Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,346
- 9,889
Bado anaonyesha chuki zake kwa watu wa kigamboni..inaonekana hakufurahia wapate daraja.Aliisha waambia asie kuwa na mia mbili apige mbizi..! Haijalishi ni mzee au mama mjamzito!
Watanzania tunapenda sana kuchonganisha! Ametoa mfano tu sio lazima Tuka link na daraja la kigamboni! Pia nimeanza kumuelewa JPM kuwa huwa hana selection nzuri ya maneno au mifano! Inaoneka hiyo mifano huwa hajaandika kwenye notes zake!
Kwa kweli kwenye swala hili mimi naungana na maghufuli, maana tuna tuna mgodi wa chuma kwanini tusijenge kiwanda ambacho kita process hayo madini mpaka kupata chuma pure, ambapo kiwanda kitakuwa na wafanyakazi si chini ya 1000, huku mgodi ukiwa na wafanyakazi si chini ya 1000, kwanza kama mfuko wa Jamii wale wafanyakazi anawafanya wanachama wake pili kiwanda badala ya kusafirisha madini ya chuma tunatengeneza chuma kabisa na kuongeza thamani, shaba toka Zambia na Congo zinapita hapa kwa nini tusitengeneze vinu vya Ku process hiyo shaba tukaanza kusafirisha waya na vipuri vingine badala ya kusafirisha shaba, kwanini tusijenge kiwanda cha kutengeneza vioo vya simu ili tusipeleke mchanga wa mabaki ya dhahabu ulaya?, kwanini wasiwekeze kiwanda cha matairi ili tuiuzie serikali na wananchi binafsi matairi huku tuwapa wakulima wetu soko la uhakika la zao la mpira
Hivi rafiki yako akisema anajenga kibanda Kinyerezi unamuelewaje?Nimesikia kauli ya JPM katika sherehe za Mei Mosi akisema kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikijiingiza kuwekeza katika miradi ya ajabu ajabu. Akaendelea kushangaa kuwa badala ya kuwekeza katika viwanda vitakavyotoa ajira nyingi zitakazotengeneza wanachama wengi zaidi wa mifuko hiyo, unakuta eti mfuko unawekeza katika ujenzi wa daraja au karavati!
Najaribu kujiuliza tu, ni mfuko gani wa hifadhi ya jamii uliowekeza katika ujenzi wa daraja au karavati kiasi cha kumshangaza rais? Haya sasa, mimi nawaachia mjadala
cc Mohamed Said, Ritz, FaizaFoxy, AbasMzeEgyptian
Watanzania tunapenda sana kuchonganisha! Ametoa mfano tu sio lazima Tuka link na daraja la kigamboni! Pia nimeanza kumuelewa JPM kuwa huwa hana selection nzuri ya maneno au mifano! Inaoneka hiyo mifano huwa hajaandika kwenye notes zake!
Kama umemsikiliza mkuu ameongea jambo zuri sana hii mirad ya majengo inakua na upigaj mkubwa sana , lakn kama wataanzisha viwanda kutakua na manufaa tena ya muda mrefu na wanufaika wengi sana
Daraja la kigamboni ni karavati kubwa!! Limejengwa kwa hela za wastaafu. Zitalipwaje? Mimi najiuliza hili swali kila siku. Ujenzi wa daraja kawaida inatakiwa iwe social service. Sasa ili zirudi wanataka kutoza naui ya kupita darajani hapo. Wenye magari wakibadili route badala ya kupita darajani hizo hela watazipataje? Tuna hakika gani kuwa watakaokusanya hizo hela wataziwasilisha asilimia mia? Za kivuko cha ferry tu zinaibiwa. Hizo hela haziwezi kurudi ndani ya miaka kumi ambayo tutakuwa naye raisi makini hivyo mimi naona ni ndoto kujenga karavati kwa hela za wastaafu. Ni kosa kubwa, na inawezekana balozi to be asipangiwe kituo. Actually alichosema raisi ni ukweli usiopingika.Nimesikia kauli ya JPM katika sherehe za Mei Mosi akisema kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikijiingiza kuwekeza katika miradi ya ajabu ajabu. Akaendelea kushangaa kuwa badala ya kuwekeza katika viwanda vitakavyotoa ajira nyingi zitakazotengeneza wanachama wengi zaidi wa mifuko hiyo, unakuta eti mfuko unawekeza katika ujenzi wa daraja au karavati!
Najaribu kujiuliza tu, ni mfuko gani wa hifadhi ya jamii uliowekeza katika ujenzi wa daraja au karavati kiasi cha kumshangaza rais? Haya sasa, mimi nawaachia mjadala
cc Mohamed Said, Ritz, FaizaFoxy, AbasMzeEgyptian
Hilo karavati halina shida. Alichosema raisi ni fedha za ujenzi wake hazitakiwi kutoka kwenye mifuko ya hifadhi za jamii. Hiyo mifuko inatunza fedha za wastaafu lazima fedha ziwekezwe kwenye miradi itakayorudisha fedha na kupata faida. Ukipiga hesabu hilo daraja ni ndoto kwamba fedha zake zitarudi. Kuna wastaafu ambao wanaweza kukosa fedha zao muda ukifika. Hiki ndicho alichomaanisha. Karavati lenyewe halina shida litasolve tatizo la wana kigamboni. Swali ni je fedha za watu zitarudi?Kama ndio hivombona ,alikuwa aanasifia hilo KKaravati la KKigamboni
Na kwa kuongezea fedha za wastaafu zitarudi. Raisi yuko sawa kabisa.Kwa kweli kwenye swala hili mimi naungana na maghufuli, maana tuna tuna mgodi wa chuma kwanini tusijenge kiwanda ambacho kita process hayo madini mpaka kupata chuma pure, ambapo kiwanda kitakuwa na wafanyakazi si chini ya 1000, huku mgodi ukiwa na wafanyakazi si chini ya 1000, kwanza kama mfuko wa Jamii wale wafanyakazi anawafanya wanachama wake pili kiwanda badala ya kusafirisha madini ya chuma tunatengeneza chuma kabisa na kuongeza thamani, shaba toka Zambia na Congo zinapita hapa kwa nini tusitengeneze vinu vya Ku process hiyo shaba tukaanza kusafirisha waya na vipuri vingine badala ya kusafirisha shaba, kwanini tusijenge kiwanda cha kutengeneza vioo vya simu ili tusipeleke mchanga wa mabaki ya dhahabu ulaya?, kwanini wasiwekeze kiwanda cha matairi ili tuiuzie serikali na wananchi binafsi matairi huku tuwapa wakulima wetu soko la uhakika la zao la mpira
Kuna tetesi kuwa hakukubaliana na uwekezaji huo ila nguvu za ziada ndiyo zilipitisha mradi huo.Ni kweli daraja limejengwa ila ni nani ajuaye yaliyo nyuma ya pazia. Mkuu akiwa Waziri ni kweli alikubali kwa moyo huo uwekezaji au kulikuwa na nguvu nyingine. Anayeijua Siri hii ni wako watatu...!
Kuna tetesi kuwa hakukubaliana na uwekezaji huo ila nguvu za ziada ndiyo zilipitisha mradi huo.
Kabisa mkuu. Huyu ni raisi wa kweli wa watanzania. Anatushushua tuliodhani mfumo utamdhibiti. Ni mkweli na haogopi kusema ukweli. Tumuombee sana.Kama ndivyo basi kauli iliyotolewa si kitu cha ajabu, tuendelee kumuombea Rais wetu....!
Tena kuna tetesi kuwa wanataka kuliuza ili fedha zirejeshwe. Tatizo hawa wakubwa wakipewa dhamana ya kutunza fedha zetu wanzifanya ni zao. Sasa tukistaafu tutalipwaje? Very poor investments tena na wasomi wetu wanaojua.Nimesikia leo Machinga Complex itachukua miaka 475 kwa deni la NSSF kulipwa!
Pia Ujiulize Serikali kuu yenye Kodi na vyanzo vyote vya mapato imeshindwa kuanzisha hivyo viwanda Pension Fund itawezaje?
Pili fedha za Mfuko wa hifadhi ya jamii ni fedha za watu walioweka akiba yao wakistaafu wanataka wakute pesa yao sio longolongo sasa inakufanya Investment hakikisha unachagua investment yenye low risk kama vile daraja ukija ku invest kwny high risk bsn ukipata hasara utawaeleza lugha gani members wakuelewe?
Mbona wastaafu wanatembea mpaka soli ya kiatu inapinda!! Ndio kupata hela kwa uhakika