Lakini TanZania siyo nchi iliyoendelea usisahau hilo kwanza!
Mradi wa DART siyo mbaya ila tatizo ni kwamba tu haueleweki, watu wengi hawauelewi, lkn ni mradi mzuri sana na ungesaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza adha ya usafiri, hata nchi zilizoendela pia zina miradi kama hii, miji mingi tu Duniani inatumia mradi kama Dart, kwa kifupi ni kwamba Dart ni kama vile kuweka trams sema kwa gharama nafuu trams ni ghali zaidi na mazingira ya nchi yetu bado hayaruhusu kuwa na trams na mfano ni mdogo tu Umeme, trams zote au nyingi zinatumia umeme sasa umeme wenyewe wa kukati kakatika unawezaje kuendesha treni kwa ufasaha? na isitoshe nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 na inatumia MW 1500 tu huwezi kutumia huwo kuendesha treni za Umeme na haya yote waliyaafikiria wakati wanabuni huu mradi!
Lakini kwa ngazi ya maendeleo ya nchi yetu DART ni mradi mzuri sana na ungesaidia kwa kiasi kikubwa kama tungeuelewa vizuri!