Ndugu yangu mimi nilikuwa huko miaka ile ya 80s wakati MWATEX imepamba moto sana pale NYAKATO!
Na biashara ya pamba ndio ilikuwa kileleni kabisa.
Stand ya basi ilikuwa bado ni vumbi na matope matupu!
Na mabasi maarufu wakati huo yalikuwa ni tanganyika bus. Na moja nakumbuka pale mjini lilikuwa limeandikwa "geza ulole!"
Those were Good old days.
Kahtaan,
Salaam.
Nilichungulia hizi
bayana zenu tangia majuzi,nami pia mumenipeleka mbali mno...
Shukran nyingi zikufikeni juu yenu
Maulamaa wangu!
Mimi binafsi nina hakika yakuwa sisi
soote lazim itakua tunafahamiana uzuri tu,au itakua
families zetu zajuana kitambo kingi!?...Wallahi,ni
raha ilioje! Kwi! Kwi! Kwi!
Nakumbuka kitambo ilikua
family yetu ikitembeleana mno na family ya
Al Marhum Balozi Idd Mtingwa pale
Mwanza. Yule Bwana alikua ni
Sahib mkubwa mno wa
Mzee Wangu.
Mara zoote tulipokua
waduchu tukifikia kwake pale
Mwanza,halikadhalika nao pia ilikua wakifikia nyumbani petu hapo
D'salaam.
Kuna wakti nilikua nikizungumza na Shariff
Ritz humu ,yeye ndo alonambia yakuwa kumbe yeye Balozi Mtingwa alikua ameoa kwa
Al Marhum Sheikh Al-Amin pale
Mwanza!?
Pia alinifahamisha yakuwa,yule
Rukia Mtingwa ndo yupo pale Vodacom D'salaam. Mimi nilikua nikimkumbuka zaidi yule
"Masele",dah! Yaani kitambo kingi sijakutana na hawa
ndugu zetu maskini!
Lakini pia nakumbuka
Shariff Abdallah Al Attas,pia kuna wakti alikwenda
Mwanza na kumposea/kumuoza
Alhaj Issa Mtambo. Najua
Mzee Wangu alikuamo kwenye ule msafara wa
Bwana harusi!
Nafikiri itakua basi wamfahamu yule
Abass,aliekua akichezea
Pazi Basketball Team,enzi ile pale
Gymkhana Club!? Nafikiri huyu ni jamaa zao katika ile family ya
Mwanza alokwenda kuoa
Alhaj Issa Mtambo!?
Nakumbuka pale
Mwanza pia palikua na family ya yule
Al Marhum Jumbe Mkila,huyu Bwana nafikiri alikua na asili ya
Bagamoyo!?
Lakini aliishi kitambi kingi pale
Mwanza,wakti ule pia alikua ni mmojawapo ya
Wafanyibiashara wazuri pale
Mwanza khasa kwenye mambo ya
stationeries. Baadae yule
Nyerere na yule mpuuzi mwingine
Moringe Sokoine walimtia ndani ati kwa yale makhanatha ya ule
"uhujumu wa uchumi"!?
Maskini,kutokana na utu uzima wake na
adhabu za kifungo kile cha kinafiki,alifariki nafikiri miaka michache baada ya kutoka
kizuizini!
Dah! Yaani
Nyerere kaadhibu mno
Wazee Wetu,takriban katika kila pembe ya hiyo
Tanganyika na katika
awamu tafauti za utawala wake alituletea
nakma/dhuluma za kiaina nyingine!
Mara ya mwisho binafsi kufika
Mwanza ilikua kitambo kiduchu,nilifikia kwa family friend wetu/rafiki ya Mzee Wangu Mr Mwinjuma ndie aliekua
GM wa ile
MWATEX pale!
Pia nina hamu kubwa mno ya kurejea tena pale
Tabora. Niliwahi kufika kitambo kingi mno.
Mara ya mwanzo ilikua kwenda kushuhudia wakti ule Mwenyekiti wa
CCM Al Rais Bwana Ali Mwinyi,alipokwenda kuhutubia na kumpigia kampeni ndugu yetu Rostam Aziz,alipokua ndo anagombania ule ubunge wa
Igunga kwa mara ya mwanzo!...lakini mie sina chama chochote cha
kisiasa! Kwi! Kwi! Kwi!
Tabora pale pana
personal memories nyingi mno za
family yangu.
Babu zangu woote wa pande zote mbili(kuumeni na kikeni),walisomea na kuhitimu pale
Tabora tangia enzi ya
Mjarumani.
Kuna wakti pia Mzee Wangu,alifuata
foot steps naealisomea pale.
Napata khadith zilo
njema mno za ndugu zetu
/Wazee Wetu wa
Tabora na
Mwanza na kwingineko
koote ndani ya
Tanganyika kila mara nizungumzapo na
Mzee Wangu. Hishma,mapenzi na tashrif nyingi mno alizopawa wakti mbali mbali wa shughuli zake
kikazi na matembezi
binafsi pia. Allah'amdulillahi...
nafarijika mno nikiona/kusikia
mshikamano mkubwa kama huu.
Mara ya mwisho kufika
Tabora mimi binafsi,tulikwenda kumtembelea
Lawrence Gama,wakti ule ndo alokua
RC pale.
Huyu
Mzee Gama,alikua ni mtu
mstaarabu na
mnyenyekevu mno. Nakumbuka ilikua ni
Al Jumaa tupo pale
Tabora.
Basi alitupeleka
Masjid mimi na Mzee Wangu...na akatusubiria yeye na
Driver wake mpaka
Sala ilipokwishwa/ilipokamilika ndo tukarejea nae pamoja! Dah!
Yaani,kitambo palikua na watu
waungwana mno...lakini amefariki maskini!
Nakumbuka siku ya pili yake bado tupo pale
Tabora,akaja yule kichaa mwingine
Augustine Mrema ati kukamata
"mafisadi"!?
....hiyo story na
vitimbi alivyofanza yule
Mrema pale
Tabora ni kichekesho na utacheka pita kiasi
Akhiy! Kwi! Kwi!
Afrika bana... yaani mpaka leo
nastaajabu mno,ilikuaje mpaka
Rais Mwinyi kumpa
kanjanja kama yule wadhifa/cheo cha
Naibu-Waziri Mkuu!? Dah!
Yuwapi
CHAMVIGA nae,nimpe khabar nilipopeleka "posa" yangu pale
Soni!? kwi! Kwi! Kitambo enzi ya
"ujahil" nalikua na mchumba kiduchu na kibarua chake alikua ni
askari/Traffic pale
Soni!? kwi! Kwi!
Hii
story ni ndefu na ya kuchekesha mno
Akhiy...mpaka siku tukikutana kwa furaha zetu
Insha Allah.
Yaani pia napapenda mno poote pale
Mazinde,Mombo,Lushoto,
Soni,Kilindi,Vunjo na vijiji/maeneo mengi mno yazungukayo huko.
....miaka ya
early 1950's,Babu yangu alifanza maskani/makao yake pale
Mazinde na alikua na
biashara kubwa mno,
kilimo/ardhi kubwa/nzuri...na pia akijulikana na kuheshimikana koote takriban kwenye maeneo hayo.
Kila
Vijiji alivyokua akipita nduguze/
Wazee Wetu wa maeneo hayo walikua wakimtaka/wakimnasihi aongeze
Mke kutoka kwao! Kwi! Kwi!
Lakini ilipofika ile
nakma ya yule
Nyerere,ule utumbo wa
"Azimio la Arusha"-1967,"tulitaifishiwa"/tulidhulumiwa takriban nusu ya hiyo
biashara/kilimo choote...wajua
Babu yangu maskini haikuchukua muda mwingi
alifariki maskini kwa joto la roho! Dah!
Khalaf,ati wanatokea
brainwashed/mashangingi wa hoja humu
JF,ati kutaka kunirubuni kwa hoja zao
dhaifu ili nimpende yule khabith/maluuni
Nyerere!? Thubutu thuma thubutu!!
Life is short...je nikuulize khabar za Mukaram,Sharjah,Seiyun au Sheibam mwenzetu!? kwi! kwi!
...nimefurahika
Akhiy,hiyo
offer ya
kumuongeza Mke ndugu yetu Maulana Al Duktuur
Kahtaan....lakini,naona keshajifanza kukwepa kiduchu,italazim tumfanzie
hila zoote mpaka
atimize wajibu huo wa
kiungwana! Kwi! Kwi!
Wallahi,
nimefurahika mno tumezungumza japo kiduchu.
Ahsantani sana.