.
Pia usisahau kuivaa hiyo namba mwisho wa somo kwa ajili ya masomo mengine yatakayokuwa yanaendelea whatsap.

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
Ngoja niichukue ilitubonge kwa undan

makinikia
 
Ahsante mwalimu nipo dawat la mbele nakusubiri
 
Mwalimu nimekuelewa sana ulipogusia kuhusu haya maneno matatu
Uwepo(existing)
Ishi(living)
Hai(being alive)
Kama nakumbuka vizuri maneno Haya yanategemeana sana kutoka kwenye hatua ya uwepo (existing) na ili uendelee kuwepo ni lazima uishi na kuishi ulikokuelezea wewe ni kupata mahitaji ya msingi yatakayokufanya uendelee kuwepo kitu ambacho wengi wetu tunaridhika tunapofikia katika hatua hii

Lakini pia mwalimu ukasema unaweza kwenda mbali zaidi na ukawaida kwamba kufanikiwa kimaisha si kwa kuwa unaweza kupata mahitaji yale unayoyaona kwako ni ya msingi peke yake hapana bali unapotazamia namna ambavyo unaweza kuikomboa jamii yako kiujumla pasipo ww kuathirika au kuteteleka kiuchumi

Swali langu lipo kwenye mtazamo wa kwamba endapo mtu huyu ana uwezo wa kuisaidia jamii inayomzunguka pasipo kuathiri mfumo mzima wa maisha yake na umesema kuwa jamii hyo inaanzia kwenye ukoo wangu
Kwa nn tusimuite mtu huyu amefanikiwa maisha kwa 100%
Yaan kwa lugha rahisi ameweza kufika katika kiwango cha yye kuweza kuitwa SUPERIOR

Asante
Vizy boy

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom