Somo la pili, sehemu ya tano (Lesson two part five) Mwendelezo.
Kengele imegongwa tayari baada ya mapumziko turejee tena katika kuiangalia sehemu yetu hii ya tano ya somo hili la pili ukiwa ni mwendelezo.
Tuliishia njia ya kwanza ya kusafisha ubongo na akili hivyo twendelee na njia ya pili.
NJIA YA PILI
JISAMEHE MWENYEWE.
Moja ya mzigo mzito ambao moyo, nafsi na ubongo wako unabeba ni
HUKUMU ya ndani inayokupelekea ujione mwenye
HATIA juu ya hali ya maisha uliyonayo na juu ya hali ya maisha uliyopitia. Na tena kabla ya kuzama ndani zaidi anza kwa kujisamehe kwa kutokuijua elimu hii, mwingine atajilaumu kwanini asingeyasoma yote haya kungali mapema. Mwalimu anakwambia huu ndio muda wako muafaka wa wewe kuyajua haya, kama haitakuwa juu ya faida yako basi itakuwa juu ya jamii yako inayokuzunguka.
Kuna huyu mzee mwenzangu anasema;
Hivyo usijihukumu kwa hili pia. Kujiona mwenye hatia juu ya hali ulizopitia katika maisha yako kunakuja baada ya mengi uliyoyafanya na matokeo yake yakawa ndivyo sivyo, Unawaza jinsi ulivyoianza biashara flani lakini mwisho wa siku ukaporomoka mpaka kuja kula mtaji na sasa umebaki hauna kitu, sura inaonesha tabasamu mchana lakini usiku ukizima taa basi unayawasha mawazo mpaka asubuhi huku swali kichwani likiwa kwanini sikufanya vile? Kwanini sikutumia njia ile?
Huku unasahau kuwa kabla ya kufanya ile biashara ulikuwa na dhamira njema, ukiomba kabisa na Mungu akusaidie uweze kuinuka katika maisha kupitia biashara ile, lakini ukasahau jambo moja kuwa
DHAMIRA na
MATOKEO ni vitu viwili tofauti, unatamani siku zirudi nyuma uanze upya, unaishia kujitupia lawama za kuona matokeo uliyoyapata ni
UZEMBE.
Mwalimu anakuweka sawa juu ya neno uzembe, ni pale unapofanya jambo unalolielewa vyema bila ufasaha wake kwa mfano najua kabisa ili niweze kuvuna mazao yanipasa kuweka mbolea ya kukuzia lakini endapo sitaiweka, siku nikija kupata mazao hafifu kwasababu sikuweka hiyo mbolea ni
UZEMBE haijalishi nilishindwa kuweka kwasababu gani.
Tofauti na hapa mwanadarasa anapojiona mzembe kwa kitu ambacho alitumia akili yake yote, maarifa ufahamu na nguvu zake zote katika kufanya kitu hicho, lakini kikaja kuleta majibu
HASI huo sio uzembe bali ndipo
UBONGO wako ulipoishia kusukuma kiwango cha akili iliyotumika katika kutekeleza kitu hicho. Hivyo hupaswi kujihukumu na kujiona mwenye hatia kwa kitu ambacho ulikifanya kwa
DHAMIRA nzuri halafu kikaleta majibu hasi.
Nini ambacho ulitakiwa kukifanya ni hiki, kuna Dr mmoja anaitwa Dr.Seuss anasema
“Don’t cry because it’s over, but smile because it happened” usilie kwasababu unaona ndo mwisho, mambo yote yameharibika laah bali tabasamu kwasababu tayari yamekwishatokea.
Kuna njia mbili za kujifunza.
Njia ya kwanza kwa kuona, kwa kuuliza, kwa kuelekezwa, kwa kusikia na kwa kila aina ya kutumia milango yako ya fahamu ikiwa na maana yote ya kujifunza kitu kwa kupata usaidizi wa nje (
external support).
Njia ya pili na ndo njia iliyobora na ndo njia inayokuja kuleta hukumu na hatia ndani yako ni njia ya
JARIBIO, njia hii inahusisha “uhusika wa wewe mwenyewe katika kutekeleza kujifunza” na kupata msaada mdogo kutoka nje hapa ndo ambapo mtu anapoingia kwenye biashara kama ni ya nguo atakachohitaji msaada ni kuelekezwa kuwa sehemu gani atapata nguo za jumla lakini shughuli zingine zote zinazofuata zinakuwa juu yake, yeye ndo atajua nguo hii nilinunua elfu kumi hivyo mimi niuze elfu 15. kwanini tunaita jaribio ni kwasababu kitu chochote unapokifanya kwa mara ya kwanza linakuwa ni jaribio.
Kwamba una nadharia kichwani kwamba hiki kitu kinaenda hivi na hivi wana kemia wanaita (
hypothesis formulation) lakini je ni kweli kiko hivo? Hivyo kukifanya ndo jaribio lenyewe ambapo utakuja kujua kama uko sahihi au hapana. Sasa basi kuwa makini hapa matokeo yoyote ya jaribio lako huwa ni njia ya kujifunza haijalishi matokeo ni mabaya ama mazuri, hapa ndipo unapokuja kujifunza kwa kitu tunachoita UZOEFU (
experience).
Tatizo la mwanadarasa endapo matokeo yatakuja mabaya basi huwa ndo mwisho wa safari, mwalimu anakwambia hilo ndo kosa kubwa, yani unaacha kitu baada ya kukijua unapata hofu ya kukifanya tena baada ya kukijua na huku ulikifanya kwa ujasiri kabla ya kukijua inachekesha sana. Ndio maana katika kujutia kwako au kujilaumu kwako unazungukwa na mawazo ya kwanini nimefanya hivi na kwanini sikufanya vile lakini unasahau kuwa umezijua njia hizo kwasababu yametokea.
Unapishana na mavuno mwanadarasa, nini unatakiwa kufanya msikilize huyu jamaa anaeitwa Joseph Campbell anasema “we must let go of the life we have planned, so as to accept the one that was waiting for us” tuyaruhusu yale matokeo yetu yaliyotupata, tuyaache yaende maana yale ndiyo tuliyokuwa tumejipangia lakini kuna uhalisia wa jambo ambao ulikuwa unatusubiri lakini ulituhitaji tungali tumejifunza tayari. Sio huyo tu kuna huyu jamaa mwingine anaeitwa Thomas A. Edson mgunduzi wetu wa bulb anasema;
“Our greatest weakness lies in giving up, the most certain way to succeed is always just to try one more time” udhaifu wetu mkubwa ni kukubali kushindwa lakini njia ya mafanikio pasi na shaka ni kujaribu kwa mara nyingine tena.
Mwalimu anakwambia usijione mwenye hatia wala kujihukumu jisamehe jione uko huru akili ipate uhuru wa kuwaza njia bora ambazo ni zaidi ya zile ulizokwishazitumia. Kwendelea kujiona mwenye hatia ni kuzidi kupunguza muda wa akili nyingi kuelekezwa kwenye ufumbuzi kwasababu majuto sio tiba hata hivyo.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa.
Tuonane kwenye njia ya tatu na ya mwisho.
USISAHAU KUMCHEKI MWALIMU KWA NAMBA YAKE AKUWEKE KATIKA LIST.
<H.FARADAY> (0625934471).