Daraja la NSSF Kigamboni ndio karavati?

Daraja la NSSF Kigamboni ndio karavati?

Nimesikia kauli ya JPM katika sherehe za Mei Mosi akisema kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikijiingiza kuwekeza katika miradi ya ajabu ajabu. Akaendelea kushangaa kuwa badala ya kuwekeza katika viwanda vitakavyotoa ajira nyingi zitakazotengeneza wanachama wengi zaidi wa mifuko hiyo, unakuta eti mfuko unawekeza katika ujenzi wa daraja au karavati!

Najaribu kujiuliza tu, ni mfuko gani wa hifadhi ya jamii uliowekeza katika ujenzi wa daraja au karavati kiasi cha kumshangaza rais? Haya sasa, mimi nawaachia mjadala
cc Mohamed Said, Ritz, FaizaFoxy, AbasMzeEgyptian
Hata Mimi nimesikia alipokuwa anazungumzia hoja ya "hifadhi ya jamii "kuwa mifuko ya jamii iwekeze ktk viwanda ili kuzalisha ajira sio kukalia kutengeneza Makaravati tu. Nikajua Nyerere bridge is now a karavati
 
Nimesikia kauli ya JPM katika sherehe za Mei Mosi akisema kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa ikijiingiza kuwekeza katika miradi ya ajabu ajabu. Akaendelea kushangaa kuwa badala ya kuwekeza katika viwanda vitakavyotoa ajira nyingi zitakazotengeneza wanachama wengi zaidi wa mifuko hiyo, unakuta eti mfuko unawekeza katika ujenzi wa daraja au karavati!

Najaribu kujiuliza tu, ni mfuko gani wa hifadhi ya jamii uliowekeza katika ujenzi wa daraja au karavati kiasi cha kumshangaza rais? Haya sasa, mimi nawaachia mjadala
cc Mohamed Said, Ritz, FaizaFoxy, AbasMzeEgyptian
Hata Mimi nimesikia alipokuwa anazungumzia hoja ya "hifadhi ya jamii "kuwa mifuko ya jamii iwekeze ktk viwanda ili kuzalisha ajira sio kukalia kutengeneza Makaravati tu. Nikajua Nyerere bridge is now a karavati
 
Kwa kweli kwenye swala hili mimi naungana na maghufuli, maana tuna tuna mgodi wa chuma kwanini tusijenge kiwanda ambacho kita process hayo madini mpaka kupata chuma pure, ambapo kiwanda kitakuwa na wafanyakazi si chini ya 1000, huku mgodi ukiwa na wafanyakazi si chini ya 1000, kwanza kama mfuko wa Jamii wale wafanyakazi anawafanya wanachama wake pili kiwanda badala ya kusafirisha madini ya chuma tunatengeneza chuma kabisa na kuongeza thamani, shaba toka Zambia na Congo zinapita hapa kwa nini tusitengeneze vinu vya Ku process hiyo shaba tukaanza kusafirisha waya na vipuri vingine badala ya kusafirisha shaba, kwanini tusijenge kiwanda cha kutengeneza vioo vya simu ili tusipeleke mchanga wa mabaki ya dhahabu ulaya?, kwanini wasiwekeze kiwanda cha matairi ili tuiuzie serikali na wananchi binafsi matairi huku tuwapa wakulima wetu soko la uhakika la zao la mpira
Hata viwanda vya sukari = ajira ya watumishi wa kiwandani,wakulima wa miwa na kazi zingine zisizo za moja kwa moja.
 
Kuna kiwanda cha maana utachojenga kwa billion 200 kama sio madaraja na makaravati tu? tutumie ubongo kidogo.
Mkuu kuna small and medium industries, inawezekana kabisa - hata hio 200bn ni kubwa mno, kama unayo hio cash ni pm tupige kazi.
 
Kuna haja vilaza kufahamishwa maana na matumizi ya maneno "NA" na "AU".
 
Wanaolidharau Daraja la kigamboni nadhani hawajawahi kupata dhiki kwenye kivuko (pantoni)au hawapajui kigamboni japo kuwa wanaishi Dar-es-salaam.
Watu wenye magari walikuwa wanapoteza muda mwingi kuvuka kutoka upande umoja kwenda mwingine si chini ya saa mbili kiwango cha chini. Mtu anatoka kwake saa 10alfajir anarudi saa 3usiku,fikiria huyo mtu ni mfanyakazi ufanisi wake kazini ukoje?hapumziki! Hili tunalolibeza ni karavati huvuki BURE utalipa kwa kulitumia,jee karavati/daraja tunayotumia tunalipia?
Wanajamvi tuangalie mambo kwa upana zaidi tusimlishe Mhe Rais maneno haipendezi
 
Mkuu Obuma mwana JF yoyote haitaji specific software kupata taarifa kuwa katajwa jamvini,nenda kwenye settings ya JF utaona mfano huu hapa chini Nash
d0b46ef0da169d1f543e7006b1d32125.jpg

Chagua nini unataka hapo you'll be alert
Nashukuru mkuu
 
Mmh, hilo la kuanzisha viwanda bila utaalam/wataalam na utaalam wa usimamiz nalo ni tatizo kubwa. Ni afadhali kujifunza na kujenga uwezo kabla ya kuingia huko!

hujui unachokiongea na hilo ndo tatizo,
 
Sawa, je utafiti wa masoko. Halafu usichukulie suala jepesi kwa kuwa ni kiwanda cha ngozi, je kina tija? Soko lipo? Return? So kuna mengi ya kujiridhisha, tusije kuangukia tulipoteleza awali.

utahira unakusumbua, yawezekana huwa unaweka ugumu hata kwenye mipango yako, vinginevyo ww ni tatizo. #nyumbu.
 
Watanzania tunapenda sana kuchonganisha! Ametoa mfano tu sio lazima Tuka link na daraja la kigamboni! Pia nimeanza kumuelewa JPM kuwa huwa hana selection nzuri ya maneno au mifano! Inaoneka hiyo mifano huwa hajaandika kwenye notes zake!
Ni kweli kabisa,sijui kwa nini?yaani wabongo wanapenda sana kuchonganisha hata sielewi wao wanafaidika nini,wakati JPM kazungumzia mambo mengi tu ,likiwamo suala la wafanyakazi hewa,lakini hili wabongo hawakulisikia wamekuja na suala la daraja kwa kuwa wanajua wakilizungumzia hili litaleta misuguano na majibizano ya kijinga ambayo ndo wanafurahia,si ajabu upuuzi huu ukaukuta kesho kwenye gazeti kurasa za mbele ikawa lead story.
 
Hiyo sentensi ya mwisho CC ndiyo imenivunja mbavu, Yaani FaizaFoxy utamuona soon hapa jamvini na ujiandae.Aisee nashindwaga kujua amejitendenezea software ambayo ameintegrate na JF kuwa akitajwa tu imualert. Ukiangalia na ukimsikiliza vizuri Raisi utagundua alilenga mfuko gani wa jamii, ni wazi aliulenga mfuko wa NSSF na alilenga daraja la kigamboni aliloagiza lipewe jina la Mw.Nyerere.Na ukiwa mzalendo wa kweli Raisi yuko sahihi kabisa.Watu wamekazana kuwekeza kwenye madaraja na majengo ambayo return yake ni ndogo wanacha kuwekeza kwenye viwanda na miradi ambayo itainua uchumi wa nchi kwa haraka na kutoa ajira nyingi za kudumu kwa vijana. Ila hii miradi ya maraja,makalavati na majendo ina ulaji wa maana sana.

Ulianza vizuri
 
Back
Top Bottom