duh, hawa wachina wanatisha jamani, mwaka jana kwenye shanghai expo nilitembelea daraja refu sana lililoko shanghai. daraja lile linaingia baharini kiasi kwamba linaenda hadi zaidi ya upeo wa macho! wakati ule wenyeji wangu waliniambia kuwa ndilo daraja refu kuliko yote duniani! kwangu ilikuwa ni maajabu makubwa kushuhudia katika sekta ya miundombinu, pia kuna shanghai financial centre ina majengo marefu kuliko sehemu nyingine yoyote duniani! sasa kwa hili la qingdao, hakika hapa wamekufuru kabisa!!
hongera zao wenye akili, sie na magamba yetu??!!
tutajibeba!!
Nakuhakikishia majamaa ya nchi hii yapo yapo tuu, yaani ukiwakuta wanavyoshangaa wakitoka nje na wanavyolalamika basi mlala hoi Kama sisi hutalalamika tena wala hutatarajia watafanya kitu chochote na wala usiwategemee kwa sababu wabalalamika kuliko hata mlala hoi.Ndio Viongozi wetu hawa.hivi haya majaaa hawayaoni hayo madaraja.....ktk hizo picha angalau kidogo waigi
mkuu....sisi na china wapi na wapi mkuu...
wasikililize waheshimiwa hapo mjengoni wanavyoteteana kwa kulala badili ya kuwawakilisha wenyenchi...unadhani tutafika kwa namna hiyo kweli!!!???
sisi tuhangaike tu na kikombe cha babu huko loliondo, walau huku tabora kikombe cha bibi kime-expire pengine watu watakuwa na akili ya kufikiri namna ya kubadili maisha yao na siyo kutegemea miujiza ya kikombe..yale yale ya mwenge kuleta maendeleo!!!
huwa najiuliza hivi hao waliondelea wana mienge mingapi???!!!!!
kweli mkuu, yaani sisis ni kikombe tuu na ngoka eleven
Hivi mkulu huwa anaona mambo haya!?