Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Mabilioni yaliyowekezwa kwenye Ujenzi wa hili Daraja ni kama yamepotea bure kwa maana halihitajiki, halina umuhimu mkubwa kiasi hicho kwa maana ya kwamba halitasaidia kuboresha maisha ya wakazi wa Dar kwa walio wengi ukilinganisha na gharama ya Ujenzi wake hii ni prestige project ambayo kwa nchi masikini na yenye kila aina ya shida inayojulikana na binadamu hapa Duniani hatukupaswa kulijenga badala yake hizi fedha zingewekezwa kwenye miradi mikubwa kama DART kwa mfano hii fedha ingetosha kujenga DART nyingine kutoka Mwenge mpaka Kivukoni hivyo kuwa na DART mbili ambazo zingesadia sana wakazi wa Dar, kuliko hili Daraja!
Itatuchukuwa muda sana sisi Watanzania kuja kuendelea, mpaka tuje tuweke vipaumbele vyetu sawa tuna safari ndefu sana, mradi mwingine ambao nasikia uko mbioni na namwomba Rais Magufuli auzuie huu mradi kama ule wa bandari ya Bagamoyo ni wa kujenga daraja baharini ktk daraja la Salenda kuunganisa na Coco Beach, hili daraja hatulihitaji badala yake hizi fedha ziende kujenga DART nyingine labda ya Br. ya Mandela- Buguruni -Kariakoo!