Daraja la NSSF Kigamboni ndio karavati?

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
22,569
23,450
Nimesikia kauli ya JPM katika sherehe za Mei Mosi akisema kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikijiingiza kuwekeza katika miradi ya ajabu ajabu. Akaendelea kushangaa kuwa badala ya kuwekeza katika viwanda vitakavyotoa ajira nyingi zitakazotengeneza wanachama wengi zaidi wa mifuko hiyo, unakuta eti mfuko unawekeza katika ujenzi wa daraja au karavati!

Najaribu kujiuliza tu, ni mfuko gani wa hifadhi ya jamii uliowekeza katika ujenzi wa daraja au karavati kiasi cha kumshangaza rais? Haya sasa, mimi nawaachia mjadala
cc Mohamed Said, Ritz, FaizaFoxy, AbasMzeEgyptian
 
Hiyo sentensi ya mwisho CC ndiyo imenivunja mbavu, Yaani FaizaFoxy utamuona soon hapa jamvini na ujiandae.Aisee nashindwaga kujua amejitendenezea software ambayo ameintegrate na JF kuwa akitajwa tu imualert. Ukiangalia na ukimsikiliza vizuri Raisi utagundua alilenga mfuko gani wa jamii, ni wazi aliulenga mfuko wa NSSF na alilenga daraja la kigamboni aliloagiza lipewe jina la Mw.Nyerere.Na ukiwa mzalendo wa kweli Raisi yuko sahihi kabisa.Watu wamekazana kuwekeza kwenye madaraja na majengo ambayo return yake ni ndogo wanacha kuwekeza kwenye viwanda na miradi ambayo itainua uchumi wa nchi kwa haraka na kutoa ajira nyingi za kudumu kwa vijana. Ila hii miradi ya maraja,makalavati na majendo ina ulaji wa maana sana.
 
kicheko hapa jamani, eti karavati do!!
Japo kuna ukweli kidogo hapo.
 
Ni vizuri kuwatia moyo waliothubutu na kuwatia moyo kufanya zaidi...maana ni lazima pawepo pa kuanzia. Tunajifunza kwa makosa. Naona Mheshimiwa Rais hapa amefungua mlango mpana sana na wa kufaa. Sheria na taratibu ziangaliwe ili ku accomodate wazo hili jema na jipya.
 
Ni kweli daraja limejengwa ila ni nani ajuaye yaliyo nyuma ya pazia. Mkuu akiwa Waziri ni kweli alikubali kwa moyo huo uwekezaji au kulikuwa na nguvu nyingine. Anayeijua Siri hii ni wako watatu...!
 
Watanzania tunapenda sana kuchonganisha! Ametoa mfano tu sio lazima Tuka link na daraja la kigamboni! Pia nimeanza kumuelewa JPM kuwa huwa hana selection nzuri ya maneno au mifano! Inaoneka hiyo mifano huwa hajaandika kwenye notes zake!

unajua watu wengine wanaposikiliza hotuba kazi yao ni kutafuta la kukosoa tu, hawana shida na ujumbe uliolengwa. tuwavumilie tu
 
unajua watu wengine wanaposikiliza hotuba kazi yao ni kutafuta la kukosoa tu, hawana shida na ujumbe uliolengwa. tuwavumilie tu
Mimi sijakosoa hotuba, isipokuwa nimenukuu kile alichosema JPM bila kutia chumvi, then nikakaribisha mjadala kuhusu kusudio lake. Kama kuna kitu unadhani sikunukuu vyema unaweza ukanionyesha, nitarekebisha.
 
Mmh, hilo la kuanzisha viwanda bila utaalam/wataalam na utaalam wa usimamiz nalo ni tatizo kubwa. Ni afadhali kujifunza na kujenga uwezo kabla ya kuingia huko!
 
Mmh, hilo la kuanzisha viwanda bila utaalam/wataalam na utaalam wa usimamiz nalo ni tatizo kubwa. Ni afadhali kujifunza na kujenga uwezo kabla ya kuingia huko!
Anetolea mfano wa viwanda vya ngozi na viatu. Je, navyo tutahitaji wataalamu wengi wa nje?
 
Watanzania tunapenda sana kuchonganisha! Ametoa mfano tu sio lazima Tuka link na daraja la kigamboni! Pia nimeanza kumuelewa JPM kuwa huwa hana selection nzuri ya maneno au mifano! Inaoneka hiyo mifano huwa hajaandika kwenye notes zake!

kweli tusichonganishe hapa!
 
Kwa kweli kwenye swala hili mimi naungana na maghufuli, maana tuna tuna mgodi wa chuma kwanini tusijenge kiwanda ambacho kita process hayo madini mpaka kupata chuma pure, ambapo kiwanda kitakuwa na wafanyakazi si chini ya 1000, huku mgodi ukiwa na wafanyakazi si chini ya 1000, kwanza kama mfuko wa Jamii wale wafanyakazi anawafanya wanachama wake pili kiwanda badala ya kusafirisha madini ya chuma tunatengeneza chuma kabisa na kuongeza thamani, shaba toka Zambia na Congo zinapita hapa kwa nini tusitengeneze vinu vya Ku process hiyo shaba tukaanza kusafirisha waya na vipuri vingine badala ya kusafirisha shaba, kwanini tusijenge kiwanda cha kutengeneza vioo vya simu ili tusipeleke mchanga wa mabaki ya dhahabu ulaya?, kwanini wasiwekeze kiwanda cha matairi ili tuiuzie serikali na wananchi binafsi matairi huku tuwapa wakulima wetu soko la uhakika la zao la mpira
 
Anetolea mfano wa viwanda vya ngozi na viatu. Navyo tutahitahi wataalamu wengi wa nje?
Sawa, je utafiti wa masoko. Halafu usichukulie suala jepesi kwa kuwa ni kiwanda cha ngozi, je kina tija? Soko lipo? Return? So kuna mengi ya kujiridhisha, tusije kuangukia tulipoteleza awali.
 
Kama umemsikiliza mkuu ameongea jambo zuri sana hii mirad ya majengo inakua na upigaj mkubwa sana , lakn kama wataanzisha viwanda kutakua na manufaa tena ya muda mrefu na wanufaika wengi sana
....

.....tuna safari ndefu sana
 
Nimesikia kauli ya JPM katika sherehe za Mei Mosi akisema kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikijiingiza kuwekeza katika miradi ya ajabu ajabu. Akaendelea kushangaa kuwa badala ya kuwekeza katika viwanda vitakavyotoa ajira nyingi zitakazotengeneza wanachama wengi zaidi wa mifuko hiyo, unakuta eti mfuko unawekeza katika ujenzi wa daraja au karavati!

Najaribu kujiuliza tu, ni mfuko gani wa hifadhi ya jamii uliowekeza katika ujenzi wa daraja au karavati kiasi cha kumshangaza rais? Haya sasa, mimi nawaachia mjadala
cc Mohamed Said, Ritz, FaizaFoxy, AbasMzeEgyptian
Ni ngumu sana kumuelewa huyu Rais wetu. Mwanzo alisifia, sasa anaponda. Ni kigeugeu.
 
Back
Top Bottom